3. Kongezwa kwa upana wa uelewa kwa vyombo vingine vya haki na sheria
Muhadhara huu kwa ujumla wake unaleta umuhimu katika kukuza uwajibikaji, uwazi na uelewa wa umma kuhusu masuala ya sheria na haki nchini Urusi na hata kwa mataifa mengine.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash ameagiza kufungwa kwa Taasisi ya Mango Kinder iliyopo Kata ya Dunda Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya kituo hicho kukiuka utaratibu wa leseni yake ya kutoa haki kwa Watoto na badala yake kuwakusanya Watoto zaidi ya 200 na kuwapa elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo yaliyo kinyume na maadili ya Mtanzania chini ya ufadhili wa Raia wa Ujerumani.
Kituo hicho huwakusanya Wanafunzi kuanzia saa nane mchana hadi saa 12 jioni na kuwapikia chakula kisha kuwafundisha masuala mbalimbali bila ya kibali ambapo DC Halima ameagiza pia kusitishwa kwa kibali cha Taasisi hiyo na leseni na ameitaka Kamati ya Usalama kuondoka na Mmiliki wa Taasisi hiyo Mtanzania Franky Silvester Neumann na Timu yake akiwemo Mke wa Franky ambaye ni Raia wa Ujerumani ili wakahojiwe zaidi.
Awali wakati wa mahojiani yake na DC, Franky amesema “Mimi nilikuwa Ujerumani nikawaambia Tanzania nina Watoto hali yao sio nzuri, wakanipa ufadhili Euro 1000 kila mwezi tuwe tunawapikia Watoto chakula, wakimaliza wanasoma msomo mbalimbali”
DC Halima amesema “Tumekuta zana mbalimbali ambazo inatupeleka kugundua Watoto hawafundishwi maadili mema na mengi ya mambo wanayofundishwa ni mambo ya kijinsia ambayo yanakiuka taratibu na mila na desturi zetu”.
“Nimeelekeza tutasitisha kibali na leseni ya Taasisi hii na wote wanaohusika na Taasisi tutaondoka nao kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi lakini hili eneo halitotumika tena, hawa Watoto tangu November mwaka jana wanakuja hapa na Watu hawatoi taarifa kwa wakati, utamaduni wa kwetu wanaenda kuubadilisha”
Mkutano unahakikisha kuwa maoni ya vyama vyote vya siasa, na wananchi yanapewa uzito na kuzingatiwa katika kutengeneza sheria mpya. Ushirikiano wa wadau wote unaboresha uwazi na uwajibikaji, kuhakikisha kuwa mchakato wa kisheria unafanyika kwa njia inayowakilisha maslahi ya jamii
MBUNGE wa Viti Maalumu, Neema Lugangira ameshauri Mswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi uwe na Ibara inayoongelea masuala ya Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi ikiwemo (Akili Mnemba – AI)
“Kikombe tulichonyweshwa kuanzia mwaka 2015 hakuna Mtanzania ambaye atakisahau. Mimi ninavyoona hapa tuanze na maridhiano (reconciliation). Hizi R4 zifafanuliwe vizuri na Watanzania waelewe. Maridhiano yasiwe kati ya chama na chama, maridhiano yawe ni yawatanzania na siyo kati ya chama na chama. Naomba kuwe na semina maalum ya hizi R4 ili zieleweke” Bw. Joseph Thelasini.
“Chochote kinaandikwa kwenye Sheria haipaswi kuwa na mashaka juu ya mamlaka ya Mhe. Rais. Hatuwezi kutengeneza nchi chini ya mashaka, ni vema kumuamini Rais chini ya vyombo vyake. Ni vema tuamini kuwa kuna Watumishi wa Umma ambao ni waaminifu maana wanapitia michakato. Tumesema kuwa Tume itakuwa huru, tumeshaandika kwenye sheria kuwa Tume itakuwa huru, hii inatosha hatuhitaji maneno mengine. Watumishi wasiwe waoga kwakuwa watu wengi wanasema kuhusu jambo Fulani (tunaondoa paradox), tutunze ustahimilivu (Resiliency)” Bw. Thabiti Mlangi;
Mkutano ulianza na ufunguzi uliofanywa na Mhe. Othman M. Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao kilianza na salaam za utangulizi na viongozi mbalimbali, ikijumuisha Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu.
Mada kuu ya kikao ilikuwa mswada wa sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, na matokeo ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika awali.
Maoni ya Wadau
Wadau mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu mswada huo.
