Category: Maendeleo

WATUU

UFAFANUZI WA 4R KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI KATIKA MREJESHO WA MKUTANO WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA


Bw. Doyo.

Naomba nianze na nia ya Mhe.Rais, nianze na Watendaji wa chini. Serikali itengeneze programu maalum yakuwafanya hawa Watumishi wa Serikali wazielewe vizuri R4. Dira ya Taifa ikieleweka tutapata Wawekezaji pia. Mhe. Rais anasisitiza kusikilizana na kutuvumilia. Hivyo kuna umuhimu watendaji wawe na uelewa.

Bw. Salim

Kwa kiwango gani R4 zinaweza kuisadia kuendana na Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda za 2063. Haya yote yanapaswa yaangaliwe na nguzo za kidunia, ili dunia itupime hivyo. Kama kuna joto kubwa la kisiasa hautaweza kufikia kwenye haya maendeleo.  Reforms zinazozungumzwa hapa ni pamoja na kuvumiliana kwa hoja ilituweze kuitengeneza nchi yetu, tunapaswa kuja na reforms za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hivyo tuweze kupimana kwa uvumilivu na ukweli.

Bw. Ado Said

Falsafa hii ikitekelezwa kwa ukamilifu basi tutaenda sambasamba na Ajenda ya 2063 na Maendeleo Endelevu ya 2030.  Maridhiano ni sawa, ila nguzo mama ni Mabadiliko. Ni lazima sasa hii nguzo mama hii iendane na nguzo ya Katiba Mpya, Mchakato wa Katiba Mpya uanze hivi sasa na kuweka misingi madhubuti ya kisheria. Pamoja na kujadili miswada hii, lakini bado hatuna kalenda za utekelezaji wa Tume ya Haki Jinai na Kikosi Kazi, tunataka kuwa na kalenda, tunahitaji muafaka wa kitataifa. Mambo ambayo yameshapata muafaka wa kitaifa badi yatekelezwe. Kuhusu mifumo ya ruzuku bado ina shida, hivyo tufanye mabadiliko ya kimfumo. Tuwe na Kalenda ya utekelezaji.

NAFASI ZA R4 KULETA UTENDAJI MZURI WA HALI YA KISIASA

Bw. Ado

Mhe. Rais amezichukua hizi R4 kama nyenzo yake muhimu yakufanyia kazi. Maboresho ya kisiasa yaweze kukidhi haja ya Watanzania wote. Kwakiasi gani Wananchi wanaulewa kuhusu R4 za Mhe. Rais;

Sisi Wanasiasa tumeleewa vizuri sana kuhusu 4R na ndio maana tumekuwa tukishiriki kwenye meza ya mazungumzo. Hivyo hata uwepo wetu hapa unaonesha kuwa kumeelewa vizuri kuhusu hii R4. Mhe. Rais ametuonesha utashi wake na sisi tumeonesha kuwa tunamuamini. Hivyo tujenge misingi imara ya kikatiba na kisheria.

Bw. Salim.

Wananchi hawataki kuelewa kuhusu R4 ila wanataka kuona matokeo ya R4. Hivyo nguzo kuu ni Reforms, hivyo tunahitaji matokeo ya R4 na siyo mahubiri yake ya R4.  Matokeo kwenye uchumi, ajira ubora wa elimu, tija ya kiuchumi, umasikini wa kipato unapungua. Tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa kisiasa, tuwe na tume huru, kujenga ,msingi wa kitaifa kuhusu kuwa na Katiba Mpya. Hivyo Watanzania tunaweza kuanza kukata tamaa. Dhamira ipo, hivyo tumsaidie mwenye dhamira ili tupate matokeo. Hivyo wananchi wataelewa baada ya kuona matokeo. 

Bw. Doyo.

Kama unadai mkono na ukarudishiwa kodle basi utashukuru. Lapili, Watanzania hawa wanaelewa sana R4 za Mhe. Rais, kabla ya R4 kulikuwa na Mahabusu ambao walikuwa wanaonewa. Hivyo tuipongeze Serikali kwa kupeleka hii miswada kwa njia ya kawaida, kama ambavyo Mhe. Waziri amesema kuwa tutapokea maoni yote ya Wadau. Wote tumeona kuwa mada ni kujadili ajenda. Hivyo tunaomba tuweke maoni yetu sasa. Hata kuruani hakiundikwa kwa siku moja, tunapaswa tuige mifumo ya kiroho, haya mambo ni mchakato.

