Category: Uchumi

MAH

YALIYOJILI KATIKA HUKUMU YA KESI YA KUPINGA MKATABA WA UWEKEZAJI WA BANDARI 10 AUGUST 2023

No 1

Majaji wote watatu wameingia muda huu saa 3:42.

Majaji;

Mhe. Ndunguru 

Mhe. Ismail 

Mhe. Kagomba

Wakili wa serikali anatambulisha mawakili wa pande zote mbili. Na wote wako tayari kupokea hukumu.

Mahakama imetulia kwa ukimya mkuu.

Majaji wanazungumza kidogo, Mhe. Ismail na Ndunguru.

Kisha, Jaji Kagomba na Ndunguru pia wanazungumza kidogo.

Wanaendelea kuandika.

Karani wa Mahakama leo ni MAPUNDA

Majaji wanasema wako tayari kusoma hukumu na kwamba itasomwa kwa kiswahili

Jaji Ndunguru: Kabla ya kuanza usililizwaji huo, Mawakili wa pande zote mbili waliunda kwanza viini vya kuamuliwa (Issues) pamoja na kiini kimoja ambacho kiliongezwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wameeleza kwamba Bunge lilitoa taarifa kwa umma ili kupata maoni, na wamesema kwamba watu 72 walijitokeza kutoa maombi.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa njia ya mdomo, mawakili wa pande zote mbili wakiwakilisha wadaawa.

Jaji Ndunguru anaanza kusoma hukumu.

HUKUMU YA MAHAKAMA 

Katika lalamiko hili waleta maombi wanne ni raia wa Tanzania wameleta maombi haya dhidi ya Mkataba wa Tanzania na Emirati ya Dubai.

 No 2

Kesi Bandari

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi wamejenga hoja kwamba suala hilo ni la ndani ya Bunge.

Mahakama inatambua kuwa Ibara ya 63(3)(e) na Kanuni ya 108(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Jaji Ndunguru: Kukosekana kwa Viambatanisho muhimu kama Mkataba wa IGA katika Tangazo hilo, na kutokea kwa watu 72 tu, ndiyo hoja ya Waleta Maombi.

Jaji Ndunguru: Viini hivyo ni pamoja na kuhoji iwapo Ibara kadhaa ya IGA zinakiuka Ubara ya 1, 8, 28(1)(3) za Katiba ya Tanzania.Pia, kiini kingine kilihoji iwapo IGA ni mkataba

Jaji Ndunguru: Kwa hoja tajwa hapo juu mahakama hii inatupilia mbali hoja za waleta maombi.

Anamaliza kusoma hukumu hiyo .

Watu wanasimama majaji wanatoka.

Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.

Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.

 No 3.

KESI YA BANDARI.

Jaji Ndunguru: Baada ya kupitia hoja za pande zote, tunakubaliana na hoja za wajibu maombi kwamba Bunge halitakiwi kuingiliwa katika majukumu yake..

Read More
JAMA

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 28,2023. SEHEMU YA NNE

 KESI YA BANDARI TAREHE 28 JULAI 2023

Majaji wote watatu wanaingia saa 09: 44 asubuhi Tarehe 28 Juli 2023.

MAJAJI WATATU;

1. Hon. Ndunguru

2. Hon. Ismail

3. Hon. Kagomba

Wote wameinama wanaandika

Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.

MAWAKILI WA SERIKALI;

1. Adv. Chang’a

2. Edson Mwaiyunge

3. Alice Mkulu

4. Stanley Kalokola

5. Edwin Lwebilo

MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI;

1. Mpale Mpoki

2. Boniface MWABUKUSI

3. Philip Mwakilima

4. Livino Ngalimitumba.

WALALAMIKAJI WOTE WAMEFIKA WAPO MAHAKAMANI

1. Alphonce Lusako

2. Emmanuel Chengula

3. Raphael Ngonde

4. Frank Nyarusi.

Anasimama wakili wa serikali na kusema wako tayari kwa ajili ya REJOINDER kama hakuna pingamizi.

Anasimama wakili senior Mpale Mpoki kwamba wako tayari na anaijulisha mahakama kwamba ataanza wakili msomi Boniface Mwabukusi kuwasilisha majibu yake. Atafuata wakili Msomi Livino na atamalizia Wakili Msomi Philip Mwakilima.

Sasa anamkaribisha Wakili  Mwabukusi aendelee.

Anasimama sasa wakili msomi Boniface Mwabukusi ( Mayweather) kwa ajili ya kuwasilisha majibu.

Adv. Mwabukusi: Wakili: Mwabukusi: nitajikita katika issue namba 1, 4 na 5

Wahe. majaji naomba kuelezea kuhusu Capacity to contract. Jambo la msingi sana kwa pande mbili katika mkataba.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walitumia katiba ya Dubai kwamba inaruhusu hiki kilichofanyika, wasilisho hilo sio sahihi kwani ibara ya 120 (1] Cha katiba ya UAE

Kifungu hiki kipo wazi, unapo Montevideo convention, Viena convention. Vinahusu mambo ya kimataifa na sio domestic matter.

Adv. Mwabukusi: Tulitarajia wenzetu watuonyeshe sifa za Dubai kama nchi kimataifa. Mpaka wanafunga mawasilisho yao, hakuna chochote tulichoonyeshwa kinachokidhi matakwa ya viena convention.

Adv. Mwabukusi: Kuhusu hadhi ya ubalozi, hadhi ya nchi m, kama dubai inakiti umoja wa mataifa. Hatujaambiwa sio kwa bahati mbaya, ni kwa sababu havipo.

Waheshimiwa, wenzetu walisema IGA imeeleza kwamba ibara ya 28 ya IGA Imeeleza kuhusu Competence.

Adv. Mwabukusi: In that angle they missed the target.

Wenzetu walisema IGA ni International treaty hivyo inatakiwa kushugulikia kwa sheria za kimataifa sio za ndani. Waheshimiwa majaji.

Adv. Mwabukusi: Kwakuwa wenzetu wameshindwa kuonyesha utu wa kisheria wa DUBAI, hawawezi kutengeneza kitu ambacho kikapata sifa za International teaty.

Adv . Mwabukusi: IGA hii katika ibara 2(1) wenzetu hawajakataa wala kukanusha kwamba huu mkataba wa IGA is a binding agreement unaohusu kuendeleza, kuimarisha, kuendesha na kusimamia bandari za maziwa na bahari.

Adv. Mwabukusi: Ili kuimarisha maeneo ya kiuchumi na shoroba za kibiashara pamoja na miundombinu ambata kuhusiana na Bandari.

Adv. Mwabukusi: Kwa wenzetu kukubali; wamekubali kwamba mkataba huu unagusa Mali asili (Natural resources) za Tanzania ambazo zinagusa sovereign na kunasheria maalumu ziinazolinda permanent sovereign kwenye Natural resources.

Adv.Mwabukusi: Wenzetu hawajapingana na mawasilisho yangu ya sheria za Rasilimali Na.5 ya mwaka 2017 ambayo inatoa sovereignty kwa Watanzania katka rasilimali zao.

Adv. Mwabukusi: Ili kuhakikisha ulinzi wa Rasilimali za nchi. Preamble ya hii sheria ipo wazi ambayo inatoa effect ya article 8(1] 9[f), ya katiba ya Tanzania na wenzetu hawajapinga.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa Sheria hii Na.5 katika Preamble inaakisi ibara 27(1) ya Katiba ya Tanzania kuhusu permanent sovereignty ya Rasilimali zetu.

Waheshimiwa majaji, ukisoma sheria ya maliasili Na 5 na Na 6 za mwaka 2017. Kwenye sheria na 6. Kifungu cha 6(a,b,c)

Adv. Mwabukusi: Maudhui yake ni kuweka usimamizi wa Rasimali za Watanzania kwa watanzania na wenzangu hawajasema hizi sheria kama zimeshafutwa. Sheria hizi bado ni hai na are so fundamental.

Adv. Mwabukusi: Na are forming basis of protection of our natural resources. Ibara zote tulizozitaja kwenye IGA , inakiuka Katiba ya Tanzania.

