Category: Siasa

MATUMIZI YA MITANDAO KATIKA UCHAGUZI YAINGIE KATIKA SHERIA

MBUNGE wa Viti Maalumu, Neema Lugangira ameshauri Mswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi uwe na Ibara inayoongelea masuala ya Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi ikiwemo (Akili Mnemba – AI)

Read More

HATUWEZI KUTENGENEZA NCHI CHINI YA MASHAKA

“Chochote kinaandikwa kwenye Sheria haipaswi kuwa na mashaka juu ya mamlaka ya Mhe. Rais. Hatuwezi kutengeneza nchi chini ya mashaka, ni vema kumuamini Rais chini ya vyombo vyake. Ni vema tuamini kuwa kuna Watumishi wa Umma ambao ni waaminifu maana wanapitia michakato. Tumesema kuwa Tume itakuwa huru, tumeshaandika kwenye sheria kuwa Tume itakuwa huru, hii inatosha hatuhitaji maneno mengine. Watumishi wasiwe waoga kwakuwa watu wengi wanasema kuhusu jambo Fulani (tunaondoa paradox), tutunze ustahimilivu (Resiliency)” Bw. Thabiti Mlangi;

Read More
JM

TATHIMINI YA KINA JUU YA MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA, UKIFAFANUA MJADALA MZIMA JINSI WADAU WALIVYOTOA NA KUCHANGIA MAWAZO YAO JUU YA MADA ILIYOWEKWA MEZANI 

(SIKU YA PILI)

UFUNGUZI 

 Mkutano ulianza na ufunguzi uliofanywa na Mhe. Othman M. Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kikao kilianza na salaam za utangulizi na viongozi mbalimbali, ikijumuisha Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu.

 Mada kuu ya kikao ilikuwa mswada wa sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, na matokeo ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika awali.

Maoni ya Wadau

Wadau mbalimbali walitoa maoni yao kuhusu mswada huo.

Bw. Majaliwa Kyala aliipongeza Serikali kwa kuondoa kifungu cha mgombea binafsi na kuelezea umuhimu wa kusimamia uchaguzi wa Serikali ya Mitaa.

Bi. Nuru Kimwaga aliipongeza Serikali kwa kuwaunganisha wanasiasa na kutoa wito wa kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika Tume ya Uchaguzi.

Bw. Hassan Almasi alikumbusha historia ya miswada ya sheria na umuhimu wa kuzingatia maoni ya wadau.

Bi. Neema Lugangira alisisitiza umuhimu wa matumizi ya mitandao katika uchaguzi na kutoa wito wa kuimarisha usalama wa kadi za kupigia kura.

Prof. Ibrahimu Lipumba alitilia mkazo umuhimu wa kufanya marekebisho ili kutatua matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Mzee Cheyo alisisitiza umuhimu wa kuwa na Tume inayojali maoni ya wananchi na kutunza mila na desturi.

Bw. Abdul Nondo alitoa mapendekezo kadhaa kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi na jinsi ya kuboresha mswada.

Bw. Thabiti Mlangi alisisitiza umuhimu wa kumuamini Rais na kudumisha ustahimilivu wakati wa uchaguzi.

Majumuisho ya Maoni ya Washiriki

Dkt. ADA alitoa maoni kuhusu rushwa ya ngono na umuhimu wa kuwajengea uwezo wanawake.

Bw. Baruani Mshale kutoka TWAWEZA alipendekeza kuunganisha mswada na kufanya marekebisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuhusu matumizi ya teknolojia.

Washiriki wengine walitoa mapendekezo kuhusu uteuzi wa wajumbe, sifa za wagombea, na mchakato wa kusikiliza kesi na rufaa.

Hitimisho

Kikao kilifungwa na Dkt. Doto M. Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Mada zilizojadiliwa zilikuwa kuhusu sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, na washiriki walitoa maoni yao kwa kina kuhusu mswada huo.

Mgeni rasmi alikuwa Bw. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

HIVYO BASI 

Mjadala ulionyesha umuhimu wa kufanya marekebisho katika sheria za uchaguzi na vyama vya siasa ili kuboresha mchakato wa uchaguzi.
Kuna haja ya kuzingatia maoni ya wadau wote na kuhakikisha kwamba mabadiliko yanafanyika kwa njia inayosaidia demokrasia na usawa wa kijinsia.

