MASWALI NA MAJIBU YA MWENDELEZO WA MJADALA JUU YA KUMBUKUMBU YA MUUNDO WA KATIBA YETU NA HISTORIA YAKE..MJADALA UNAENDELEA
[06:59, 13/05/2023] A: Nimejaribu kufatilia kwa kina mjadala bado nimeona ipo haja kubwa mno wanachi kupewa elimu ili kuielewa kwa upana katiba tuliyonayo kuelekea ktk mpya kimsingi wananchi hawana uelewa mzuri wa katiba iliyopo kwa mantiki hiyo kutakuwa na ugumu wao kuchangia ktk upatikanaji wa katiba mpya ikiwa ya zamani hawaielewi [07:35, 13/05/2023] +255 783 157: Sisi tunataka katiba ile ya warioba. Anania njema kuliko ile rasimu ya Bunge iliyojaa maslahi ya wanasiasa. [07:41, 13/05/2023] A: ktk kupata kuna michakato ambayo ipo kisheria ktk kuchakata kuanzia ukusanyaji wa maoni hadi bunge la katiba,ndipo nikasema ipo haja ya wanachi kupewa elimu ili kuielewa katiba hii tulioonayo ili waweze kutoa maoni kwa ufasaha baada ya kuona mafungufu ambayo yakipatiwa ufumbuzi kwa faida ya afya ya Taifa kwa ujumla [07:58, 13/05/2023] +255 62: Mpaka watu tukaenda kutoa maoni kwenye ile ya jaji wariomba bado tulikua hatuelewi tu?Hata ukianza saiz kuelimisha watu kuhusu katiba bado kunawengine kwa makuaudi kabisa wataamua wasichukue hiyo elimu ila kwakua wengi kwasasa wanayo iyo elim na watu wameshiriki kutoa maoni Yao tusipoteze muda ikashindwa kukamilika kwa wakat tuendelee na ile ya Jaji Wariomba
[08:13, 13/05/2023] P: Ukisema hivi, na mimi naomba niulize; kwani hiyo katiba ya zamani wangapi wameiona? Wangapi wameisoma? Lini Iliwahi kusambazwa kwa wananchi wakashindwa kuisoma?Na hao “wananchi wengi” tunaosema “hawajui katiba” ni akina nani hasa? Je, ni sisi tuliopo hapa mtandaoni au watanzania kwa ujumla?
Maana kama wengi wetu hapa hatuijui na hatuwahi kuiona ya zamani, achilia mbali kuisoma na kuielewa, je, hao wananchi wa kawaida huko mtaani inakuwaje?
Kwa mantiki hiyo ya “universal ignorance ya katiba”, wanaotegemewa kujadili na kutoa maoni yao na yachukuliwe serious, ni akina nani hasa? Maana sehemu kubwa ya watanzania watakuwa hawajui katiba ya zamani, na hata hii ya sasa ni wachache wamewahi kuisoma seriously kifungu kwa kifungu.
Kwa uzoefu wa kawaida, Katiba nzuri, huandaliwa na watu wacheche sana wenye weledi wa kiwango fulani cha mambo sheria, siasa, na utawala. Sehemu kubwa ya wananchi wa kawaida hushiriki m kutoa maoni yao tu wkt wa kukusanya maoni. Baada ya kukusanya maoni ya wenye nchi, hakunaga tena hizi gimmicks za kujizungusha zungusha.
Hata sisi Tanzania tumefanya haya, tena kwa ushirikishaji mpaka sana wa wananchi nchi nzima. “Rasimu ya matakwa ya wananchi” ipo intact kabisa.
Kinachotakiwa sasa hivi siyo kurudia tena kukusanya maoni, kwani tunataka maoni gani zaidi, ya nani, na kwa ajili gani?
Kinachobaki hapo ni timu ya watu wachache tu wenye sifa nilizotaja hapo juu, kujifungia mahala; kuchambua, kuchakata, kudadavua, na kuja na majibu ya kutukwamua tulipokomea last time, that’s it.
Nilidhani lengo la Rais kuunda Timu Kazi, na baadae kum task Msajili wa vyama na kazi ya kuwaita wanasiasa ili wakae na (timu kazi?) Ilikuwa ni kufufua tu kilichokuwa kimetaka kufishwa ili kiendelee kupumua na kuidhi.
Leo tunapianza mijadala ya kuhimizana kutoa maoni tena najiuliza: kumbe tayari imeshaamriwa kwamba mchakato wa kwanza ulikuwa batili, na kwa hiyo muda na gharama iliyotumika tuhesabu ndio tumeliwa?
Au kuna nini ambacho mimi sielewi? 🤷🏾♂️

Wazo langu bado elimu ya uraia inahitajika sinauhakika kama wananchi tunaijuwa katiba kutoka kava yake mpaka ukurasa wa mwisho,
1. Katiba ni nini
2. Kunaumuhimu gani wa kuwa na katiba
3. Je katiba iliyopo ina matatizo gani
4. Kwa nn tunahitaji katiba mpya
Najaribu kuyaeleza haya kwan masuala mengi yakiwemo haya wananchi wengi wanajiliza na kwa bahati mbaya hakuna jibu ambalo litamuezesha mwananchi wa kawaida kutoka hapa tulipo na kuingia katika hiyo mijadala ya katiba.

Elimu inahitajika na nishauru serikali zetu zote mbili kuvihusisha vyombo v…
[10:22, 13/05/2023] A: Hayo maswali manne ni muhimu mno lkn hata ukifatilia hao wanaojita wana harakati wote ni watu Dar Mjini ukiukiza uwakilishi wa wakulima huko vijivini uko wapi hupati jibu na hakuna mwaharakati hata mmoja wa nyamisati au kibondo wote ni wamjini wapiga dili [10:26, 13/05/2023] +255 : wakibondo tupo wasomi… tunawakilisha… ila naonga mkono hoja… wafikiwe wote kama zinavyopitishwa sheria ndogo za halmashuri inamaana mikutano ya wananchi kwenye vijiji na mitaa ifikiwe na kwenye kata. Maana sio wote wako kwenye mitandao wala kusikiliza radio.. [10:29, 13/05/2023] A: sasa nini tufanye ili kufikia malengo?..Mjadala unaendelea………….