Waheshimiwa majaji maudhui ya sheria hii yana ukatiba kwani sheria hizi zinafafanua Katiba ya Tanzania Ibara ya 27[1

Adv. Mwabukusi: Wenzetu wanasema Kwa sababu ni International treaty hivyo Viena Convention kutumika na wao walisahau kuwa sheria husika imeweka pia angalizo.

Katika ibara ya 46(1) cha Viena Convention [Quote).

Anasimama wakili wa serikali aitwaye Kalokola anaweka pingamizi.

SA Kalokola: Objection, waheshimiwa majaji msomi hakutumia Ibara ya 46(1) na hawakutumia ibara husika hivyo hatakiwi kutumia ibara yako.

Adv. Mwabukusi: Mwabukusi: wao walisoma kifungu cha Viena convention in absolute na wakasahau kwamba kuna angalizo kwenye VIENA CONVENTION.

Jaji: Tunakubaliana na wakili wa serikali kwamba hiki kitu ni kipya na wao hawana nafasi ya kujibu.

Adv. Mwabukusi: Taifa letu tume-domesticate charter of Economic rate and Duty of the state, under Article 2(1)(2)a, b kwenye sheria ya Rasilimali. Na.6 ya 2019.

Wakili Mwabukusi anasoma hivyo vifungu.

Adv. Mwabukusi: Yametumika maneno Sovereignty na maneno haya hayapo kwa bahati mbaya. Kesi ya SMZ Vs. Machano Hamisi, page 7 paragraph 1 inayoeleza nini maana ya Sovereignty.

Paragraph ya kwanza na paragraph ya mwisho: (isomwe) kwa msisitizo.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walisema IGA ni frame work na kutakuwa na mikataba mingine midogo kwamba HGA ndio zitaweka masharti haikuwa sahihi.

Kwa sababu ibara ya 12 (2) ya IGA imeeleza wazi na naomba waheshimiwa majaji wakati mnatafakari msome ni kinyume cha wenzetu walivyosema.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walisema masuala yanayolalamikiwa yatakuwa kwenye HGA lakini ukweli ni kwamba kifungu cha 12(2) kimeshaweka masharti.

Jaji: Naomba usome 12(1)d.

#Updates kesi ya bandari.

Anaendelea wakili Mwabukusi kuwasilisha majibu yake.

Adv. Mwabukusi: kifungi hiki kimetumia neno shall na hivyo HGA tayari masharti yake yapo kwenye mkataba wa IGA na nawaalika msome Ibara ya 20[3] ya Mkataba wa IGA.

Adv. Mwabukusi: Hii ibara wenzetu wanasema tutaikuta kwenye mkataba wa HGA wakati tayari imeshatajwa kwenye Mkataba wa IGA. Hivyo HGA tayari ipo kwenye Mkataba wa IGA.

Anasimama wakili wa serikali anaweka pingamizi kwamba Boniface Mwabukusi anaingiza jambo jipya.

SA Kalokola: Objection, tunapinga kinachoendelea, ni kubadili pleadings hawakulalamikia ibara ya 23[3) atuonyeshe wapi wamelalamikia hiyo ibara.

Jaji: SA Kalokola, nenda kwenye Originating Summons soma kwenye paragraph 2 kinasomekaje

SA Kalokola: hakuna ibara hiyo ya 20[3) ya Mkataba wa IGA.

Adv. Mwabukusi: Wao waliwasilisha kuhusu HGA kwamba HGA itafanyika baada ya MKATABA wa IGA na mimi ninajibu kwenye hoja waliyoiwasilisha.

SA Kalokola: waheshimiwa majaji akijielekeza kwenye ibara ya 20, 21 ya mkataba wa IGA Na sio Ibara ya 23(1].

Jaji: Kuanzisha hoja mpya katika Rejoinder ni kukuza mjadala naomba juelekeze kwenye hoja ambazo sio mpya. Sisi tutasoma nyaraka zote.

Adv. Mwabukusi: Wakati mawakili wa serikali wanawasilisha majibu yao walisema migogoro ya IGA itatatuliwa na mahakama za ndani, lakini ibara ya 20(2]a,e(i)[ii][iii][iv] ya IGA zinaeleza kwamba mabaraza ya kigeni ndio yatashughulikia migogoro baina ya pande mbili.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa majaji, hiki ni kinyume na Katiba ya Tanzania na sheria za nchi zinazohusu rasilimali za nchi.

Kesi na 23 ya TLS ya mwaka 2014 ulioamuliwa mwaka 2019 uamuzi huu haukuzingatia Sheria hizi za Rasilimali za asili Na.5 na 6 za 2017.

Anamaliza wakili Mwabukusi sasa anamkaribisha wakili Livino kuendelea kujibu.

#Updates kesi ya bandari.

Anasimama wakili Livino Ngalimitumba.

Jaji; maana ya jina Ngalimtumba ninini

Adv.Livino: kwa asili sisi ni wakisi na maana ya hili jina maana ake ni Kutatua migogoro.

Mahakama: kichekoooo

Adv. Livino: Wakili : Nitajibu hoja za wakili wa serikali Edwin aliyejibu hoja zangu waheshimiwa.

Kwanza alilalamikia kwamba kitabu cha Rules of Law VRulers of law sikuwapa kopi ili akasome.

Adv. Livino: Ningependa kujibu kwamba alikuwa na muda wa kujiandaa maana alikuja kujibu hoja siku ya pili na Senior wake Wakili Mark alikubaliana na kitabu husika na content zake.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, alieleza kuhusu kanuni zilizowekwa kwenye kesi mbalimbali haswa kunapokuwa na malalamiko kuhusu uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Ni muhimu kulinganisha vifungu vya katiba pamoja na vifungu vinavyolalamikiwa.

Adv. Livino: Alitaka kesi ya AG Vs dickson sana, kesi ya Christopher Mtikila Vs AG 1995.

Na kunukuu maneno yaliopo katika kesi ya mtikila ya 1995 ukurasa wa 34.

Naomba mahakama itambua kuwa katika hizo kesi kulikuwa na issue tofauti na issue tulizonazo leo.

Adv. Livino: Kesi ya Dickson ilieleza kuhusu uhalali wa kifingu cha 145[8] CPA Cap 20 kuhusu issue ya dhamana katika makosa ya jinai.

Kesi ya mtikila, mahaka ilikuwa inatatua hija nyingi, uk.36 par. [g) ilijikita Katika kurekebisha marekebisho ya 8 ya katiba ya Tanzania ya 1977.

Adv. Livino: Kesi zote hizi mbili mahakama ilialikwa kutazama uhalali wa Statutes Act of Parliament na sisi tuko hapa kutazama vifungu vya mkataba na sio statutes na sio bunge.

Adv. Livino: Ni rai yangu kesi alizozinukuu SA Edwin hazipaswi kuwa applied kwenye kesi hii absolute bila kutazama circumstances ya kesi tuliyonayo hapa

Kwa kuwa tunatazama uhalali wa Mkataba, ni kanuni ya wazi kuwa mkataba wowote unaokwenda kinyume na sheria ni mkataba Batili.

Adv. Livino: Kwakuwa tunatazama uhalali wa Mkataba, ni kanuni ya wazi kwamba mkataba wowote unaokwenda kinyume na sheria ni mkataba Batili.

Waheshimwa majaji, mwenzangu alicante kesi ya SMZ Vs. MAchano Hamisi na wenzake, katika ukurasa wa 17 haswa kwenye tafsiri ya Sovereignty.

Adv. Livino: Tunakubaliana kwamba tafsiri husika ni sahihi kwakuwa ndio standard ya sheria za kimataifa.

Ningependa kukumbusha mahakama na wakili wa serikali Edwin kwamba issue zilizokuepo katika hiyo kesi, inapatikana katika page na 4 na 12 ya hiyo hukumu. Mahakama inaeleza.

Adv. Livino: Kwamba watuhumiwa hawa walikuwa wameshitakiwa kwa makosa ya uhaini ya kumuondoa Raisi wa Zanzibar.

Na page namba 12 paragraph 3 inaeleza kama Zanzibar ni Sovereignty state (Is zanzibar a Sovereign state.

