Katiba ya Muungano wa Tanzania Baada ya Uhuru
KATIBA ni sheria au kanuni zinazoainisha jinsi ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao. KWA UPANDE WA WANANCHI, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali. Katiba za nchi pia huainisha haki za msingi za wananchi. Kuna aina kuu mbili za Katiba (a) Katiba isiyo ya maandishi (ya kimapokeo) (b) Katiba ya maandishi.
Mabadiliko ya Katiba mwaka 2005
Sheria ya mabadiliko ya Kumi na Nne katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mabadiliko ya Katiba mwaka 2000
Sheria ya kufanya mabadiliko katika Katiba ya Jamhuri ya Muungani ili kurekebisha mambo kadhaa kutokana na maoni ya wananchi.
Mabadiliko ya Katiba mwaka 1995
Sheria ya kufanya mabadiliko katika katiba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kufafanua masharti yahusuyo viongozi wakuu nchini, kuweka misingi ya maadili katika Utumishi wa Umma na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Mabadiliko ya Katiba mwaka 1992
Sheria ya kufanya mabadiliko katika Katiba ya Muungano wa Tanzania ili kuweka masharti mapya ya uteuzi wa mgombea pekee katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar
Mabadiliko ya Katiba mwaka 1990
Sheria ya kufanya mabadiliko katika Katiba ya Muungano wa Tanzania ili kuweka masharti mapya ya uteuzi wa mgombea pekee katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar
Mabadiliko ya Katiba mwaka 1982
Kufanya mabadiliko katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya kuweka utaratibu upya wa uteuzi wa Wakuu wa Mikoa
Mabadiliko ya Katiba mwaka 1980
Sheria ya kubadilisha baathi ya masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, kwa madhumuni ya kubadilisha idadi ya Wabunge waowakilisha wilaya za uchaguzi ili idadi mpya ya Wabunge iwe sawa na idadi mpya ya wilaya za uchaguzi
Katiba Mpya mwaka 1977
Katiba mama ilipatikana kwa udhamini wa baba wa Taifa ikiwa ni katiba ya kwanza kuanza kutumika kwa nchi yetu.
~ Mwalim J.K. Nyerere
Latest Publications
Read our latest news. Be always in trend with daily news.



