
Julai 2, 1992, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya kuruhusu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
tumepiga hatua, lakini, mpaka hii leo, bado upinzani kwa wengine unatafsiriwa kama ni uadui, na wakati mwingine ni uhaini.
Ni busara kutambua, kuwa wakati umebadilika. Mtanzania wa mwaka 1977 si Mtanzania wa mwaka 2023. Ni Zaidi ya miaka 40 atiii..
Hoja hii ya Katiba si kama inzi anayetua na kuruka. Hoja ya Katiba kwa sasa inaongozwa na kundi kubwa la vijana wanaotaka mabadiliko.
Hawa si inzi wanaotua na kuruka, ni siafu wanaokuja kwa kuongezeka idadi yao. Na hili Rais wa sasa ameliona hili na ndio maana ameridhia tuanze tu..
Na harakati za Watanzania kutaka marekebisho ya Katiba zina muda mrefu. Hizi si harakati mpya. Si harakati za chama au kikundi kidogo cha ’wapinzani’ wasioitakia mema nchi hii naamini hapana..
Siku zote, yamekuwa ni madai ya msingi ya Watanzania, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, rangi na makabila.
Kama ni shauri mahakamani, basi, lilishafunguliwa zamani. Kinachofanyika sasa ni mwendelezo tu wa shauri lenyewe
Si wengi, miongoni mwetu vijana wa sasa, wenye kumbukumbu ya ukweli huu ama kuyasoma na kuyatambua haya..
Ninachoomba katika forum hii ya KATIBA YA WATU, baada ya kupitia Nondo zinazoshuka hapa hebu kwa uchache tukumbusheni sisi wengine nini kilitokea miaka ya tisini, ilikuwaje hadi Julai 2, 1992 bunge likaridhia? Nani waliendesha harakati hizi za kudai mabadiliko? Na walipata kashikashi na upinzani wa namna gani?
[10:22, 17/05/2023] T: Nasoma Neno kwa neno script safi hii ngoja niifanyie kazi….Wadau wote wako hapa Duuuh! hoja imejengwa hii haya twende sawa 👍🏼MAJIBU…
[15:04, 17/05/2023] T: Tayari mwaka 1991 vuguvugu la kudai vyama vingi na Katiba mpya lilikwishakuanza.Wakati huo madai makubwa yalikuwa mawili;
Vyama vingi na Marekebisho ya Katiba.
Wapo hapa mnaokumbuka ’ KAMAKA’- Kamati ya Marekebisho ya Katiba iliyoundwa na wanaharakati.
Ikumbukwe, kuwa hayo yalikuwa ni madai ya Watanzania ndani ya mfumo wa chama kimoja.
Chifu Abdallah Fundikira aliongoza Kamati iliyoundwa, si na Serikali, bali wanaharakati, kuratibu mchakato wa kudai vyama vingi na Katiba mpya.
Hata wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kama Rais, aliweka ‘ mkwara’, kuwa madai hayo yasiendeshwe na watu au makundi ya watu bila kibali cha Serikali. Presha ya madai ilipoongezeka, wapo wazee wanakumbuka jinsi Mzee Ali Hassan Mwinyi aliweza kusoma alama za nyakati.
Mzee Mwinyi Alizungumza pale Chuo Kikuu Mlimani na kuweka bayana dhamira ya Serikali ya kuunda ‘ Tume ya Nyalali’ . Tume hiyo ilizunguka nchi nzima kuwauliza Watanzania kama wanataka kuendelea na Chama kimoja au Vyama vingi.
Chifu Fundikira alipata kutamka; kuwa huko ni kupoteza muda na fedha za wananchi. Itakumbukwa pia, Mabere Marando alikuwa Katibu wa Kamati ile ya wanaharakati ya kuratibu mchakato wa madai ya kuwapo na vyama vingi na marekebisho ya Katiba.

……………… Twendelee Sasa
[10:30, 17/05/2023] A: Kwa katiba yetu ya sasa wabunge wanawajibika kwa nani?Nimejaribu kusoma waliotangulia hapo kuangalia mgawanyo wa majukumu katika mihimili yetu hii mitatu.