Adv. Livino: Katika hilo naungana na wakili wa serikali kalokola alieleza kuwa muundo wa Emirates of Arabs inafanana kabisa na muundo wa Tanzania.

Hivyo Dubai haina mamlaka ya kuingia mkataba wa kimataifa kwa kuwa sio sovereign.

Adv. Livino: Wakati wakili wa serikali anawasilisha majibu yao alisema hatuwezi kupoteza Sovereignty kwa kuwa Tanzania ilipata uhuru 1961. Namkumbusha kwamba huo mwaka wa 1961 Tanzania haikuwepo.

Adv. Livino: Tanzania iliundwa 1964 Kwa hiyo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika ilipoteza sovereignty zanzibar ilipoteza sovereignty na kuunda Tanzania yenye sovereignty kama nchi moja.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, Mwenzangu alielezea Ibara 6(2) ya IGA kwamba Tanzania inaweza kuinterfere DP WORLD. Sisi tunapenda kusisitiza kwamba ibara hiyo imeweka interference Conditionally.

Adv. Livino: Kwamba interference lazima ieleweke na pande zote mbili na zjnapaswa kukubaliwa na pande zote mbili.

Hivyo Tanzania ikikubali kwamba kuna mgogoro na wenzetu wasipokubali maana yake Tanzania haita fanya interference. Hii inapoka sovereignty kama nchi.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, ni ukweli kwamba uandishi wa kifungu hiki unanyang’anya Sovereignty kinyume na ibara ya 1,8 na 28 ya Katiba ya Tanzania.

Kama nchi inawekewa vikwazo vya kujilinda kwa namna yoyote IGA ni batili.

Adv. Livino: Kuhusu ibara ya 8(2] ya IGA issue ya Land Rights alisema tusome tafsiri na anakubali kwamba sheria za nchi haziruhusu mgeni kumiliki ardhi.

Adv. Livino: Namkumbusha kwamba tafsi aliyoitaja ya IGA kuhusu land Rights. Ni mtizamo wetu kwamba inaongelea Ownership of land na inampa mgeni haki ya Occupancy of land.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, tafsiri ya ibara husika, ni mtizamo wetu kwamba sheria zetu zinaeleza kuhusu occupancy. Ukisoma kifungu cha 8(1)[2] vifungu hivi vinakusudia kumpa title DP WORLD Ku-occupancy land in Tanzania.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, wenzetu walieleza ibara ya 66 ya Viena Convention ambayo inaeleza kuhusu kutatua migogoro kati ya nchi zilizokuwa katika nakubaliano.

Imeeleza kuwa kuna kwenda ICJ na pili ni ARBITRATION na migogoro chini ya IGA itakwenda kwenye mabaraza ya nje.

Adv. Livino: Ni mtizamo wetu kwamba uwepo tu wa vifungu vya IGA vjnavyoelekeza utatuzi wa migogoro katika mabaraza ya nje ni kitendo kinachokinzana na sheria za nchi kama Senior wakili mwabukusi slivyosema hapo awali.

Adv. Livino: Serikali wakati inaenda Dubai kufanya mazungumzo na DP World ilitakiwa kuwa na duty bind ya kuzingatia sheria za nchi yetu na kwa mantiki hiyo IGA inakuwa batili tangu mwanzo kwa kuwa sheria hazikufuatwa.

Adv. Livino: Ibara ya 21(3) ambayo inakataza Tanzania kujiondoa katika mkataba mpaka ridhaa ya DP WORLD ni mtizamo wetu kwamba kifungu hiki kinapoka sovereignty kama nchi

Ibara ya 23[4] isomwe pamoja na 23(4] kwamba mkataba huu hautaruhusiwa kuvunjwa inapoka sovereignty ya nchi.

Adv. Livino: Wenzetu walieleza juu ya Termination ibara ya 54 ya Viena convention. Ni maoni yetu kwamba ibara hii isomwe na ibara ya 60 ya Viena convention.

Waheshimiwa majaji, IBARA 23[4] wa IGA inasema mkataba huu haupaswi kuvunjwa hata kama kuna uvunjwaji wa terms za mkataba.

#Updates kesi ya bandari,

Anaedelea wakili Msomi Livino kujibu hoja zake.

Adv. Lovino: Tunaomba mahakama hii itambue kwamba hata VIENA CONVENTION Imevunjwa ambayo ilikuwa basis ya submission yao.

Adv. Livino: Wahe.majaji,wenzetu walieleza kuhusu nchi yetu kutii masharti ya kimataifa na serikali pamoja na Bunge ilitekeleza hilo.

Ni msimamo wetu kwamba ibara ya 14 ya Viena convention inatamka kwamba sovereignty ya mataifa iheshimiwa na Sheria za ndani ziheshimiwe.

Adv. Livino: Hivyo ni mtizamo wetu kwamba malengo ya kufanya ratification ya IGA kwa mujibu wa sheria za kimataifa na ndani hayakuzingatiwa.

Tunaomba mahakama hii itamke kuwa mkataba wa IGA imevunja pamoja na Viena Convention.

Wakili wa serikali Kalokola anaweka pingamizi kwamba; wenzetu hawakuomba order ya mahakama kwamba IGA imevunja Viena convention.

Jaji : Kwamba usingeomba order kungekuwa na tofauti?

Adv. livino; naondoa prayer husika waheshimiwa.

Adv. Livino: Wakili wa serikali Mr. Edwin alitaja ibara 4(2) ya IGA kwamba hakuna Binding obligation ya Tanzania kutoa taarifa kuhusu fursa za Tanzania. Ningependa kumwambia kwamba Mkata wote wa IGA is a binding document. Na hiyo inaonekama katika ibara 4(2) ya IGA.

Adv. Livino: Wakili wa serikali alisema ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania kwamba ibara hii inaongelea VITA. Alieleza kwa IGA haijaeleza masuala ya Vita.

Ningependa kusema kwamba Dunia imebadilika. Uvamizi wa sasa sio lazima wavamizi wakanyage ardhi ya Tanzania.

Adv. Livino: Uvamizi ni pamoja na uvamizi wa misingi ya uchumi pamoja na vyanzo vya mapato yake kama Rasilimali za nchi ikiwemo Bandari.

Kwa hiyo tunaposema usalama wa nchi na kutambua adui wa nchi. Hatupaswi kuangalia ardhi pekee na nimaelekezo ya kanuni za utafsiri wa Katiba.

Adv. Livino: Kwamba isitafsiriwe kwa namna ambayo inapoteza maslahi ya nchi. Kuna kesi ya Julius Ishengoma ipo naomba musome page 16 ambapo mahakama inaeleza namna ya kutasmfsiri vifungu vya katiba.

Adv. Livino: Ilisema mambo yafuatayo, Katiba itafsiriwe in a Liberal manner, jealously, our people enjoy their rights, will of the people must prevail.

Adv. Livino: Dhumuni letu kwamba katiba itafsiriwe kwa mawanda hayo na tunapoitafsiri ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania kuhusu usalama wa nchi tunamaanisha tusiishie maneno tu yaliyopo hapo kwenye katiba tunapaswa kuakisi mabadiliko ya nchi.

Adv. Livino: Tuko ibara 2(1) ya Katiba Tanzania inaeleza mawanda ya Tanzania (Quote) lakini neno anga halijatajwa hapa.

Na ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania haijataja anga. Swali ni je, Watanzania hawahusiki na anga na hivyo tusideal na anga.

SA Edwin: Objection, Ibara ya 2(1) haikutajwa hivyo tunaomba asiitumie

Livino: Naondoa kwa kuwa mahakama ilisema itasoma nyaraka zote.

Kwa kumalizia ni kwamba mahakama ijielekeze katika nyanja mbalimbali katika kutafsiri Masuala ya Katiba.

Adv. Livino: Kwa kumalizia wakili wa serikali alitaja taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo TBS , uhamiaji n.k lakini ukweli ni kwamba hayo ni maneno yake mwenyewe na wala hayapo kwenye IGA.

Anamaliza Wakili Livino sasa anamkaribisha Philip Mwakilima.

#Updates kesi ya bandari.