Bi. Mongela.

Naomba nitumie mfano wa kutaka mabadiliko ya katiba, aya ya 12 na 13 imesema Binadamu wote ni sawa, hivi hii katiba itaniondelea hayo. Mfano mwingine wakati ule wa Rais wa Kwaza wa Taifa hili, Rais alikuwa anazungumzia kuhusu utofauti wa kipato. Ni lazima tujue hiyo katiba itaandikwaje, mkakati wake ukoje na italiwekaje suala la usawa wa Mtanzania.

Jambo lingine ni hili la R4, juzi nimewaeleza kuwa naenda kwenye R4 watu walikuwa wananishangaa, hizi R4 ziwe za Mtanzania na zisiwe na Mama Samia. Tunapaswa tutumie Kiswahili, bado tuna kazi yakuwaelimisha Wananchi kuhusu R4. 

Bw. S.Wasira.

Uelewa wa Wananchi kuhusu R4.

Nimesisitiza kuhusu  Maridhiano (Recolianciation) ili turidhiane kwanza ndipo tufanye mabadiliko. Ni ngumu kuwa na ratiba yenye tarehe kwenye mambo makubwa ya nchi. Ni muhimu kuzungumza kuhusu Ustahimilivu (Resiliency), kuhusu Katiba hatuwezi kuwa na tarehe ya upatikanaji wa Katiba. Tutoe maoni yetu ilí ‘minimum reforms’ ifike mahali, tunapaswa kuwa na mchakato wa muda mrefu, mfupi na wa kati. ‘Reform’ haiwezi kutupatia majibu kesho.


ITAENDELEA…..

Read More
JA

UFAFANUZI WA 4R

KAMA ULIVYOONGOZWA NA 

BW. ABBAKARI MACHUMU

MWONGOZA MADA (SIKU YA 01)

Wachochea Mada walipata nafasi kusisitiza mambo 

yafuatayo

Dhana ya R4

Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resiliency), Mabadiliko (Reforms), Kujenga Upya (Rebuiling), uelewa wa jumla wa watoa mada ulikuwa washiriki asilimia 80%.  Ilisisitizwa kuwa tofauti zetu za kiitikadi zisivunje umoja wetu kama nchi.

Misingi ya kutengeneza dira

Uhuru wa vyomba vya habari na Uhuru wa Kujieleza, kujenga upya, kuvumiliana, kusameheana na maridhiano.

Kurudishwa kwa vikao vya kisiasa, utendaji wa Jeshi la Polisi umebadilika, na sasa tunaweka misingi thabiti. Kuna mambo yakuweka mifumo ya kisiasa, uchaguzi na demokrasia. Dira ya umoja inayounganisha taifa. Changamoto zetu za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kidemokrasia visijirudie. Kwa hivi sasa tunasahihisha yale yaliokuwa yametokea huko nyuma.

Nyenzo inayotuongoza ni uchambuzi wa kimuktadha (contextual analysis), jawabu la swali la R4 linapatikana kwenye hotuba ya kwanza ya Mhe. Rais mara baada ya kula kiapo. Hii imeonesha kuwa ukurasa mpya umefunguliwa na tunapaswa kufungua ukurasa mpya wa kisiasa. Hii imeonesha kuwa huko tulikotoka kulikuwa na giza ndio maana tumepaswa kufungua ukurasa upya. Sasa tunakuja na mambo ya mshikamao wa kitaifa kwa maana kuwa tunahitaji maridhiano.

Bw. S. Wasira.
“Misingi ya R4 yameendelea kubadilika sura kutokana na nyakati. Tatizo kubwa nikuelewa mahusiano yetu sisi kama Watanzania. Mhe. Rais sasa anataka tuzungumze na turidhiane. Mhe. Rais amechukua hatua stahiki, hata vyombo vya habari sasa vinaendelea kufanya kazi kwa uhuru. Kwa hivi sasa uchumi wetu ni endelevu. Hapa Tanzania bado tunaishi kijamaa japo hatuwezi kuuona. Hivyo chakwanza ni maridhiano ya kimfumo na unapaswa kuwa endelevu”

Bi. Mongela 

Maridhiano, hizi R4 mwisho wake tutaweza kubadili fikra zetu. Hivi sasa ukiangalia ni kama tumekuwa wanaharakati ni kama vile nchi yetu haijapata uhuru. Mabadiliko ya Tehama ni mabadiliko makubwa sana. Hivi sasa tunapaswa kujipanga kimawazo kwakuwa sasa kuna ‘artificial intelligence’. R4 zitusaidie kujenga nchi yetu.