Bw. Majaliwa Kyala aliipongeza Serikali kwa kuondoa kifungu cha mgombea binafsi na kuelezea umuhimu wa kusimamia uchaguzi wa Serikali ya Mitaa.
Bi. Nuru Kimwaga aliipongeza Serikali kwa kuwaunganisha wanasiasa na kutoa wito wa kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika Tume ya Uchaguzi.
Bw. Hassan Almasi alikumbusha historia ya miswada ya sheria na umuhimu wa kuzingatia maoni ya wadau.
Bi. Neema Lugangira alisisitiza umuhimu wa matumizi ya mitandao katika uchaguzi na kutoa wito wa kuimarisha usalama wa kadi za kupigia kura.
Prof. Ibrahimu Lipumba alitilia mkazo umuhimu wa kufanya marekebisho ili kutatua matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Mzee Cheyo alisisitiza umuhimu wa kuwa na Tume inayojali maoni ya wananchi na kutunza mila na desturi.
Bw. Abdul Nondo alitoa mapendekezo kadhaa kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi na jinsi ya kuboresha mswada.
Bw. Thabiti Mlangi alisisitiza umuhimu wa kumuamini Rais na kudumisha ustahimilivu wakati wa uchaguzi.
Majumuisho ya Maoni ya Washiriki
Dkt. ADA alitoa maoni kuhusu rushwa ya ngono na umuhimu wa kuwajengea uwezo wanawake.
Bw. Baruani Mshale kutoka TWAWEZA alipendekeza kuunganisha mswada na kufanya marekebisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuhusu matumizi ya teknolojia.
Washiriki wengine walitoa mapendekezo kuhusu uteuzi wa wajumbe, sifa za wagombea, na mchakato wa kusikiliza kesi na rufaa.
Hitimisho
Kikao kilifungwa na Dkt. Doto M. Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Mada zilizojadiliwa zilikuwa kuhusu sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, na washiriki walitoa maoni yao kwa kina kuhusu mswada huo.
Mgeni rasmi alikuwa Bw. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
HIVYO BASI
Mjadala ulionyesha umuhimu wa kufanya marekebisho katika sheria za uchaguzi na vyama vya siasa ili kuboresha mchakato wa uchaguzi. Kuna haja ya kuzingatia maoni ya wadau wote na kuhakikisha kwamba mabadiliko yanafanyika kwa njia inayosaidia demokrasia na usawa wa kijinsia.
Mkutano ulilenga kuimarisha demokrasia na kuleta maridhiano kati ya vyama vya siasa. Kauli mbiu ya mkutano ilikuwa “Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia.” Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na wadau katika mkutano huo ni pamoja na dhana ya R4 (Reconciliation, Resiliency, Reforms, Rebuilding), misingi ya kutengeneza dira, na nafasi ya R4 katika kuleta utendaji mzuri wa hali ya kisiasa.
Watoa mada walisisitiza umuhimu wa maridhiano na uelewa wa pamoja kati ya vyama vya siasa, na kueleza kuwa tofauti za kiitikadi hazipaswi kuvunja umoja wa nchi. Pia, walijadili misingi ya kutengeneza dira, ikiwa ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, kujenga upya, kuvumiliana, kusameheana, na maridhiano.
Watoa mada walisisitiza pia umuhimu wa kufanya marekebisho katika sheria za uchaguzi na sheria za vyama vya siasa. Waliongelea mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, uchaguzi, na demokrasia, pamoja na kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya. Waliomba pia uwiano wa jinsia na uwiano wa umri katika mchakato wa kisiasa.
Wakati wa majadiliano, wadau walitoa maoni yao kuhusu jinsi R4 zinavyoweza kuchangia katika maendeleo ya kitaifa, kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 na Ajenda ya 2063. Walisisitiza umuhimu wa kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia na kufanya marekebisho katika mifumo ya elimu, siasa, na utamaduni ili iendane na uchumi wa nchi.
Mkutano pia ulijadili nafasi ya serikali, asasi za kiraia, na vyombo vya habari katika kusaidia utekelezaji wa R4. Baadhi ya washiriki walitoa maoni yao kuhusu jinsi wananchi wanavyoelewa R4 na umuhimu wa kuona matokeo ya sera na mikakati inayotekelezwa.
Katika mchana wa siku hiyo, washiriki walipata fursa ya kusikiliza mada kutoka kwa wataalamu na kutoa maoni yao kuhusu marekebisho ya sheria za vyama vya siasa na gharama za uchaguzi. Wadau walizungumzia changamoto zinazowakabili wanawake katika siasa, pamoja na kutoa mapendekezo ya kuboresha sheria na taratibu za uchaguzi.