Anasimama wakili Philip Mwakilima kujibu hoja

Adv. Mwakilima: Waheshimiwa majaji: nitajikita katika issue na.6 kama IGA ilifuata sheria ya Manunuzi(Procurement Act) na naomba sehemu niliyofanya katika mawasilisho ya awali iwe sehemu ya Rejoinder hii.

Adv. Mwakilima: Wakili Kalokola akirespond kiapo cha walalamikaji kuhusu neno DPW na neno linatakiwa kusomwa ni DP Word.

Adv. Mwakilima: Kutokana na principle za overriding objectives ibara 107A (2)e ya Katiba ya JMT,1977 as amended inaitaka mahakama ijikite katika kutenda haki kwenda kwenye substance na sio legal technicalities.

Adv. Mwakilima: Hivyo typing Error inapaswa kutoathiri haki za wateja wetu.

Katika kiapo kinzani wamekiri kwamba hakukuwa na Mchakato wa kutoa Tenda na pia hawapingi kwamba sheria inayotuongoza mcahakato wa Tenda ni Procurement Act.

Adv. Mwakilima: Ni kwamba wanakili kuwa sheria hiyo imevunjwa.

Waheshimwa majaji wenzetu walitaja kifungu cha 4(1) ya Procurement Act, wakili akiwa amekuja na tafsiri kwamba IGA ni International treaty.

Adv. Mwakilima: Waheshimiwa majaji kifungu husika, there is no any conflict between PROCUREMENT ACT and International treaty. Pia IGA haina sifa ya kuwa International treaty.

Adv. Mwakilima: Kama kalokola alivyosema Zanzibar na Tanzania ni sawa Dubai na Emirates of Dubai. Kwa misingi hiyo hakuna International treat

Kama mahakama itakubaliana na sisi kwamba kifungu cha 64 cha Sheria ya Manunuzi (Procurement Act) Mkataba wa IGA Umekinzana na sheria hii.

Adv. Mpoki: Waheshimiwa imetuchukua siku nne, na research imefanyika. Kuna msemo unasema if you can’t convince them confuse them.

Mahakama: kicheko kidogo 

Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji, tunasubiria uamuzi wenu. Thus all.

Anamaliza wakili Mpoki sasa mahakama inakaa kimya kwa muda.

Majaji Ndunguru: naomba kabla sijatamka tarehe ya maamuzi; kwa niaba ya majaji wenzangu nawashukuru sana Mawakili pande mbili.

Jaji: Kwa kile mlichokionyesha, sisi tumeona the highest level of professionalism namshukuru sana.

Jaji: Naomba pia kipekee nimshukuru wakili Boniphace Mwabhukusi kwa kucheza vizuri sana akiwa ndani ya mahakama na akiwa ulingo wa siasa huko nje. Mwabukusi ameitendea haki taaluma yake.

Baada ya kusema hayo niseme kwamba mahakama hii itatoa hukumu yake siku ya tarehe 7 August 2023 siku ya jumatatu.

Majaji wanatoka.

Read More
MBL

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. MWENDELEZO SEHEMU YA TATU

Kesi Bandari majibu ya Upande wa Serikali

SA Mayunge: Waheshimiwa majaji, Maamuzi ya Diana Rose Vs AG na alisemea viapo vya watu 72 havipo na walitakiwa kuleta viapo:

Haya maamuzi yanategemea na maada inayobishaniwa. Na hoja yao ni suala la muda sio suala la idadi ya watu walioshiriki kutoa maoni. Tujikite kwenye  muda.

SA Mayunge: Kwenye kiapo cha Maria, kwenye verification alisema haya anayoyasema, ni kwa ufahamu wake mwenyewe lakini pia 14.07.2023 tulifile kiapo cha Maria Mpale, kiapo hicho hakikupingwa na kimeeleza uwepo wa watu hao, maoni yalivyotolewa na kikaambatisha maelezo ya Bunge.

SA Mayunge: Waheshimiwa majaji, kwenye annexure OSGAF5 ya Maria Mpale, kuanzia ukurasa wa 6 (Taarifa ya Bunge). Katika taaifa hiyo(anasoma;..)Sehemu hii inaeleza na kukiri  namna maoni yaliyopokelewa na Bunge kutoka kwa wadau yalivyosaidia na walalamikaji hawakupinga suala husika

SA Mayunge: Waheshimiwa kwa upande wetu tumetekeleza mambo yote kwa mujibu wa sheria na hata hivyo walalamikaji hawakuzuiwa kutoa maoni. Naomba niende kwenye issue ya 1 ya mahakama kuhusu ratification na kwangu nimebakiza machache tu.

SA Mayunge: Waheshimiwa majaji: Mkataba huu IGA ni Mkataba ya kimataifa unaoweka misingi na maeneo ya ushirikiano hapo baadae. Nirejee katika ibara ya 5(2] ya IGA Kifupi kinasema: kwamba mkataba huu unategemea mikataba mingine ya miradi na huu ulivyo hauwezi kutekelezwa

SA Mayunge: Waheshimiwa majaji IGA kwa hivi ilivyo haivunji kabisa  sheria ya Rasilimali Na.6 ya mwaka 2017 kwani IGA sio mkataba wa utekelezaji.

Waheshimiwa majaji vifungu vyote vilivyosemwa na wakili Mwabukusi tunaungana navyo lakini havihusiani na Ratification process.

SA Mayunge: Wahe. Majaji, Irene linus &11 others Vs. TPA &another.  Mahakama ya rufaa ilisema sio suala la courtesy bali ni ya lazima. Majaji hawapaswi kutoa maamuzi yanayopingana.Kwa wakati huu mkataba huu upo incapable of violating sheria za Rasilimali,  Act no. 5, 6 za 2017

SA Mayunge: Naomba nirejee annexure OSGOF5 Katika ukurasa wa7(Maelezo ya Bunge); kwamba aina ya ubia, kiasi cha ubia kitakuja baadae na sio mkataba huu wa IGA.

SA Mayunge: Na IGA sio mkataba wa mradi wowote wa Bandari na mikataba ijayo ndio inapaswa kutathiminiwa kama inavunja Sheria za Rasilimali, Sura na.5 na sura na. 6 za mwaka 2017

SA Mayunge: Katika uwasilishwaji wa Mwabukusi alirejea mahakama katika Preamble J” ya mkataba wa IGA then ibara ya 2(1)  inayoongelea maeneo ya ushirikiano na sisi tunaona is fine kuwa na mawanda hayo.

SA Mayunge: Aliongelea Article 4(2] ya IGA Kama ilikuwa na shida sisi tunaona ipo proper. Yani kutoa taarifa kwa DP World kunashida gani? Anamaliza kwa kuuliza hivyo wakili wa serikali Mayunge.

 SA Edwin: Waheshimiwa majaji, kuna malalamiko dhidi ya ibara ya 28 ya katiba. Hii ni ibara inayotoa wajibu kwa watanzania dhidi ya uvamizi wa nchi.

Katika hili lazima kuwa na uthibitisho na lazima ionekane kama kuna vita.

SA Edwin: Na TPA ikiona zinafaaa kwa nchi itaruhusu DP WORLD Kuendelea na uwekezaji na kama itaona haifai haitaruhusu.

Wahe.majaji suala linaloenda kufanyika saizi sio jipya na hata kabla ya DP WORLD Kulikuwa na TICS. 

Anasimama wakili wa wananchi senior Mpoki anaweka pingamizi

SA Edwin: Kwa mujibu wa ibara ya 28 ya katiba inasisitiza lazima kuwepo na Vita, na katika mawasilisho ya waleta maombi hatukuonyeshwa kwamba nchi ipo vitani.

Pia hatukuonyeshwa kwamba tumetia Sain kukubali tumeshindwa vita na adui, hatukuonyeshwa na tumeridhia uvamizi ufanyike.

SA Mark: Waheshimiwa yale yote yaliyoombwa na walalamikaji na hata ukichujua katiba yetu na mkataba unakuta hakuna kifungu kilichovunjwa.

Naomba mahakama itamke kwamba kwa mujibu wa taratibu za bunge, wamanchi walipewa muda wa kutoa maoni kwa mujibu wa sheria.