Kuhusu Maendeleo Endelevu, msipofanya maridhiano mtakuwa hakuna muda wakutafakari, tunapaswa kwenda kweye maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mifumo yetu ya Elimu, Siasa, Utamaduni n.k inapaswa iendane na uchumu wetu.

ITAENDELA…

Read More
WATU

MKUTANO MAALUM WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA   NCHINI, UKIJADILI   NA KUPOKEA MAONI YA MSWADA WA SHERIA ZA   UCHAGUZI NA SHERIA ZA VYAMA VYA SIASA. 

Baraza la Vyama vya Siasa nchini liliandaa Mkutano Maalum wa kujadili na kupokea maoni ya Wadau juu ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa ambayo ni matokeo ya mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Mgeni Rasmi katika mkutano huu alikuwa Bw. Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wadau na Washiriki walijulishwa na kuhusu lengo la Mkutano, pamoja na mambo mengine, ilielezwa kuwa ni Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaojadili na kupokea maoni ya mswada wa Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa 

Kauli mbiu ya mkutano huu Ilikuwa ni “Toa Maoni Yako Kuimarisha Demokrasia”. Mara baada ya maelezo haya. Mkutano huu uliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Katika ufunguzi wa mkutano huu taratibu zote na itifika ilizingatiwa ipasavyo na kikao kilifunguliwa rasmi na Mgeni Rasmi.

ITAENDELEA…….

Read More
SIM

MKUTANO HUU UMEKUWA WENYE TIJA KWANI MMETOA MAONI KWA KUZINGATIA MASLAHI MAKUBWA YA NCHI YETU – MHE. DOTO BITEKO

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaungana na watu wengine waliosema hapa nami nitoe shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa Juhudi zake ameweza kuimarisha ustawi wa Demokrasia hapa nchini sambamba na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuwaletea maendeleo Watanzania”

“Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amekuwa mfano wa kuigwa kitaifa na kimataifa kuhakikisha Demokrasia yetu inazidi kustawi na kuifanya Demokrasia yetu kuendeshwa kwa misingi ya haki, utawala bora na kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea na bila kusahau mazingira ya watu ambao bila wao Serikali haipati uhalali”

“Mkutano huu umekuwa wenye tija na mimi nimekuwa nikiufuatilia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mmezungumza mengi kutokana na Ajenda mlizomuwa nazo na ni wazi kabisa wadau waliokuwa wengi wametoa maoni yao mbalimbali kwa kuzingatia maslahi makubwa ya Nchi yetu”

“Upekee uliopo kwenye jambo hili. Baraza la vyama vya siasa mmeamua kutualika na sisi Serikali kama wadau na ndio maana mtaona mkutano huu si wa serikali ni Baraza la vyama vya siasa na yale yatakayosemwa hapa Serikali si ya imeamua bali yeye ni mdau kama wadau wengine”

“Mkutano huu si mali ya Serikali kwasababu katika yaliyojadiliwa haswa kwenye hii miswaada mitatu kwa taratibu zetu za utawala bora baada ya mswaada kusomwa bungeni basi mswaada ule ni mali ya bunge na si serikali tunabaki kama wadau wengine”

“Baada ya haya yote mliojadiliana, mchukue nafasi kuitikia wito wa Spika wa Bunge la Tanzania ambaye amealika wadau mbalimbali kwenda Bungeni kutoa maoni yao kuanzia tarehe 6 – 10 Jijini Dodoma, msiache kwenda na haya mliyozungumza naamini mmejifua vizuri, mmepata focus kama vyama vya siasa, naoni yenu yanazingatiwa na Serikali kwa umuhimu wa kuzingatia utawala bora unaozingatia mihimili yetu ya dola”

Mhe. Doto Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Nchini.

Read More
KIJU

NI KWA NAMNA GANI WANANCHI WANANWEZA KUPATA MSAADA WA KISHERIA

Nchi nyingi huwa na ofisi za huduma za kisheria zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipia huduma za mawakili binafsi. Huduma hizi zinaweza kujumuisha ushauri wa kisheria, usuluhishi wa migogoro, na hata uwakilishi kisheria kwa mahakamani.

Kuna mashirika mengi ya kutoa msaada wa kisheria ambayo yanaweza kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa wananchi. Mashirika haya yanaweza kuwa ya kiraia au yanaweza kuungwa mkono na serikali.