Read More
MIKONO

TATHIMINI YA KINA JUU YA MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA, UKIFAFANUA MJADALA MZIMA JINSI WADAU WALIVYOTOA NA KUCHANGIA MAWAZO YAO JUU YA MADA ILIYOWEKWA MEZANI 

(SIKU YA KWANZA)

Mkutano ulilenga kuimarisha demokrasia na kuleta maridhiano kati ya vyama vya siasa. Kauli mbiu ya mkutano ilikuwa “Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia.” Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na wadau katika mkutano huo ni pamoja na dhana ya R4 (Reconciliation, Resiliency, Reforms, Rebuilding), misingi ya kutengeneza dira, na nafasi ya R4 katika kuleta utendaji mzuri wa hali ya kisiasa.

Watoa mada walisisitiza umuhimu wa maridhiano na uelewa wa pamoja kati ya vyama vya siasa, na kueleza kuwa tofauti za kiitikadi hazipaswi kuvunja umoja wa nchi. Pia, walijadili misingi ya kutengeneza dira, ikiwa ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, kujenga upya, kuvumiliana, kusameheana, na maridhiano.

Watoa mada walisisitiza pia umuhimu wa kufanya marekebisho katika sheria za uchaguzi na sheria za vyama vya siasa. Waliongelea mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, uchaguzi, na demokrasia, pamoja na kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya. Waliomba pia uwiano wa jinsia na uwiano wa umri katika mchakato wa kisiasa.

Wakati wa majadiliano, wadau walitoa maoni yao kuhusu jinsi R4 zinavyoweza kuchangia katika maendeleo ya kitaifa, kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 na Ajenda ya 2063. Walisisitiza umuhimu wa kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia na kufanya marekebisho katika mifumo ya elimu, siasa, na utamaduni ili iendane na uchumi wa nchi.

Mkutano pia ulijadili nafasi ya serikali, asasi za kiraia, na vyombo vya habari katika kusaidia utekelezaji wa R4. Baadhi ya washiriki walitoa maoni yao kuhusu jinsi wananchi wanavyoelewa R4 na umuhimu wa kuona matokeo ya sera na mikakati inayotekelezwa.

Katika mchana wa siku hiyo, washiriki walipata fursa ya kusikiliza mada kutoka kwa wataalamu na kutoa maoni yao kuhusu marekebisho ya sheria za vyama vya siasa na gharama za uchaguzi. Wadau walizungumzia changamoto zinazowakabili wanawake katika siasa, pamoja na kutoa mapendekezo ya kuboresha sheria na taratibu za uchaguzi.

Hitimisho la mkutano lilisisitiza umuhimu wa kulinda utulivu na kudumisha maridhiano, na washiriki walitoa ombi maalum kwa vyama vya siasa kuhusu marekebisho ya sheria na ushiriki wa wanawake katika siasa.

#IMARISHA DEMOKRASIA TUNZA AMANI

Read More
SAVE

NINI NAFASI YA SERIKALI, ASASI ZA KIRAI, NA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HIZI R4 NA NINI KIFANYIKE?

Bw. Salim.

Niliposema ‘reform’ sikuwa na maana tuanze na reform. Hivyo ni lazima tuanze na maridhiano na kuvumiliana. Nakubaliana na wote wanaosema kuwa R4 ni falsafa sahihi sana. Hii mimi ninaamini kuwa hii itakuwa ni ‘legacy’ kwa mama Samia. Nini kifanyike, tuione Serikali ikifanya kwa vitendo, hili sio suala la kisiasa. Tunaona mabadiliko kwenye mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali. Ingawa kwenye siasa kuna mkwamo kwenye Sheria za Uchaguzi na Katiba mpya. Asasi za kiraia ziwaeleze wananchi na kuwafundisha.

Bw. S.Wasira.

Vyombo vya Habari vifanye kazi yake ya kuelimisha umma kwakuwa vinasilikizwa na Wananchi. Nafasi ya Serikali ni haya yanayoendelea, Serikali iko kwenye usahihi. Tutazame ‘reforms’ kwenye maeneo yote kwa mfano elimu,  vyama vya siasa vina nafasi ipi.

Bw. Ado – ACT WAZALENDO.