 SA Mark: Pia itoe tamko kwamba: mkataba wa IGA ni mkataba wa kimataifa na Serikali yetu ilikuwa na haki ya kuingia katika mkataba husika na haufungwi na sheria zetu za ndani. Taratibu zote za ratification zilifuatwa pamoja na uchambuzi wa kamati ya mkataba wa IGA zilikuwa proper

SA Mark: Na vile vile kwenye mikataba ya aina hii haihitaji consideration.

Kuhusu sheria ya mamunuzi ya Tanzania, mahakama itamke kwamba   sheria hii haina nguvu dhidi ya mkataba wa kimataifa (IGA)

SA Mark: Waheshimiwa majaja walalamikaji wameomba maomba takribani 10, tunaomba mahakama itamke wazi kwamba maombi hayapo justified  hivyo not granted.

Walalamikaji wameomba maomba takribani 10, tunaomba mahakama itamke wazi kwamba maombi hayapo justified  hivyo not granted

SA Mark: Waheshimiwa majaji, katika mazingira kama haya tunaomba kupatiwa gharama zetu na pia shauri hili lifutiliwe mbali (To dismiss the petition with cost to the government)

Naomba kama serikali kuwasilisha 

Anamaliza wakili kiongozi wa serikali Bw. Mark.

Adv. Mpoki: Na hichi ndicho kilisemwa katika kesi ya tabora: “Salimu kabora Vs. Tanesco Ltd, ukurasa wa 16” hivyo mahakama kuu haina limited jurisdiction na mnamamlaka ya kuangalia uvunjwaji wa katiba na your defenders of the Constitution.

Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji mna kazi ya kuhakikisha katiba yetu inalindwa na kutovunjwa.

Sasa nije issue ya Constitution: waheshimiwa majaji, wenzetu walitaja ibara ya katiba na sheria na tuna kubaliana nao.

Adv. Mpoki: Lakini kama kweli unataka watu washiriki kuna kanuni kuu tatu [ adequate, sufficient, reasonable) na hakuna hata kimoja kilichotimizwa.

Wanakubali kwamba notice ilitolewa tar 5 June 2023 na kuwataka watu watoe maoni tar 6 June.

Adv. Mpoki: Wanakubali kwamba notice ilitolewa kwa mitandao na wao wanataka tuthibitishe.

Waheshimiwa majaji, the principle is we can’t prove the negative but to disprove by evidence.

Kwa mfano nakuambia sina hela halafu unaniambia proof. You can’t proof the negative.

Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji tukikubaliana nao tutakuwa tuna water down the essence of notice. Anaweza akaja mtu akatoa notice ya masaa mawili kwenye jambo kama hili?

Angalia walioshiriki ni 72, mmoja peke yake ndio alihudhuria na wengine wote  walituma email.

Adv. Mpoki: Wanasema ambaye angefika kutoa maoni angeridishiwa nauli. Lakini tangazo halikutangaza kwamba watao hudhuria watapewa nauli.

Pia wanakubali kwamba waliweka resolution to be adapted lakini hawakuweka mkataba halafu wanaitwa watu kudiacuss mkataba hawapo serious hawa.

Adv. Mpoki anasoma Notice ya bunge ya wito kwa wananchi kutoa maoni ya bandari.

Adv. Mpoki: Nasisitiza kwamba walitaka watu waje kudiscuss azimio la bunge kuhusu mkataba wa bandari ambao wananchi  hawaujui.

Adv. Mpoki: Ni rai yetu kwamba notice haikuwa sufficient kwa kuwa watu wameitwa kudiscuss Azimio tar 05.june kabla halijapitishwa na Bunge tar 10.june.

Hii ilipunguza sana ushiriki wa watu waheshimiwa majaji.

Adv. Mpoki: Wenzetu wametoa kesi 2 za South Africa kuonyesha kwamba ni bunge lenyewe linaweza kuamua kuhusu reasonable  time.

Kwenye kesi ya kwanza waliyoitumia, wao walipewa siku 30 na walilalamika. Sisi notice ya masaa 24 kulalamika sio jambo baya.

Adv. Mpoki: Na kwamba kitendo chochote cha kutoa notice kusifanye public isishiriki kwa namna yoyote kama hii yetu ilivyokuwa.

Pamoja na kwamba ni bunge lenyewe lina ridhaa ya kuweka notice lakini lengo linapaswa liwe kufanya watu washirki.

Adv. Mpoki: Nimalizie kitu kimoja kwamba, kwa sababu wananchi wamechagua wabunge. Wabunge ni wawakilishi wao. It seems very attractive lakini lakini kifungu cha 108[2] ya kanuni ya Bunge Imewekwa ili wananchi washiriki katika kutoa maoni kwenye mambo yanayowahusu.

Adv. Mpoki: Naomba mahakama hii isichukulie maanani kwamba wabunge wenyewe ndio wanapaswa kushiriki na ndio msingi wa kanunu ya 108[2]  ya kanuni ya bunge na haitakiwi kuwa kiini macho.

Adv. Mpoki: Na mwishoni  wenzetu katika submission zao wamesema kwa sababu hatukujibu majibu yao hivyo Tumekubaliana. Ni kanuni kwamba mwenzangu akisema mimi nikibisha ndio msingi wa kukutana mahakamani.

Adv. Mpoki: Kwa misingi hiyo hakukuwa na msingi wa sisi kujibu jambo ambalo tushalibishia awali na wao wamejibu na ndio maana tupo hapa.

Waheshimiwa baada ya kusema hayo naishia hapo na namualika msomi Mwabukusi aendelee.

Baada ya wakili Mpoki kumaliza kujibu hoja za mawakili wa serikali, mahakama inaairishwa mpaka  asubuhi saa 09:00 ya Tarehe 28Julai 2023 ambapo wakili Boniface Mwabukusi ataendelea kujibu hoja za mawakili wa serikali.

Tukutane kesho asubuhi hapa mahakama kuu Mbeya.

ASANTENI MUNGU AWE NANYI JIONI NJEMA.

Read More
KIPA

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA TATU

TAREHE 27 JULAI 2023 MAJAJI WANAINGIA MUDA  SAA 09: 44 ASUBUHI.

MAJAJI WATATU;

1. Hon. Ndunguru

2. Hon. Ismail

3. Hon. Kagomba

Wote wameinama wanaandika

Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.

MAWAKILI WA SERIKALI;

1. Adv. Mark Muluambo

2. Edson Mwaiyunge

3. Alice Mkulu 

4. Stanley Kalokola

5. Edwin Lwebilo.

MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI;

1. Mpale Mpoki

2. Boniface MWABUKUSI 

3. Philip Mwakilima 

4. Livino Ngalimitumba.

Anasimama wakili kiongozi wa serikali Mr. Mark na kuijulisha mahakama kuwa wako tayari kuendelea na majibu yao.

Mahakama inaruhusu.

SA Kalokola: waheshimiwa naendelea na hoja namba 6 kama mkataba huu IGA ulizingatia sheria ya Manunuzi (Procurement Act)

SA Kalokola: Hoja hii inatokana na ombi na 4 ya Origjnating summons kwamba IGA haikuzingatia Sheria ya Manunuzi.

Na katika aya ya 12, walalamikaji wanasema kuna tender inetolewa kwa DP WORLD Kinyume na sheria za manunuzi.

SA Kalokola: Majibu yetu yapo katika aya ya 14 ya kiapo cha  Mohamed Salumu kwamba; Hakuna tender iliyotolewa na hakuna majibu yaliyoletwa na wenzetu kupinga hili.

Waheshimiwa majaji wenzetu waliandika jina la kampuni DPW na sisi tunajua kuwa kuna kampuni ya DPW Na hawakukanusha

SA Kalokola: Pia kwa Kuwa Mkataba wa  IGA ni mkataba wa Kimataifa unasinamiwa na sheria za kimataifa hivyo sheria ya manunuzi haiwezi kutumika bali sheria za kimataifa.

SA Kalokola: Waheshimiwa Mkataba huu ni framework agreement ni mkataba wa ushirikiano  wenye mifumo ya uwekezaji kitu ambacho hakiwezi kuhusiana na dhana ya manunuzi kana kwamba kuna nchi inamnunua mwengine.