 

Mabaraza ya Mawakili

Mabaraza ya mawakili katika nchi nyingi yanaweza kutoa mwongozo na rufaa kwa mawakili wenye ujuzi na waaminifu. Wananchi wanaweza kuwasiliana na baraza la mawakili ili kupata mwongozo wa jinsi ya kupata msaada wa kisheria.

Vyama vya Watumiaji.

Vyama vya watumiaji na mashirika yanayolinda haki za watumiaji mara nyingine hutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanaokumbana na masuala ya kibiashara au wanaotaka kushughulikia migogoro na wauzaji.

Wakili Binafsi   
Kwa wale walio na uwezo wa kifedha, kuajiri wakili binafsi ni njia nyingine ya kupata msaada wa kisheria. Wakili binafsi ataweza kutoa ushauri wa kisheria wa kibinafsi na kutoa uwakilishi katika kesi au mchakato wowote wa kisheria.

Tovuti na Rasilimali za Mtandaoni
Kuna tovuti nyingi na rasilimali za mtandaoni zinazotoa habari za kisheria na hata zinaweza kuunganisha wananchi na mawakili au mashirika ya kutoa msaada wa kisheria.

Mashauriano ya Kisheria ya Bure
Baadhi ya mawakili na ofisi za kisheria hutoa mashauriano ya kisheria ya bure kwa wananchi. Hii ni fursa ya kuzungumza na wakili na kupata ufahamu wa awali juu ya suala linalowakabili.

Huduma za Kijamii

Huduma za kijamii mara nyingine hutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanaopata changamoto za kijamii, kama vile unyanyasaji wa kijinsia, haki za watoto, au masuala ya nyumba.

 Kwa kuzingatia aina ya suala la kisheria na hali ya mtu binafsi, njia bora ya kupata msaada wa kisheria inaweza kutofautiana. Ni muhimu kutafuta msaada wa kitaalamu mapema na kuchunguza chaguzi zote zinazopatikana ili kufikia suluhisho la kisheria linalofaa

Read More
SAM

Jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuleta maelewano, usalama, na maendeleo endelevu nchini Tanzania baada ya historia ya vyama vingi na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika vyama vya upinzani na serikali

Historia ya siasa nchini Tanzania imekuwa na changamoto, hasa baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Mapungufu na uhasama katika vyama vimekuwa vichocheo vya mivutano na migogoro katika jamii.

Rais Samia ameazimia kujenga nchi yenye maelewano, usalama, na maendeleo. Mpango mkakati wa R4 unalenga kuhamasisha msamaha, uvumilivu, mabadiliko, na ujenzi wa nchi kwa pamoja. R4 ni mfumo wa kivitendo unaolenga kuleta mageuzi ya kweli na kufufua umoja na mshikamano.

Rais Samia amekutana na vikwazo na upinzani kutoka kwa baadhi ya watu wasio na nia njema na nchi. Hata hivyo, ameendelea kutekeleza mpango wake licha ya changamoto hizo, akionyesha utayari wake wa kusimamia mabadiliko hata kwenye mazingira magumu

Ripoti ya tume ya Jaji Nyalali inaonesha kwamba awali, Watanzania wengi hawakuwa tayari kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Serikali iliona mbali na kuchukua hatua ya kulazimisha kuanzisha mfumo huu ili kuzuia athari za kutokea na kuanguka kwa mfumo wa ujamaa.

Mfumo wa vyama vingi umekuwa na changamoto, na katika vipindi vya uchaguzi, umesababisha mahusiano mabaya katika jamii. Hii imepelekea majanga na hasara za maisha na mali.

Rais Samia ameanza kwa kutilia mkazo upatanishi kama njia ya kujenga maelewano na kuimarisha umoja wa kitaifa. Hii inaonyesha utambuzi wa changamoto za kihistoria na azma ya kuleta mabadiliko yenye tija.

Katika muktadha huu, Rais Samia anachukua hatua madhubuti kuelekea kujenga jamii inayojali, yenye maelewano, na inayoelekeza nguvu zake kwenye maendeleo endelevu. Ni mchakato unaohitaji muda na ushirikiano wa wananchi wote kuleta mabadiliko anayoyaongoza.