Mchakato wa Katiba nchi siyo jambo la kusubiri, mchakato wa Katiba mpya na ukamilike mapema baada ya uchaguzi mkuu. Mhe. Rais hakuwa na shinikizo lolote baada ya kichapo cha mwaka 2020, kwa hiari yake akaamua kufanya mabadiliko. R4 itapimwa kwa vitendo, kila mmoja wetu ana wajibu. Ingawa yako mambo ambayo yameshajenga mambo ya kitaifa. Sisi kama ICT Wazalendo tumechambua mambo ambayo yameshatekelezwa. Mengi yapo kwenye ripoti ya kikosi kazi, hivyo yaendelea kutekelezwa.

Bi. Mongela.

S5 za Japani zimewezesha maendeleo ya Japani. Hivyo na hili la R4 tunapaswa kufanyia mkamkati, tunapaswa kuitengenezea dira ili iwe ya Taifa. Tumuombe Mhe. Rais tulitoe mkononi mwa Mhe. Rais kisha tukimbiee nalo. Mimi natoa mapendekezo hizi R4 ziwe za umma na ziweze kwenda hata kwenya familia. Naomba kuwe na muendelezo ya kufikisha kwa kila mtu yaani Methodolojia, tukumbatie vile ambavyo tumeshavifanyia kazi.

Bw. Doyo.

Naomba kuungana na Mhe. Lipumba, ni vema wenzetu wa Serikali wakalichukua hili.  Kuhusu ajenda 2063, Mhe. Rais ameruhusu mwanamke aongoze mwanamke mmojammoja kwenye baraza ili washiriki kisheria. Nawaomba tutumie R4 kwenye  mjadala huu.

Read More
WATUU

UFAFANUZI WA 4R KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI KATIKA MREJESHO WA MKUTANO WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA


Bw. Doyo.

Naomba nianze na nia ya Mhe.Rais, nianze na Watendaji wa chini. Serikali itengeneze programu maalum yakuwafanya hawa Watumishi wa Serikali wazielewe vizuri R4. Dira ya Taifa ikieleweka tutapata Wawekezaji pia. Mhe. Rais anasisitiza kusikilizana na kutuvumilia. Hivyo kuna umuhimu watendaji wawe na uelewa.

Bw. Salim

Kwa kiwango gani R4 zinaweza kuisadia kuendana na Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda za 2063. Haya yote yanapaswa yaangaliwe na nguzo za kidunia, ili dunia itupime hivyo. Kama kuna joto kubwa la kisiasa hautaweza kufikia kwenye haya maendeleo.  Reforms zinazozungumzwa hapa ni pamoja na kuvumiliana kwa hoja ilituweze kuitengeneza nchi yetu, tunapaswa kuja na reforms za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivyo tuweze kupimana kwa uvumilivu na ukweli.

Bw. Ado Said

Falsafa hii ikitekelezwa kwa ukamilifu basi tutaenda sambasamba na Ajenda ya 2063 na Maendeleo Endelevu ya 2030.  Maridhiano ni sawa, ila nguzo mama ni Mabadiliko. Ni lazima sasa hii nguzo mama hii iendane na nguzo ya Katiba Mpya, Mchakato wa Katiba Mpya uanze hivi sasa na kuweka misingi madhubuti ya kisheria. Pamoja na kujadili miswada hii, lakini bado hatuna kalenda za utekelezaji wa Tume ya Haki Jinai na Kikosi Kazi, tunataka kuwa na kalenda, tunahitaji muafaka wa kitataifa. Mambo ambayo yameshapata muafaka wa kitaifa badi yatekelezwe. Kuhusu mifumo ya ruzuku bado ina shida, hivyo tufanye mabadiliko ya kimfumo. Tuwe na Kalenda ya utekelezaji.

NAFASI ZA R4 KULETA UTENDAJI MZURI WA HALI YA KISIASA

Bw. Ado

Mhe. Rais amezichukua hizi R4 kama nyenzo yake muhimu yakufanyia kazi. Maboresho ya kisiasa yaweze kukidhi haja ya Watanzania wote. Kwakiasi gani Wananchi wanaulewa kuhusu R4 za Mhe. Rais;

Sisi Wanasiasa tumeleewa vizuri sana kuhusu 4R na ndio maana tumekuwa tukishiriki kwenye meza ya mazungumzo. Hivyo hata uwepo wetu hapa unaonesha kuwa kumeelewa vizuri kuhusu hii R4. Mhe. Rais ametuonesha utashi wake na sisi tumeonesha kuwa tunamuamini. Hivyo tujenge misingi imara ya kikatiba na kisheria.