Ni kweli chanya ni chache sana ukilinganisha na hasi. Mimi nitajikita kujaribu kujua kwa katiba yetu ya sasa hawa wabunge wanawajibika kwa nani? Je, mwezi kwa mwezi hawa watu wanatoa ripoti ya shughuli zao kwa nani? Je boss wa wabunge ni nani?
Maana kwa sasa hapa nchini ikiwa mbunge wewe tayari ni tajiri mkubwa na hakuna wa kukugusa. Na isitoshe kwa sasa ubunge imekuwa ndiyo mafanikio na siyo utumishi tena. Watu wananunua magari ya bei za juu na vitu vingine vya bei kubwa sana. Ubunge kwa sasa imekuwa ni kitega uchumi na siyo utumishi wa wananchi tena.
Na kwasababu wananchi hali zao ni duni wabunge wamekuwa Miungu watu kwenye majimbo yao. Mbunge anaweza kupita na kugawa chumvi ili kuwapoza wananchi. Na baada ya miaka mitano atapota tena kuomba kura. Hakuna wa kumpima hakuna ripoti yoyote ya alichokifanya.
Na kwa sababu ya vyama vingi wabunge sasa hawaondolewi kuhofia kushindwa kwenye uchaguzi.
Kwenye katiba hii napendekeza pawepo na check and balance kwenye bunge.
Pawepo na aina mbili ya Assembly
1. Lower Assembly
2. Upper Assembly
[10:33, 17/05/2023] A: Lower AssemblyHawa wawe ni hawa wabunge wanaochagulia kwenye majimbo na hawa ndio wanaowakilisha wananchi moja kwa moja. Hawa ni mdomo wa wananchi. Huku ndiko watakako toka mawaziri. Lakini mienendo yao itakuwa monitored na Upper Assembly
[10:37, 17/05/2023] A: Upper AssemblyHawa watapatikana kutokana na utaalam wa aina tofauti tofauti. Watakuwepo wawakilishi wa tasnia hizo na kutoka katika kundi hili tutapata makatibu wakuu wa wizara.
Makatibu watakuwa watendaji wakuu wa Wizara lakini mawaziri watakuwa viongozi wa wizara.
Hiyo itafanya mawaziri wawe wakuu kwenye wizara lakini Bunge la Lower Assembly litakuwa monitored na Upper Assembly
Tukitaka kuweka check and balance ya uhakika. Expenses haziepukiki.
Hata ni mawazo yangu
[10:40, 17/05/2023] +255 67: Samahani: Umelielewa swali langu? [10:42, 17/05/2023] T: fafanua swali ueleweke zaidi wadau watalijibu..lakini Msajili huteuliwa na Rais [10:50, 17/05/2023] A. Na ninavyoona upande wa Mahakama hakuna changamoto nyingi. Lakini huku kwenye Bunge na Serikali naweza kuliita hili bunge la katiba ya sasa ni Bunge la Serikali. Siyo bunge la wananchi.Mbunge anachaguliwa baada ya kuchaguliwa haonekani kwenye jimbo lake. Kila siku tunapishana na wabunge wote huku Dar.
Kilio changu kikubwa kabisa ni kuhusu hawa wabunge. Katiba ya Watu lazima ilete solution katika hili.
Ikiwezekana Mahakama iwe na meno ya kung’ata hawa wabunge.
[10:55, 17/05/2023] +255 : Sasa ulikuwa unazunguka nini? Nilitaka tu kujua anavyopatikana huyo msajili! Kumbe anateuliwa na Rais kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi? Yaani Mwenyekiti wa Chama cha Siasa ndiye anayemteua Msajili wa Vyama vya Siasa? Na Mgombea Urais ndiye anayemteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi? Sina maswali ya ziada kwa leo.
Vile vile usisahau kupitia malalamiko ya uchaguzi kwenye baadhi ya nchi kama Marekani zenye ‘katiba bora’. Mwisho unaweza kuangalia uapishwaji wa Mfalme hapo Uingereza na mapokeo yake
[12:01, 17/05/2023] K: Natofautiana na wewe kwa asilimia kubwa ; umekiri kuwa Wabunge uwajibikaji wao una maswali (**hili ni la kujadili lirekebishwe )Pia umependekeza mabadiliko ya mfumo wa Bunge (**sio vibaya tu kujadili hili pia )
Hoja yako ya pili imeambatana na kauli za vijembe juu ya ukwasi wa wabunge kuonyesha namna “unavyoumizwa “ na matumizi yao.