Read More
SWADA

MALENGO MAKUU YA DEMOKRASIA 

Ni kuhakikisha kwamba wananchi wanawakilishwa katika mchakato wa maamuzi na serikali. Hii inamaanisha kutoa fursa kwa watu kuchagua viongozi wao kupitia uchaguzi na kushiriki katika maamuzi yanayowahusu. Demokrasia ya Tanzania inamalengo makuu yafuatayo;

1.Uhuru na Haki za Binadamu: Demokrasia inalenga kuhakikisha uhuru wa kimsingi na haki za binadamu kwa wananchi wake. Hii ni pamoja na uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuabudu, haki ya kufanya mikutano na maandamano, na haki nyingine za msingi za binadamu.

2.Utawala wa Sheria: Demokrasia ina lengo la kuanzisha utawala wa sheria, ambapo hakuna mtu au kundi la watu wanaotawala juu ya sheria. Hii inahakikisha kuwa kila mtu, pamoja na viongozi wa serikali, wako chini ya mamlaka ya sheria.

3.Uwajibikaji: Malengo ya demokrasia ni kuhakikisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi wao. Viongozi wanapaswa kufanya maamuzi yao kwa kuzingatia maslahi ya umma na kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu utendaji wao.

4.Kuwepo kwa Taasisi Madhubuti: Demokrasia inalenga kujenga taasisi madhubuti kama bunge, mahakama, na tume huru ambazo zinaweza kusimamia mamlaka na kutoa usawa wa madaraka. Hii inasaidia kuzuia ukiritimba wa madaraka na kuhakikisha kuna uwazi na uwajibikaji.

5.Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii: Demokrasia inaweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuweka mazingira ya biashara yenye ushindani, kukuza uvumbuzi, na kutoa fursa za elimu na huduma za afya kwa wananchi.

6.Usawa na Uwiano: Malengo ya demokrasia ni kusukuma kuelekea usawa na uwiano katika jamii. Hii inaweza kumaanisha kujenga sera za kijamii zinazolenga kupunguza pengo la utajiri, kutoa fursa sawa kwa watu wote, na kushughulikia changamoto za ubaguzi.

7.Amani na Utulivu: Demokrasia inalenga kukuza amani na utulivu kwa kuwezesha mchakato wa kisiasa wa amani, kutatua mizozo kwa njia ya mazungumzo, na kudumisha utawala wa sheria.

Demokrasia sio tu suala la kisiasa bali pia ni suala la kijamii na kiuchumi. Elimu, afya, na usawa wa kiuchumi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha demokrasia inafanya kazi kwa manufaa ya wote.

Read More
NDO

Je, Katiba inamtambua mtu mwenye haki ya kupata msaada wa kisheria bure?

Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, Marekebisho ya mwaka 2005, hutoamsingi wa utoaji wa faraja au msaada kwa wananchi waliokumbwa na majanga mbalimbali. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa lugha ya “faraja zinazotolewa na serikali” inaweza kumaanisha mambo mengi, ikiwa ni pamoja na msaada wa kijamii, huduma za dharura, na hata msaada wa kisheria.

Vifungu vya Katiba vinavyohusu haki za binadamu na wajibu wa serikali kwa wananchi wake. Baadhi ya vipengele muhimu ni.

Ibara ya 9, Inaelezea haki za msingi za binadamu na wajibu wa kila raia kuzingatia haki za wengine na kanuni za kijamii.

Ibara ya 14, Inalinda haki ya usalama wa mtu na mali yake. Hii inaweza kumaanisha kuwa serikali ina jukumu la kuchukua hatua za kutosha kuhakikisha usalama wa raia wake, ikiwa ni pamoja na wakati wa majanga.

Ibara ya 18, Inahakikisha haki ya msaada wa kisheria. Hii inaweza kuwa na maana kwamba wananchi walioathirika na majanga wana haki ya kupata msaada wa kisheria ili kulinda haki zao.

Ibara ya 29, Inalinda haki ya kila raia kupata haki sawa mbele ya sheria. Hii inaweza kumaanisha kuwa serikali inapaswa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata fursa sawa ya kupata msaada, ikiwa ni pamoja na msaada wa kisheria, wanapokumbwa na majanga.

serikali ina jukumu la kutoa faraja na msaada kwa wananchi waliokumbwa na majanga mbalimbali. Msaada huu unaweza kujumuisha si tu huduma za dharura na msaada wa kijamii bali pia msaada wa kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 18. Wananchi wanapaswa kupata haki sawa mbele ya sheria, na serikali inapaswa kuhakikisha kuwa haki hizi zinalindwa hata wakati wa majanga.