Bw. Salim.

Wananchi hawataki kuelewa kuhusu R4 ila wanataka kuona matokeo ya R4. Hivyo nguzo kuu ni Reforms, hivyo tunahitaji matokeo ya R4 na siyo mahubiri yake ya R4.  Matokeo kwenye uchumi, ajira ubora wa elimu, tija ya kiuchumi, umasikini wa kipato unapungua. Tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa kisiasa, tuwe na tume huru, kujenga ,msingi wa kitaifa kuhusu kuwa na Katiba Mpya. Hivyo Watanzania tunaweza kuanza kukata tamaa. Dhamira ipo, hivyo tumsaidie mwenye dhamira ili tupate matokeo. Hivyo wananchi wataelewa baada ya kuona matokeo. 

Bw. Doyo.

Kama unadai mkono na ukarudishiwa kodle basi utashukuru. Lapili, Watanzania hawa wanaelewa sana R4 za Mhe. Rais, kabla ya R4 kulikuwa na Mahabusu ambao walikuwa wanaonewa. Hivyo tuipongeze Serikali kwa kupeleka hii miswada kwa njia ya kawaida, kama ambavyo Mhe. Waziri amesema kuwa tutapokea maoni yote ya Wadau. Wote tumeona kuwa mada ni kujadili ajenda. Hivyo tunaomba tuweke maoni yetu sasa. Hata kuruani hakiundikwa kwa siku moja, tunapaswa tuige mifumo ya kiroho, haya mambo ni mchakato.

Bi. Mongela.

Naomba nitumie mfano wa kutaka mabadiliko ya katiba, aya ya 12 na 13 imesema Binadamu wote ni sawa, hivi hii katiba itaniondelea hayo. Mfano mwingine wakati ule wa Rais wa Kwaza wa Taifa hili, Rais alikuwa anazungumzia kuhusu utofauti wa kipato. Ni lazima tujue hiyo katiba itaandikwaje, mkakati wake ukoje na italiwekaje suala la usawa wa Mtanzania.

Jambo lingine ni hili la R4, juzi nimewaeleza kuwa naenda kwenye R4 watu walikuwa wananishangaa, hizi R4 ziwe za Mtanzania na zisiwe na Mama Samia. Tunapaswa tutumie Kiswahili, bado tuna kazi yakuwaelimisha Wananchi kuhusu R4. 

Bw. S.Wasira.

Uelewa wa Wananchi kuhusu R4.

Nimesisitiza kuhusu  Maridhiano (Recolianciation) ili turidhiane kwanza ndipo tufanye mabadiliko. Ni ngumu kuwa na ratiba yenye tarehe kwenye mambo makubwa ya nchi. Ni muhimu kuzungumza kuhusu Ustahimilivu (Resiliency), kuhusu Katiba hatuwezi kuwa na tarehe ya upatikanaji wa Katiba. Tutoe maoni yetu ilí ‘minimum reforms’ ifike mahali, tunapaswa kuwa na mchakato wa muda mrefu, mfupi na wa kati. ‘Reform’ haiwezi kutupatia majibu kesho.


ITAENDELEA…..

Read More
JA

UFAFANUZI WA 4R

KAMA ULIVYOONGOZWA NA 

BW. ABBAKARI MACHUMU

MWONGOZA MADA (SIKU YA 01)

Wachochea Mada walipata nafasi kusisitiza mambo 

yafuatayo

Dhana ya R4

Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resiliency), Mabadiliko (Reforms), Kujenga Upya (Rebuiling), uelewa wa jumla wa watoa mada ulikuwa washiriki asilimia 80%.  Ilisisitizwa kuwa tofauti zetu za kiitikadi zisivunje umoja wetu kama nchi.

Misingi ya kutengeneza dira

Uhuru wa vyomba vya habari na Uhuru wa Kujieleza, kujenga upya, kuvumiliana, kusameheana na maridhiano.

Kurudishwa kwa vikao vya kisiasa, utendaji wa Jeshi la Polisi umebadilika, na sasa tunaweka misingi thabiti. Kuna mambo yakuweka mifumo ya kisiasa, uchaguzi na demokrasia. Dira ya umoja inayounganisha taifa. Changamoto zetu za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kidemokrasia visijirudie. Kwa hivi sasa tunasahihisha yale yaliokuwa yametokea huko nyuma.