Ila pia umependekeza muundo ambao utaathiri “separation of powers” kwa kuleta mkanganyo wa Katibu mkuu kuwa bosi wa waziri kwenye upper assembly lakini wakiwa wizarani bosi ni Waziri anaye tokana na lower assembly nadhani unaona mkanganyiko huo.
Umehitimisha pia kwa kusisitiza kuwa gharama haziepukiki katika uongozi wa nchi ( ingawa nadhani Unamaanisha ilimradi wabunge waishi kimaskini )
Tukitaka Tanzania iliyoendelea Kiuchumi haya mawazo lazima yachakatwe kwa umakini
Tufikiri miaka 200 baadaye ambapo kizazi chetu cha tano ndio kitafaidi
[12:28, 17/05/2023] +255 76: Kwa hoja hii kumbe shida ni watu wanaochaguliwa na sio Bunge [12:53, 17/05/2023] A: Katika nchi nyingi zilizofanikiwa duniani zinatumia mfumo wa Bicameral legislature than Unicameral legislatureNitaeleza zaidi kuhusu mambo haya mawili. Lakini kwa sasa ngoja nilitolee ufafanuzi suala ambalo umeliiya ni vijembe
Ni kweli kabisa mbunge ni mtumishi wa umma hatakiwi kuonesha kiburi na kuvimba. Na pia sijasema wabunge wawe masikini bali nimesema kuwa ubunge kwa sasa imekuwa kama kitenge uchumi na sio utumishi.
Sasa nakuja kuongelea wazo langu la kuhusu Bicameral legislature
Kwa sasa hapa Tanzania tupo na bunge la aina moja tu kwamba hakuna anayewamulika hawa wabunge wanajiongoza wao wenyewe tu. Lakini tukiwa na mfumo wa Bicameral legislature tunakuwa na mmoja anamsimamia mwingine kwa namna nyingine.
[12:58, 17/05/2023] D: Hivi kuna mtu anaijua Katiba na Mfumo wa Bunge la China? [13:07, 17/05/2023] A: Kwa kiasi kidogo nimejaribu kufuatilia maandiko kadha wa kadha kuhusu bunge la china.Bunge la china linaitwa National People’s Congress
Hawa huchaguliwa kisha huingia kwenye congress na hawalipwi maana ni kazi ya utumishi. Mwaka 2018 lilikuwa na watu 2,980.
Huwa wanakutana mara in full mara moja kwa mwaka kwa muda wa wiki mbili. Lakini wamekasimu madaraka yao kwenye Standing Committee of the National People’s Congress
Hawa wapo kama watu 170 hivi.
Mfumo wa china ni unicameral legislature hii ni kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kuwa na Chama kimoja

Sisi bado tuna hungovers za mfumo wa chama kushika hatamu, ambapo Rais (the executive branch) hutakiwa kuwa overpowering ya mifumo mingine, albeilt implicitly. And it is by design and deliberate ili kumpa Mwkt wa chama dola kubaki supreme, indeed.
Huko tunakotoka mpaka hapa tulipo, hii separation of power ilifanywa kinadharia zaidi kuridhisha uwepo wa serikali inayoeleweka katika anga za kimataifa, but in reality, tuna mfumo wa kijanja sana ambao unampa Rais na Serikali, too much power to always arm-twist the other two branches of govt to comply with whatever the executive branch desires.
Yes, kwa Tanzania, checks and balances is a mere gimmick to fool the unlearned minds but it’s rarely practised in a real sense of the word. Bunge halina chombo cha kuli regulate linapokuwa dhaifu na kupitisha mambo ya hovyo.
Bunge letu ni extention of the executive branch zaidi kuliko kuwa a regislative assemby inayowakilisha wananchi kutunga sheria za kujiongeza wenyewe kama wenye nchi.