Hivyo wenzetu hawakupaswa kulazimika kuja na hoja ya kimanunuzi.

SA Kalokola: Wakili Mwakilima alisema kuhusu sheria ya manunuzi naomba tuongozwe  na kifungu cha 12 cha Tanzania Port Act. Kunachozungumzia Kazi za TPA.

Majukumu ya TPA ni kupromote local &FOREIGN  investment kwenye bandari. Na kama wenzetu wangeanzia katika dhana ya uwekezaji.

SA Kalokola: Kunapokuwa na International obligations  na inakinzana na sheria za ndani, Sheria za kimataifa zitasimama dhidi ya sheria za ndani hivyo masharti yaliyopo kwenye IGA yanasimama.

SA Kalokola: Na kwamba Mkataba wa IGA haukuzingatia matakwa ya sheria ya manunuzi is a misconception (Kupotoka).

Yaani wametumia dhana fulani kwenye eneo ambalo sio mahala pake. Hivyo hoja ya 4 na 5 na 6 kwenye matumizi ya mikataba nimejibu hivyo na naomba hoja zangu zizingatiwe

SA Kalokola: Waheshimiwa majaji Walalamikaji wameshindwa kuthibitisha hoja zote tatu na niombe mahakama irejee kwa shauri la Center for strategic litigation Ltd & another Vs. AG and others.

Anamaliza wakili wa serikali Bw. Kalokola sasa anamkaribisha wakili mwingine wa serikali kuendelea kujibu.

Anafuata wakili wa serikali aitwaye Mayunge.

Sasa ni zamu ya wakili wa serikali aitwaye Mr. Mayunge na ni wakili wa tatu wa serikali katika kuwasilisha majibu kwenye kesi hii ya bandari.

SA Mayunge: amekaribishwa na anaendelea. Nitaanza kujibu hoja namba 2 ya Senior Mpoki:

SA Mayunge: Waheshimiwa, Nikirejea ibara ya 21(1] ya Katiba ya Tz, kimsingi inaelezea kuchagua na kuchaguliwa kwa wabunge na kwamba ni wawakilishi wa wananchi.

Pia ibara ya 63(2] ya Katiba ya Tz, maudhui yake ni kwamba Bunge linasimama kwa niaba ya wananchi kuisimamia serikali

SA Kalokola: Nirejee pia ibara ya 63(3]e ya Katiba Tanzania inayotamka kwamba; utekelezaji wa madaraka ya  Bunge: ni kujadili na kuridhia mikataba.

Nirejee 89(1],(2] ya Katiba ya Tanzania, inayosema bunge litatunga kanuni za kudumu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake.

SA Mayunge: Ibara ndogo ya [2) Bunge kutunga kanuni ndogo za utekelezaji lakini pia ibara ya 96inayoeleza: BUNGE Laweza kuunda kamati mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza madaraka ya Bunge.

SA Mayunge: Waheshimiwa, kutokana na ibara ya 89(1] Bunge la JMT limetunga kanuni za kudumu kama ilivyoelekezwa mfano kanuni ya 108 ambayo nitasoma kanuni ndogo ya 2.(Quote as its )

SA Mayunge: Waheshimiwa katika kiapo cha Maria ambacho pia ni kiapo cha Bwana Salum, serikali iliwasisha Mkataba wa IGA bungeni kwa ajili ya ratification.

Katika aya ya tatu anaeleza jinsi serikali ilivyopeleka mkataba Bungeni kupitia barua iliyoambatanishwa.

SA Mayunge: Pamoja na yote yaliyoandikwa naomba nisome aya ya kwanza: Baada ya kukamilika shughuli za serikali, Kutokana na umuhimu wake tunaomba kuwasilisha shuguli 7 ili Bunge lifanyie kazi kwa mambo yafuatayo.

SA Mayunge: 1. Kuazimia azimio la serikali kuingia Mkataba wa IGA na DP WORLD From Dubai. Baada ya hapo kanuni ya 108[2] ikaanza kutekelezwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na bunge.

SA Mayunge: Na bunge ilialika wadau ili watoe maoni yao kupitia Notice iliyoambatanishwa kwenye kiapo cha Maria, kiambata OSGF2 Kwenye aya ya 5.

Wahe. majaji naomba nisome kiapo husika ili muone kama it was reasonable

Majaji : wanamruhusu

Wakili: Serikali: anasoma barua husika

SA Mayunge: Kwa ujumla notice inahusu Mkutano wa Kupokea Maoni dhidi ya mkataba wa IGA.

Waheshimiwa majaji, hili tangazo waliliona waleta maombi na niwao wameeleza katka kiapo chao, aya ya 11 walivyopata tangazo hilo.

SA Mayunge: Na katika kiapo chao hawajasema muda ulikuwa mfupi sio kwamba uliwazuia kutoa maoni na hawajasema chochote.

Na hatujua walalamikaji wanalalamika kwa niaba ya nani na hwapo hapa kwa niaba ya nani.

SA Mayunge: Waheshimiwa majaji wenyemaoni walikuepo japo hawakuwa wao na ndio maana waheshimiwa majaji katika aya ya 7 ya kiapo cha Maria kimesema watu 72 walitoa maoni.

SA Mayunge: Wale waliokuwa wanataka na wakatoa maoni, sasa haya maombi haya ni just speculations, na hata hawakushiriki kutoa maoni lakini wanalalamika.

Na hakuna hata malalamiko ya barua ya kuomba kuongezewa muda wa kukusanya maoni.

Jaji: kwahiyo unasema muda ulikuwa reasonable?

SA Mayung:  it was duly saved, adequate and reasonable na waheshimiwa sasa ni wakati wa utandawazi mtu anaweza kutoa maoni yake popote kuputa barua pepe.

SA Mayunga: Waheshimiwa waliotoa maoni walitoka Mwanza, Arusha, na sehemu mbalimbali za nchi wote hao walitoa maoni yao.

Katika kanuni ya 108(2] ya Kanuni ya Bunge haikutoa kabisa suala la muda na kunasababu zake nitafafanua.

SA Mayunge: Waheshimiwa kwanin tuna tunasema muda ulitosha: ni Bunge lililohitaji maoni kutoka kwa watu.

BUSARA YA BUNGE; Bunge kwa busara zao waliona muda waliotoa unatosha kwa watu kutoa maoni yao dhidi ya Mkataba wa IGA.

SA Mayunge: WAHESHIMIWA suala la reasonable linategemea mazingira, umuhimu, uharaka na mengine mengi ngoja nitaje kidogo.

Suala la Reasonableness kwa masuala ya Bunge, mahakama kadhaa kutoka sehemu mbalimbali duniani zimejadili suala hili na tusiwe tofauti na mahakama zingine.

SA Mayunge: Naomba turejee Uamuzi wa Africa kusini Doctor for life .V. Speaker of National Assembly &Others katika ukurasa wa 70, paragraph  2.

Mahakama ilisema: reasonableness is…..(anasoma) kimsingi reasonableness  inategemeana na mambo kadhaa.

SA Mayunge: Kwamba mahakama haiwezi kuipangia bunge. Kwamba Bunge ndio lilihitaji maoni na ndio linalojua kiwango cha ushirikishwaji wa wananchi na vile vile mahakama haitegemei kulibishia Bunge kuhusu reasonableness

SA Mayunge: Waheshimiwa  hivyo masuala ya kutaka miezi sijui 6 kwa ajili ya maoni hiyo ni busara ya Bunge na si vinginevyo.

Jaji: Nani kasema miezi 6

Wadau: wanacheka 😂

Adv. Mpoki: Hizo ni imagination  zake Waheshimiwa  majaji.

Read More
MBY

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA PILI

 #Updates kesi ya bandari


—Sasa ni saa 14: 45 mchana Juli 26,2023 Majaji wanaingia,.. karani anataja namba ya kesi ambao ni kesi no.05/ 2023.

..Mahakama inakaa kwa utulivu kidogo huku majaji wakiandika.

#Kesi_Ya_Bandari.

Anasimama wakili wa serikali kuomba kuanza kujibu hoja za waleta maombi.