Nyenzo inayotuongoza ni uchambuzi wa kimuktadha (contextual analysis), jawabu la swali la R4 linapatikana kwenye hotuba ya kwanza ya Mhe. Rais mara baada ya kula kiapo. Hii imeonesha kuwa ukurasa mpya umefunguliwa na tunapaswa kufungua ukurasa mpya wa kisiasa. Hii imeonesha kuwa huko tulikotoka kulikuwa na giza ndio maana tumepaswa kufungua ukurasa upya. Sasa tunakuja na mambo ya mshikamao wa kitaifa kwa maana kuwa tunahitaji maridhiano.

Bw. S. Wasira.
“Misingi ya R4 yameendelea kubadilika sura kutokana na nyakati. Tatizo kubwa nikuelewa mahusiano yetu sisi kama Watanzania. Mhe. Rais sasa anataka tuzungumze na turidhiane. Mhe. Rais amechukua hatua stahiki, hata vyombo vya habari sasa vinaendelea kufanya kazi kwa uhuru. Kwa hivi sasa uchumi wetu ni endelevu. Hapa Tanzania bado tunaishi kijamaa japo hatuwezi kuuona. Hivyo chakwanza ni maridhiano ya kimfumo na unapaswa kuwa endelevu”

Bi. Mongela 

Maridhiano, hizi R4 mwisho wake tutaweza kubadili fikra zetu. Hivi sasa ukiangalia ni kama tumekuwa wanaharakati ni kama vile nchi yetu haijapata uhuru. Mabadiliko ya Tehama ni mabadiliko makubwa sana. Hivi sasa tunapaswa kujipanga kimawazo kwakuwa sasa kuna ‘artificial intelligence’. R4 zitusaidie kujenga nchi yetu.

Kuhusu Maendeleo Endelevu, msipofanya maridhiano mtakuwa hakuna muda wakutafakari, tunapaswa kwenda kweye maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mifumo yetu ya Elimu, Siasa, Utamaduni n.k inapaswa iendane na uchumu wetu.

ITAENDELA…

Read More
WATU

MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA   NCHINI, UKIJADILI   NA KUPOKEA MAONI YA MSWADA WA SHERIA ZA   UCHAGUZI NA SHERIA ZA VYAMA VYA SIASA. 

Baraza la Vyama vya Siasa nchini liliandaa Mkutano Maalum wa kujadili na kupokea maoni ya Wadau juu ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa ambayo ni matokeo ya mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Mgeni Rasmi katika mkutano huu alikuwa Bw. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wadau na Washiriki walijulishwa na kuhusu lengo la Mkutano, pamoja na mambo mengine, ilielezwa kuwa ni Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaojadili na kupokea maoni ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa 

Kauli mbiu ya mkutano huu Ilikuwa ni “Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia”. Mara baada ya maelezo haya. Mkutano huu uliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Katika ufunguzi wa mkutano huu taratibu zote na itifika ilizingatiwa ipasavyo na kikao kilifunguliwa rasmi na Mgeni Rasmi.

ITAENDELEA…….

Read More
SIM

MKUTANO HUU UMEKUWA WENYE TIJA KWANI MMETOA MAONI KWA KUZINGATIA MASLAHI MAKUBWA YA NCHI YETU – MHE. DOTO BITEKO

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaungana na watu wengine waliosema hapa nami nitoe shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa Juhudi zake ameweza kuimarisha ustawi wa Demokrasia hapa nchini sambamba na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuwaletea maendeleo Watanzania”

“Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amekuwa mfano wa kuigwa kitaifa na kimataifa kuhakikisha Demokrasia yetu inazidi kustawi na kuifanya Demokrasia yetu kuendeshwa kwa misingi ya haki, utawala bora na kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea na bila kusahau mazingira ya watu ambao bila wao Serikali haipati uhalali”

“Mkutano huu umekuwa wenye tija na mimi nimekuwa nikiufuatilia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mmezungumza mengi kutokana na Ajenda mlizomuwa nazo na ni wazi kabisa wadau waliokuwa wengi wametoa maoni yao mbalimbali kwa kuzingatia maslahi makubwa ya Nchi yetu”