Bunge letu linaheshimu, kutii, a kuopa zaidi Rais na Serikali yake kuliko wananchi waliowachagua.
And you know why? Because our MPs aree too politically minded. Always thinking and calculating about the next election!
Wanamwogopa n kumsifia Rais muda wote kwa sababu Rais ndiyo pia Mwkt wa chama kinachowapa nafasi wabunge wote nafasi kugombea na kupata hizo nafasi. Usipo mwogopa na kumsifia Rais bungeni na popote unapoenda kama mbunge unajiweka kwenye hatari ya kuwa booted out kwenye teuzi za baadae.
All this goes back to mfumo uliowekwa kijanja tangu mwanzo; wa kubakiza Rais na Serikali yenye nguvu mno juu ya branches nyingine za kiutawala.
With this approach, you can forget good governance, and you can definately forget maendeleo ya nchi na watu wake for the next 200 years!
Na kuhusu tofauti ya mishahara ya wabunge na Mawaziri kutosogeleana na ya watumishi wengine wa chini, tatizo ni lile lile. Nani atam regulate nani??
Fikiria Bunge hujipangia mishahara yake na kumtega Rais apitishe. Akiwagomea na wao wanamsubiri akiwapelekea mapendekezo yake wamshughulikie!
Hakuna chombo cha tatu cha kucheck na kubalance off hii power struggle kwenye mambo yenye adverse consequences kwa nchi.
I mean, it’s just a mess.
Live Long Tanzania. God bless the URT🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Mimi sitaki niongelee sana kuhusu vyama vya siasa. Maana vyama vya siasa vilianza kwenye karne ya 17 huko uingereza na vikasambaa sehemu mbalimbali karne ya 18 baada vikaimarika kwenye karne ya 19. Lakini dunia ilikuwepo kabla ya hapo na watu walikuwa wakiongozwa na Ideology za kidini.
Lazima turudi kwenye drawing board tujiulize je, ni nini lengo letu hasa kama nchi kuwa na vyama vingi?
[14:17, 17/05/2023] A: Tangu 1992 Tumepiga hatua zipi? Je, ni muhimu tuendelee na mfumo huu wa vyama vingi? Je, hatuwezi tukaenda na mfumo wa China kisha tukauboresha? Kwamba tunakuwa na chama kimoja lakini ndani ya chama hicho kukawa na namna ya watu kushiriki na kutoa maoni yao? [14:17, 17/05/2023] P: Si umesema vyama tuviache? Sasa tena mbona unauliza kuhusu vyama?🤣🤣🤣🤣🤷🏾♂️🤷🏾♂️Mfumo wa chama komoja au vyama vingi tunaweka kwenye National vision yaani kiwepo chama kisiwepo chama lazima vision itekelezwe.
Kwahiyo kwangu tukiwa na Chama kimoja hakuna shida as long as National Vision ipo vizuri na Check and Balance imekaa vizuri.
National Vision inatengeneza national Ideology. Yaani Taifa tunakuwa na imani yetu na kila mmoja anajua wapi tunaenda.
So kuhusu vyama hata kama tukiamua tuwe na chama kimoja na ndani ya chama hicho wanasiasa wanapambana na kuonesha namna gani ya kuweza kufikia National Vision.
[14:29, 17/05/2023] A: Mimi huwa nawaangalia wachina kwenye kizazi chetu hiki wameweza kuonesha kuwa maendeleo hayatokani na vyama vingi bali ni National Foundations and National Pillars then vyama vingi vya siasa ni kama mapambo ndani ya nyumba yanaoonwa na na watu wa nje kupitia dirisha dogo la FDI, Loans and donations [14:38, 17/05/2023] K: Maono …..maono maono!Katika Kitabu cha Kale nimemsoma Mfalme Suleiman Alisema “pasipo MaONO watu(a people) huangamia…
Wakati tunaelekea kutengeneza namna ya kuiweka Katiba yetu vizuri ….tuainishe MAONO ya TAIFA letu…kwa kipaumbele!