SA = wakili wa serikali

SA Mark : Waheshimiwa majaji

W: Serikalin: Mark; waheshimiwa majaji naomba mahakama iangalie vitu gani vinapaswa kuangaliwa katika kesi ya kikatiba.

Issue ya 1, 2 Edson atawalisha, issue 4,5 na 6 itawasilishwa na kalalokola, Edwin issue 3,

Waheshimiwa maombi yameletwa chini ya ibara ya 108(2) ya Katiba ya Tanzania na Kifungu cha 2(3) cha JALA Kutumia Originating Summons na kiapo

SA Mark: Kwa sasa tunaomba kibali cha mahakama tukufu ili majibu yetu na kiapo kinzani zitengeneze sehemu ya majibu yetu kinzani. Shauri hili linapinga uhalali wa kikatiba wa kutia sahihi na kuridhia mkataba wa kimataifa (IGA) baina ya nchi mbili. Tunawashukuru wenzetu kwa submission yao kwa sa babu kuna maeneo tunakubaliana nao mfano umuhimu wa kufuata na kuheshimu katiba. Waheshimiwa tumependezwa na wenzetu kutumia kitabu chenye maandiko ya Samata J” kitabu cha Rule of Law Vs. Rulers of Law: kuishi kwa kufuata utawala wa katiba ni wokovu na sio utumwa. Tunaamini wananchi wote wanakubaliana kwamba lazima tuishi kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

SA Mark: 

Waheshimiwa majaji Katiba hii niliyoishika imeipa mahakama jukumu kubwa chini ya ibara ya 107A kama chombo cha juu cha utoaji haki. Anasoma kifungu husika (107A). Nachojarubu kusema hapa: Katika kutoa haki mahakama inapaswa kufuata sheria.

Kazi kubwa ya mahakama ni kufanya uamuzi kudetermine kama kitendo kilichofanywa na serikali kinavunja Katiba yetu ya Tanzania. Kazi kubwa ya mahakama ni kufanya uamuzi kudetermine kama kitendo kilichofanywa na serikali kinavunja Katiba yetu ya Tanzania.

SA Mark: 

Na ili mahakama ifanye hivyo inapitia pleadings zote zilizoletwa na kuangalia kama imepita Threshold ya kuthibitisha kesi ya kikatiba. Na hiki hakiwezi kufanyika ikiwa waleta maombi hawataleta kifungu cha katiba kilichokiukwa na kuonyesha kiasi gani kifungu husika kimekiukwa. Waheshimiwa ni mahakama yenyewe imetamka hili katika maamuzi mbalimbali hivyo ni vizuri tulaweka msingi huo na ueleweke. Katika shauri la AG Vs Jeremiah Ntobesya. Rufaa ya madai, 65/2016 ukurasa wa 46 mpaka 47 mahakama wakati ikikubaliana katika shauri la KIKATIBA ilitamka.

SA Mark: Mahakama ilisema kama kuna vifungu vimekiukwa, Mahakama kuu inachukua vifungu vya sheria vinavyosemwa, unaviweka pamoja na Vifungu vya katiba ili kuona ubishani. Na mahakama haipitishi wala kulaani shauri lolote linalopitishwa na Bunge kazi yake ni kuangalia kama vifungu vinakiuka katiba.

SA Mark: Waheshimiwa majaji, Shauri hili halichallange kupitishwa kwa sheria iliyopitishwa na Bunge wanachallange makubaliano. Ni vema mahakama hii ikaendelea kutambua, wenzetu wameleta shauri hili chini ya ibara ya 108[2] wakisema mahakama inamamlaka ya mahakama ya kusikiliza yale yote yaliyoletwa. Hatuna ubishi kwenye ibara husika, pia kuna ibara 30(3] ya Katiba pia inaipa mahakama kusikiliza.

Wakili Mpoki anaweka pingamizi anasema: Waheshimiwa tushaamua kuhusu Mapingamizi na wameondoa jana na naona anafanya submission ya “PO” kana haina mamlaka tufunge mabegi yetu tuondoke.

SA Mark: Sio nia yangu kuongelea PO, nachotaka kusema: mahakama iangalie mazingira yote na kujiridhisha kwamba ibara ya 108 ni sahihi na kujiridhisha vifungu bishaniwi Waheshimiwa majaji, nilikiwa nasema ni wajibu wa mahakama kufanya maamuzi kwa Mashauri yanayoletwa chini ya ibara ya 108(2) ya Katiba ya Tanzania, 1977.

Adv. Mpoki: Basi naomba afute maneno yanayosema mahakama ina limited jurisdiction

SA Mark: Tunaomba muongozo katika hili, haya sio maneno yangu, ni naneno ya maamuzi ya mahakama ya rufaa. Yangekuwa yangu ningeyafuta Naomba muongozo

Jaji : PO zilishaamuliwa kwa hiyo tunaregard kama submission endelea

SA Mark: Ninani anayetakiwa kuthibitisha; anayetakiwa kuthibitisha katika shauri la kikatiba ni mleta malalamiko.

SA Mark: Katika shauri CHRISTOPHER Mtikila V. Ag. 1995 TLR 31Page 34 inasema: ukiukwaji wa katiba ni jambo kubwa lazima uwe na ushahidi wa hakika

[7/26, 15:30] Wakili Livino Ngalimitumba: Pia katika kesi ya Center for Strategic litigation & Another Vs. AG and Anather page 40-41, Mahakama kuu ilikuwa na haya ya kusema; Pamoja na ku-cite kifungu cha katiba, ni lazima kusoma kifungu cha katiba kilichokika na namna kilivyoathiriwa na kinatakiwa kuwekwa kwa namna haina shaka.

SA Mark: Shauri ishengima, Francis ndyanabo Vs. AG ,2004 page 14 inasema: (Quite): kimsingi wanaongelea kwamba Kila kifungi cha katiba kinauhalali na yule anayesema kifungu kinamnyima haki lazima afanye hivyo. Tunaiomba hii mahakama isiamue kama IGA inavunja sheria zetu za ndani. Naomba nimkaribishe msomi Kalokola kwa mawasilisho.

—Sasa ni zamu ya wakili wa serikali Kalokola.—

SA = kifupisho cha wakili wa serikali.

SA Kalokola: 

Waheshimiwa nitajielekeza kwenye hoja namba 4 iliyotengenezwa na mahakama on where IGA is a contract. Nitajikita na kuongozwa na vitu vifuatavyo: MONTEVIDEO CONVENTION ON THE RIGHTS AND DUTIES OF STATE, Pia VIENA CONVENTION ambayo iliridhiwa na Tanzania, pia nitaongozwa na Mkataba wenyewe. Nitarejea Katiba ya Tanzania, 1977 toleo 2005 na mwisho nitaelezea Katiba ya umoja wa Falme za kiarabu katika kujibu hoja husika. Na mwisho kabisa hati ya madai ya walalamikaji. Waheshimiwa Majaji, kwenye ground ya kwanza walalamikaji wamuita as International agreement. Na ukienda kwenye maombi yao wanautambua kama International Agreement. Na walalamikaji wakatupa ushahidi wao.

SA Mark: 

Katika aya ya 5 wanasema, mjibu maombi wa pili ni Waziri amesaini mkataba wa Kimataifa. Kwa hiyo mpaka sasa walalamikaji wanautambua kama mkataba huu ni mkataba wa kimataifa. Hoja inayofuata; Je Mkataba wa kimataifa unaongozwa na sheria zipi; kujua mkataba wa kimataifa unaongizwa na sheria zipi nitataja sheria za kimataifa. Nitaanza na VIENA CONVENTION 1966 ambapo Tanzania ni mwanachama baada ya kuridhia. Ibara ya 2(a) Viena Convention on laws and treaties inajibu tafsiri ya Mkataba wa kimataifa. Unaposema mkataba ni wa kimataifa Tambua kwamba mkataba huo utasimamiwa na sheria za kimataifa. Mkataba huu uliingiwa na Nchi mbili Emirate of Dubai na Tanzania kama mkataba wa Kimataifa. Wakili Mwabukusi alijikita katika kuridhiwa kwa Mkataba na katiba ya kiswahili inatumia neno Mkataba ibara 63(3)e ya Katiba inatumia neno:

SA Kalokola: 

Wakili Mwabukusi alijikita katika kuridhiwa kwa Mkataba na katiba ya kiswahili inatumia neno Mkataba ibara 63(3)e ya Katiba inatumia neno: Bunge linaweza kuridhia mikataba. Sheria ya kimataifa huu mchakato wa ibara ya 63(3)e ni mchakato unaoitwa ratification of International agreement. Ibara ya 2b ya Viena Conv,1966 inazungumzia ratification hivyo mkataba huo IGA inatakiwa kupitia mchakato wa kuridhiwa kama ibara ya 63(3)e ya Katiba ya Tanzania. Ilikujua hadhi ya mkataba huu, ibara ya 25(2) ya IGA inasema hivi

(Quote): Serikali za nchi mbili ndani ya siku 30 baada ya kusainiwa unahalalisha bindingness under international law. Kila mhusika kwa taratibu zake na sheria za ndani ufanye ratification ili uwe na hadhi ya sheria za kimataifa Na ndio sababu ya IGA kupelekwa Bungeni. Na ndio maana mbele yenu kunamalalamiko ya namna IGA ilivyoridhiwa. Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.