“Upekee uliopo kwenye jambo hili. Baraza la vyama vya siasa mmeamua kutualika na sisi Serikali kama wadau na ndio maana mtaona mkutano huu si wa serikali ni Baraza la vyama vya siasa na yale yatakayosemwa hapa Serikali si ya imeamua bali yeye ni mdau kama wadau wengine”

“Mkutano huu si mali ya Serikali kwasababu katika yaliyojadiliwa haswa kwenye hii miswaada mitatu kwa taratibu zetu za utawala bora baada ya mswaada kusomwa bungeni basi mswaada ule ni mali ya bunge na si serikali tunabaki kama wadau wengine”

“Baada ya haya yote mliojadiliana, mchukue nafasi kuitikia wito wa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye amealika wadau mbalimbali kwenda Bungeni kutoa maoni yao kuanzia tarehe 6 – 10 Jijini Dodoma, msiache kwenda na haya mliyozungumza naamini mmejifua vizuri, mmepata focus kama vyama vya siasa, naoni yenu yanazingatiwa na Serikali kwa umuhimu wa kuzingatia utawala bora unaozingatia mihimili yetu ya dola”

Mhe. Doto Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Nchini.

Read More
WAT

FAIDA NA MANUFAA KWA JAMII JUU YA MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUHUSU MISWADA YA SHERIA ZA UCHAGUZI NA SHERIA ZA VYAMA VYA SIASA

Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa unaojadiliwa kuanzia tarehe 3 hadi 4 Desemba, 2023, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam unategemewa kuleta faida na manufaa kadhaa kwa jamii. 

ufafanuzi wa kina kuhusu faida na manufaa hayo

Uimarishaji wa Demokrasia

Mkutano huu unatoa fursa kwa vyama vyote vya siasa na wadau kuchangia katika mchakato wa kuandaa na kurekebisha sheria za uchaguzi na vyama vya siasa. Hii inaongeza ushiriki wa vyama vyote katika ujenzi wa demokrasia yenye nguvu na uwajibikaji.

Uhamasishaji wa Ushiriki wa Wananchi

Kupitia njia mbalimbali za utangazaji na mawasiliano, mkutano unawahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisheria. Hii inawapa wananchi sauti na fursa ya kuchangia kwenye maamuzi yanayowaathiri moja kwa moja.

Kuongeza Uelewa wa Sheria

 Wananchi watapata fursa ya kujifunza na kuelewa mabadiliko na mapendekezo ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa. Hii inaongeza uelewa wa kisheria miongoni mwa wananchi, ambao ni msingi wa demokrasia na ushiriki wa kiraia.

Kukuza Maridhiano na Uwajibikaji

Mkutano unaweza kusaidia kujenga mazingira ya maridhiano kati ya vyama vya siasa. Kwa kushirikiana katika mchakato huu, vyama vinaweza kujenga heshima na kuonyesha dhamira ya kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya taifa.

Elimu ya 4R

Kutoa elimu ya 4R kupitia mkutano inaleta uelewa zaidi kuhusu misingi muhimu ya demokrasia, maridhiano, uchaguzi, na haki nyingine za kisiasa. Hii inachangia kuwajengea wananchi uwezo wa kushiriki kikamilifu katika siasa.

Kushirikisha Wadau Wote

Mkutano unahakikisha ushirikishwaji wa vyama vyote vya siasa, serikali, na wananchi wengine muhimu. Hii inaongeza uwazi na uwajibikaji katika mchakato wa kutunga sheria.

Kusimamia Mkutano kwa Ufanisi

Usimamizi mzuri wa mkutano unahakikisha kuwa mchakato unafanyika kwa uwazi, haki, na uwajibikaji. Hii inajenga imani kati ya wananchi na mamlaka zinazohusika.

 Kutoa Nafasi kwa Maoni ya Wananchi

Wananchi wanapewa nafasi ya kuuliza maswali, kutoa maoni, na kushiriki kikamilifu katika mjadala. Hii inaleta uwazi na kuonyesha dhamira ya kusikiliza maoni ya raia.

Mkutano huu unalenga kuwa jukwaa la mjadala wa kisheria na kisiasa ambalo linaweza kutoa mabadiliko chanya na kujenga msingi thabiti wa demokrasia nchini Tanzania. Ili kufahamu matokeo na maamuzi ya kina, inashauriwa kufuatilia taarifa rasmi na ripoti zinazotolewa baada ya mkutano huo.

Read More