“Kikombe tulichonyweshwa kuanzia mwaka 2015 hakuna Mtanzania ambaye atakisahau. Mimi ninavyoona hapa tuanze na maridhiano (reconciliation). Hizi R4 zifafanuliwe vizuri na Watanzania waelewe. Maridhiano yasiwe kati ya chama na chama, maridhiano yawe ni yawatanzania na siyo kati ya chama na chama. Naomba kuwe na semina maalum ya hizi R4 ili zieleweke” Bw. Joseph Thelasini.