[14:39, 17/05/2023] P: Chinese? Tuna aspire kuiga China kwa mara nyingine baada ya kuwaiga mara baada ya uhuru na matokeo ndio haya?OK, kama huko ndio unataka twende, basi I reserve my comments in this discussion mpaka tutakapopata tunachotaka kuwa.🙏🏽
[14:45, 17/05/2023] T: Kuhusu mfumo wa Katiba wa China, ina Katiba ambayo ilitungwa mwaka 1982 na kufanyiwa marekebisho kadhaa tangu wakati huo. Ina mihimili mitatu ya Serikali: Rais, Waziri Mkuu, na Bunge la Watu. Rais wa China ni Mkuu wa Nchi na Mkuu wa Majeshi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Watu, anachaguliwa na Baraza la Kitaifa la Watu wa Congress ya Watu. Waziri Mkuu wa China ni Mkuu wa Serikali na mtendaji mkuu wa Baraza la Serikali la Watu. Bunge la Watu wa China, ambalo linajulikana kama Congress ya Watu, linajumuisha wajumbe kutoka kwa majimbo yote ya China, ambao huchaguliwa na raia wa China…Sijajua lengo la swali hili lakini sawa tunapaswa kujifunza kwa wengine naomba mtupitishe maeneo ambayo ni mapungufu yetu na tunatokaje huko tuendako…
Vyama vya siasa ni kuruhusu mawazo tofauti tofauti kupitia siasa. Nimejaribu kuelezea kuwa vyama vya siasa vilizna karne ya 17 huko uingereza lakini kabla ya hapo dini ndizo zilikuwa zikishughulika na maoni na wafuasi. Na mpaka leo ukiangalia dini bado zinanguvu sana.
Nikasema kwanini sasa tusiende kwenye drwing board ili tujue tangu 1992 pale vyama vingi vya siasa kurudishwa miaka 31 imepita tunaweza kujitafakari je, kuwa na vyama vingi ni nini tumefaidika?
Nikasema wachina wamewezaje maana wapo na chama kimoja na uchumi wao kwa sasa ni mkubwa mno. Ukiongelea Technology, Infrastructure nk, wachina wamepiga hatua sana.
Nikapendekeza kuwa lazima kwenye katiba yetu ya sasa ielekeze National Vision than kuelezea kuwa nchi yetu ni ya vyama vingi.
Na hiyo National Vision itazaa National Ideology so viwepo vyama vingi au visiwepo As long as direction inaeleweka.
Kwenye katiba ya sasa imesema nchi yetu ni ya Kijamaa so huo ujamaa uliosemwa kwenye katiba watu wanaujua?
Natumaini nimeeleza vizuri…..
……………….
[15:10, 17/05/2023] P: Nadhani tunatumia uwepo wa vyama vingi as distraction to the real problem!Tukitaka ku assess impact ya ama kuwepo na vyama vingi au kibaki kimoja, tusianzie mwaka 1992. Tuanzie 1961 mpaka 1992 kabla ya vyama vingi, tulifanya nin? Tulikuwa chini ya chama kimoja. Serikali toka chama kimoja. Na tulikuwa chini ya ujamaa proper. Je, kuna cha tofauti tulicho achieve wakati ule ambacho tunatamani to turn the clock back?
Kwa maoni yangu, vyama vingi Tanzania hata si vya ujadili kwa sababu kwa Katiba hii na muundo wa utawala uliopo, hawana impact popote zaidi ya kwenye uchaguzi. Kuna vyama hawajawahi kuunda serikali, na hawajawahi kupiitisha sheria au sera yoyote yenye ku affaect Taifa. Vitu vyote tangu uhuru, vimefanywa na chama kimoja au viongozi wanaotoka chama kile kile. So kama tunataka kutafuta tatizo tuliangalie kwa watu au mfumo uliodumu muda wote huu, ambao matokeo yake tunayajua.
Lakini huwezi kuniambia unataka checks and balances lakini kwa kutaka kuiga Commuinist China. Hapo tutalazimika ku drop vitu vingi sana kwenye hii Katiba na sheria zetu.
Lazima tufungulie kiwango fulani cha ukatili, secrecy, brutality, na complete disregard of human rights.
Kama tunataka kurudi huko mimi simooo…🙆🏾♂️
Kisha ndio

MJADALA UNAENDELEA……




