Nimepitia majibu ya wadau juu ya Msajili na vyama vya siasa, lakini huku mtaani uhusiano wa siasa za Tanzania na Katiba mpya haueleweki, mara wanaharakati wanasema tusiwaachie wanasiasa, mara serikali itauvuruga, mara mchakato ni wa wananchi, bado najiuliza pengine si mimi tu…Siasa za Tanzania na Katiba mpya vina uhusiano gani na mlezi wake ni MSAJILI?
MAJIBU
Siasa za Tanzania na Katiba mpya zina uhusiano mkubwa kwani siasa za Tanzania zinaathiri mchakato wa kupata katiba mpya na maudhui ya katiba yana athari kubwa katika mfumo wa siasa za Tanzania.
Katiba mpya inatarajiwa kusimamia mfumo wa siasa za Tanzania, kwa kuainisha muundo wa serikali, utaratibu wa utawala, utengenezaji wa sheria, utawala bora, na mambo mengine yanayohusiana na utawala wa nchi.
Katiba mpya itasimamia haki na wajibu wa serikali na wananchi na itaimarisha demokrasia na utawala bora.
Siasa za Tanzania zina athari kubwa katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Viongozi wa siasa na vyama vya siasa wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maudhui ya katiba mpya na wanaweza kushawishi mchakato wa kupata katiba mpya. Pia, siasa za Tanzania zinaweza kuathiri upatikanaji wa rasilimali na ushiriki wa wananchi katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Kwa hiyo, ili mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuwa na mafanikio, ni muhimu kwa siasa za Tanzania kuzingatia maudhui ya katiba na kusaidia kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa njia ya uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali wa kisiasa na kijamii.
TUNAULIZANA HAPA; Nini utofauti wa siasa za Tanzania na katiba ya Tanzania sasa?
Kuna tofauti kati ya Siasa na Katiba ya Tanzania lakn pia kuna uhusiano mkubwa wa siasa na katiba kwa nchi yeyote ile kama ifuatavyo;
1.Siasa ni mfumo wa kutawala au kusimamia mambo ya nchi ambao unahusisha shughuli za kisiasa kama vile uchaguzi,uteuzi wa viongozi wa serikali na maamuzi mengine ya kisiasa.Siasa inahusisha vyama vya siasa ambavyo vinashiriki ktk uchaguzi na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
2.Katiba ya Tanzania ni sheria kuu ambayo inaweka mfumo wa utawala,haki na wajibu wa raia na serikali na taratibu za kufanya maamuzi ya kisiasa.Katiba inaelezea Mamlaka na majukum ya vyombo vya dola kama vile,Mahakama,Bunge na Serikali.
3.Katiba pia inalinda haki na uhuru wa raia,na inatoa mfumo wa kudhibiti madaraka ya serikali.
Kwahiyo tofauti kuu kati ya Siasa na Katiba ni kwamba; Siasa inahusisha shughuli za kisiasa na Utawala wa nchi,wakati Katiba ni Sheria kuu inayoongoza shughuli hizo za kisiasa na utawala wa nchi.
Ahsante.
Mwl.Suleiman Ahmad
Usagara Sec