Je, Katiba inatambua haki ya mtu kuwa na mwakilishi wa kisheria?

Read More
GOLD

Katiba ya Tanzania inatoa misingi ya udhibiti wa maliasili na utalii kwa manufaa ya nchi

Katiba ya Tanzania haitoi sheria moja kwa moja bali inatoa misingi na mwongozo wa jumla ambao huongoza utungwaji wa sheria na sera za udhibiti wa maliasili

Katiba inasisitiza uhifadhi wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Hii inaelekezwa kwenye sheria na sera zinazolenga kuhakikisha matumizi endelevu na uhifadhi wa maliasili.

Hoja hii inaweza ikachambuliwa na baadhi ya vifungu na ibara zifuatazo katika katiba ya Tanzania.

Uhifadhi wa Rasilimali na Mazingira.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina sehemu inayotambua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na rasilimali asilia. Ibara ya 9(1)(b) inasema kuwa, “Serikali itahakikisha kuwa rasilimali za nchi zinahifadhiwa na kutumika kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo”

Mamlaka ya Ardhi na Maliasili.

Ibara ya 8(1)(b) ya Katiba inampa Rais mamlaka juu ya ardhi na maliasili zote nchini. Hii inamaanisha kuwa Rais anaweza kutumia mamlaka yake kuhakikisha uhifadhi na matumizi bora ya maliasili kwa faida ya taifa.

Sheria za Udhibiti.

Katiba inatoa mwongozo wa kisheria kwa kuwezesha Bunge kutunga sheria zinazosimamia uhifadhi wa maliasili na utalii. Sheria hizi zinaweza kugusa masuala kama uhifadhi wa wanyamapori, misitu, na mambo mengine yanayohusiana na maliasili.Haki za Wananchi.Ibara ya 27(1) inatambua haki za wananchi kushiriki katika maendeleo ya nchi. Hii inaweza kutafsiriwa kumaanisha kuwa wananchi wana haki ya kunufaika na maliasili na utalii wa nchi yao

Misingi ya Ustawi wa Jamii.

Ibara ya 9(1)(a) inasisitiza kuwa rasilimali za nchi zinapaswa kutumika kwa njia inayosaidia ustawi wa jamii. Hii inaweza kumaanisha kuwa matumizi ya maliasili na utalii yanapaswa kuchangia katika maendeleo ya wananchi.

Je, Katiba inaweka mipaka au miongozo kuhusu uwekezaji wa kigeni katika sekta ya utalii na maliasili?

Read More
SDDSD

MSAADA WA KISHERIA BAADA YA MAAFA YA KITAIFA KWA WAHANGA

Sheria inatoa mwongozo wa jinsi serikali inavyopaswa kushughulikia na kurejesha hali ya kawaida baada ya maafa kutokea. Masuala ya maafa na utawala wa dharura yanaweza kushughulikiwa katika vipengele kadhaa vya Katiba na sheria nyingine nchini.

Baadhi ya vipengele vinavyohusiana na maafa katika Katiba ya Tanzania:

Ibara ya 10: Inaelezea kanuni za msingi za utawala wa sheria na inaweza kutoa muktadha wa jinsi serikali inavyopaswa kushughulikia masuala ya dharura na maafa kwa kuzingatia kanuni za haki na sheria.

Ibara ya 11(1): Inaelezea kwamba mamlaka ya nchi inatokana na wananchi, na mamlaka hiyo inatekelezwa kwa mujibu wa Katiba. Hii inaweza kutoa msingi wa kisheria kwa hatua zinazochukuliwa wakati wa maafa.

Ibara ya 17(1): Inaelezea haki ya kuishi na haki nyingine za msingi za binadamu. Hii inaweza kuwa na uhusiano na masuala ya maafa na jinsi serikali inavyopaswa kulinda haki hizi wakati wa matukio ya dharura.

Ibara ya 32: Inaelezea haki za msingi za mtu mmoja mmoja wakati wa dharura. Inaweza kutoa mwongozo kuhusu jinsi haki za raia zinavyopaswa kuheshimiwa wakati wa maafa au utawala wa dharura.

Ibara ya 44(1)(f): Inaelezea mamlaka ya Rais kutangaza hali ya dharura na kuelezea kwamba Katiba inaweza kutoa mamlaka ya kuchukua hatua za dharura.

Je, Sheria hizi zinamanufaa ya kina kwa mwananchi na je kwa uelewa wako zinahitaji marekebisho, na kwa namna gani?

Read More