Hitimisho la mkutano lilisisitiza umuhimu wa kulinda utulivu na kudumisha maridhiano, na washiriki walitoa ombi maalum kwa vyama vya siasa kuhusu marekebisho ya sheria na ushiriki wa wanawake katika siasa.
Niliposema ‘reform’ sikuwa na maana tuanze na reform. Hivyo ni lazima tuanze na maridhiano na kuvumiliana. Nakubaliana na wote wanaosema kuwa R4 ni falsafa sahihi sana. Hii mimi ninaamini kuwa hii itakuwa ni ‘legacy’ kwa mama Samia. Nini kifanyike, tuione Serikali ikifanya kwa vitendo, hili sio suala la kisiasa. Tunaona mabadiliko kwenye mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali. Ingawa kwenye siasa kuna mkwamo kwenye Sheria za Uchaguzi na Katiba mpya. Asasi za kiraia ziwaeleze wananchi na kuwafundisha.
Bw. S.Wasira.
Vyombo vya Habari vifanye kazi yake ya kuelimisha umma kwakuwa vinasilikizwa na Wananchi. Nafasi ya Serikali ni haya yanayoendelea, Serikali iko kwenye usahihi. Tutazame ‘reforms’ kwenye maeneo yote kwa mfano elimu, vyama vya siasa vina nafasi ipi.
Bw. Ado – ACT WAZALENDO.
Mchakato wa Katiba nchi siyo jambo la kusubiri, mchakato wa Katiba mpya na ukamilike mapema baada ya uchaguzi mkuu. Mhe. Rais hakuwa na shinikizo lolote baada ya kichapo cha mwaka 2020, kwa hiari yake akaamua kufanya mabadiliko. R4 itapimwa kwa vitendo, kila mmoja wetu ana wajibu. Ingawa yako mambo ambayo yameshajenga mambo ya kitaifa. Sisi kama ICT Wazalendo tumechambua mambo ambayo yameshatekelezwa. Mengi yapo kwenye ripoti ya kikosi kazi, hivyo yaendelea kutekelezwa.
Bi. Mongela.
S5 za Japani zimewezesha maendeleo ya Japani. Hivyo na hili la R4 tunapaswa kufanyia mkamkati, tunapaswa kuitengenezea dira ili iwe ya Taifa. Tumuombe Mhe. Rais tulitoe mkononi mwa Mhe. Rais kisha tukimbiee nalo. Mimi natoa mapendekezo hizi R4 ziwe za umma na ziweze kwenda hata kwenya familia. Naomba kuwe na muendelezo ya kufikisha kwa kila mtu yaani Methodolojia, tukumbatie vile ambavyo tumeshavifanyia kazi.
Bw. Doyo.
Naomba kuungana na Mhe. Lipumba, ni vema wenzetu wa Serikali wakalichukua hili. Kuhusu ajenda 2063, Mhe. Rais ameruhusu mwanamke aongoze mwanamke mmojammoja kwenye baraza ili washiriki kisheria. Nawaomba tutumie R4 kwenye mjadala huu.
Naomba nianze na nia ya Mhe.Rais, nianze na Watendaji wa chini. Serikali itengeneze programu maalum yakuwafanya hawa Watumishi wa Serikali wazielewe vizuri R4. Dira ya Taifa ikieleweka tutapata Wawekezaji pia. Mhe. Rais anasisitiza kusikilizana na kutuvumilia. Hivyo kuna umuhimu watendaji wawe na uelewa.
Bw. Salim
Kwa kiwango gani R4 zinaweza kuisadia kuendana na Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda za 2063. Haya yote yanapaswa yaangaliwe na nguzo za kidunia, ili dunia itupime hivyo. Kama kuna joto kubwa la kisiasa hautaweza kufikia kwenye haya maendeleo. Reforms zinazozungumzwa hapa ni pamoja na kuvumiliana kwa hoja ilituweze kuitengeneza nchi yetu, tunapaswa kuja na reforms za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivyo tuweze kupimana kwa uvumilivu na ukweli.
Bw. Ado Said
Falsafa hii ikitekelezwa kwa ukamilifu basi tutaenda sambasamba na Ajenda ya 2063 na Maendeleo Endelevu ya 2030. Maridhiano ni sawa, ila nguzo mama ni Mabadiliko. Ni lazima sasa hii nguzo mama hii iendane na nguzo ya Katiba Mpya, Mchakato wa Katiba Mpya uanze hivi sasa na kuweka misingi madhubuti ya kisheria. Pamoja na kujadili miswada hii, lakini bado hatuna kalenda za utekelezaji wa Tume ya Haki Jinai na Kikosi Kazi, tunataka kuwa na kalenda, tunahitaji muafaka wa kitataifa. Mambo ambayo yameshapata muafaka wa kitaifa badi yatekelezwe. Kuhusu mifumo ya ruzuku bado ina shida, hivyo tufanye mabadiliko ya kimfumo. Tuwe na Kalenda ya utekelezaji.
NAFASI ZA R4 KULETA UTENDAJI MZURI WA HALI YA KISIASA
Bw. Ado
Mhe. Rais amezichukua hizi R4 kama nyenzo yake muhimu yakufanyia kazi. Maboresho ya kisiasa yaweze kukidhi haja ya Watanzania wote. Kwakiasi gani Wananchi wanaulewa kuhusu R4 za Mhe. Rais;
Sisi Wanasiasa tumeleewa vizuri sana kuhusu 4R na ndio maana tumekuwa tukishiriki kwenye meza ya mazungumzo. Hivyo hata uwepo wetu hapa unaonesha kuwa kumeelewa vizuri kuhusu hii R4. Mhe. Rais ametuonesha utashi wake na sisi tumeonesha kuwa tunamuamini. Hivyo tujenge misingi imara ya kikatiba na kisheria.
Bw. Salim.
Wananchi hawataki kuelewa kuhusu R4 ila wanataka kuona matokeo ya R4. Hivyo nguzo kuu ni Reforms, hivyo tunahitaji matokeo ya R4 na siyo mahubiri yake ya R4. Matokeo kwenye uchumi, ajira ubora wa elimu, tija ya kiuchumi, umasikini wa kipato unapungua. Tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa kisiasa, tuwe na tume huru, kujenga ,msingi wa kitaifa kuhusu kuwa na Katiba Mpya. Hivyo Watanzania tunaweza kuanza kukata tamaa. Dhamira ipo, hivyo tumsaidie mwenye dhamira ili tupate matokeo. Hivyo wananchi wataelewa baada ya kuona matokeo.
Bw. Doyo.
Kama unadai mkono na ukarudishiwa kodle basi utashukuru. Lapili, Watanzania hawa wanaelewa sana R4 za Mhe. Rais, kabla ya R4 kulikuwa na Mahabusu ambao walikuwa wanaonewa. Hivyo tuipongeze Serikali kwa kupeleka hii miswada kwa njia ya kawaida, kama ambavyo Mhe. Waziri amesema kuwa tutapokea maoni yote ya Wadau. Wote tumeona kuwa mada ni kujadili ajenda. Hivyo tunaomba tuweke maoni yetu sasa. Hata kuruani hakiundikwa kwa siku moja, tunapaswa tuige mifumo ya kiroho, haya mambo ni mchakato.
Bi. Mongela.
Naomba nitumie mfano wa kutaka mabadiliko ya katiba, aya ya 12 na 13 imesema Binadamu wote ni sawa, hivi hii katiba itaniondelea hayo. Mfano mwingine wakati ule wa Rais wa Kwaza wa Taifa hili, Rais alikuwa anazungumzia kuhusu utofauti wa kipato. Ni lazima tujue hiyo katiba itaandikwaje, mkakati wake ukoje na italiwekaje suala la usawa wa Mtanzania.
Jambo lingine ni hili la R4, juzi nimewaeleza kuwa naenda kwenye R4 watu walikuwa wananishangaa, hizi R4 ziwe za Mtanzania na zisiwe na Mama Samia. Tunapaswa tutumie Kiswahili, bado tuna kazi yakuwaelimisha Wananchi kuhusu R4.
Bw. S.Wasira.
Uelewa wa Wananchi kuhusu R4.
Nimesisitiza kuhusu Maridhiano (Recolianciation) ili turidhiane kwanza ndipo tufanye mabadiliko. Ni ngumu kuwa na ratiba yenye tarehe kwenye mambo makubwa ya nchi. Ni muhimu kuzungumza kuhusu Ustahimilivu (Resiliency), kuhusu Katiba hatuwezi kuwa na tarehe ya upatikanaji wa Katiba. Tutoe maoni yetu ilí ‘minimum reforms’ ifike mahali, tunapaswa kuwa na mchakato wa muda mrefu, mfupi na wa kati. ‘Reform’ haiwezi kutupatia majibu kesho.