SA Kalokola: 

Na sheria za ndani hazina nguvu dhidi ya mikataba ya kimataifa
[7/26, 16:03] Wakili Livino Ngalimitumba: 

Waheshimiwa hoja ya pili kuhusu Capacity to contract. Mwabukusi alitumia ibara 103 ya katiba ya umoja wa falme za kiarabu na ibara ya kwanza alitumia Montevideo convention. Vile vile alitumia ibara ya 123 ya katiba ya Dubai kusema Emirate inauwezo au la kuingia kwa mkataba. Nianze na Ibara ya 123 ya Katiba ya Emirate inasema (Quote) inaorodhesha mambo ya muungano kuhusu members of Emirate wanaweza kufanya makubaliano na nchi zingine. Ibara hii inazungumzia suala la foreign relation kwenye mambo yao ya muungano ni jambo la muungano

SA Kalokola: 

Hoja ya kujiuliza ni kwamba je mkataba huu umeingia in capacity of Foreign investment au international investment: Mkataba huu IGA unahusisha masuala ya uwekezaji ndio maana wanasema muwekezaji anapewa vyote.

SA Kalokola: 

Ibara ya 116 ya United Arabs Emirates inasema the Emirates shall exercise all powers not assigned to this Constitution nineno lililotumika kwa mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano: Ni sawa na katiba yetu kuhusu zanzibar na Tanganyika kuna mambo ambayo sio ya muungano ambayo nchi zinatekeleza.

Jaji: Neno shall kule Dubai lina context sawa na huku

SA Kalokola kwa context ya Tanzania shall ni lazima kwa upande wao sijajua

Jaji: ndio utuambie sasa

SA Kalokola: 

Mh Jaji nachotaka kusema parties are competent to contract Kwa mujibu wa sheria zao Waheshimiwa kwenye hoja hiyo, ninawajibu wa kusema kuhusu Katiba yetu, wajibu wa mahakama hii ni kutafsiri sheria zetu na DUBAI Pia mahakama yao ndio chombo cha kutafsiri katiba yao

SA Kalokola: 

Nilikuwa natarajia kwamba wenzetu kama wanataarifa kuwa mahakama ya Dubai imetamka kwamba kitendo cha DP WORLD kuingia makubaliano na sisi kimevunja sheria zao.

Na mwisho waheshimiwa; Katika shauri la TLS vs. Ministry of Foreign Affairs of International & AG, Cause 23/2014 mahakama hii ilipata nafasi ya kujadili hili.

[7/26, 16:25] Wakili Livino Ngalimitumba: 

Katika ukurasa wa 29 aya ya [1] ya Viana Convention. Kwamba kama mkataba umesainiwa….. (Quote). Mahakama inatuambia kukiwa na mgogoro kati ya wadau wa mkataba au mtu wa tatu, utatuzi unapaswa kufanyiwa katika mabaraza ya kimataifa.

Ibara ya 66 (a) ya viena convention inatoa namna ya usuluhishi wa migogoro ya mikataba ya kimataifa katika mabaraza ya kimataifa kwa usuluhishi.

SA Kalokola:

 waheshimiwa nasema mkataba wa kimataifa una International Forum za utatuzi wa migogoro na sio sheria zetu za ndani kama sheria ya mkataba sura 345. Subsequent project will be governed by our domestic law waheshimiwa kama ibara ya 21 ya IGA.

Jaji anatoa amri kwamba kwa maslahi la afya zetu, na watu kusimama muda mrefu kesi hii itaendelea kesho asubuhi saa 09:00.

Kesi inaendelea siku ya pili Tarehe 27 Julai 2023, mawakili wa serikali wataendelea na majibu yao.

Read More
MBY

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 26 NA JULAI 27 2023. SEHEMU YA KWANZA

KESI YA BANDARI  TAREHE 26TH JULY 2023

—–Majaji wanaingia  saa 09: 20—–

MAJAJI WATATU;

1. Hon. Ndunguru

2. Hon. Ismail

3. Hon. Kagomba

Wote wameinama wanaandika

—-Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.

MAWAKILI WA SERIKALI;

1. Adv. Mark Muluambo

2. Edson Mwaiyunge

3. Alice Mkulu 

4. Stanley Kalokola

5. Edwin Lwebilo

MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI;

1. Mpale Mpoki

2. Boniface MWABUKUSI 

3. Philip Mwakilima 

4. Livino Ngalimitumba

Anasimama wakili wa waleta maombi senior adv. Mpoki.

Adv. Mpoki: 

–Iwapendeze Waheshimiwa majaji tupo tayari kuendelea kwa utaratibu ufuatao. Nitatoa utangulizi na kuongelea kiini Na.2

Wakili Mwabukusi atazunguzmia issue no. 1 na 4. Msomi Livino atazungumzia issue na. 3 na Msomi mwakilima atazungumzia issue no.5

Bado anaendelea senior Mpoki.

Adv. Mpoki Naomba nianze kwamba maombi haya yameletwa na walalamikaji 4 ambao wapo mbele yenu kwa mujibu wa ibara 108(2] ya Katiba ya Tanzania. Inayoipa mahakama mamlaka ya pekee katika shauri hili.

Pia kifungu cha 2[3] Cha JALA

Vifungu hivi vinaipa mahakama kusikiliza shauri hili.

Pia kuna kiapo cha tar 26 June 2023 kilichoapwa na waombaji vile vile Originating Summons ambayo naomba ku adopt kuwa sehemu ya mwenendo

[7/26, 09:35] Wakili Livino Ngalimitumba: Katika Originating Summons waombaji wanaomba vitu vikubwa 9 ambavyo vipo ukurasa wa 5 mpaka 6 wa maombi ya waombaji

Anaendelea senior Mpoki kwamba Kwanza ni tamko kwamba kitendo cha mjibu maombi wa pili kupeleka mkataba kati ya Tanzania na Dubai uliohusu rasilimali za Tanzania bila kushirikisha wananchi na kupitishwa bungeni ilikinzana na ibara 1,8,18(d), 21[2] 27 ya katiba ya Tanzania 1977, Na kifungu kifungu 11[1][2][3] na kifungu cha 12 cha sheria ya mali asili, sheria na. 5 ya mwaka 2017.

Anaendelea wakili Mpoki kwamba; Vile vile mkataba huo unavifungu 6(2) 7[2], 23[4] kinaathiri Usalama wa nchi, uhuru wa nchi na kuhatarisha usalama wa rasilimali za nchi kwa kuwa inakinzana na ibara ya 1,8,18(d) 28 ya Katiba ya Tanzania.

Adv. Mpoki: Vile vile mkataba haupo wazi kuhusiana na muda, haina kadimio (consideration) kama ambavyo inatakiwa na kifungu cha 25 cha sheria ya mkataba, haielezi limitation ya maeneo ya uwekezaji.

Adv. Mpoki: Jambo la nne, Mkataba huo haukufuata sheria ya Manunuzi ya mwaka 2022 Vile vile kitendo cha bunge kuridhia mkataba ilikuwa kinyume na sheria. Waombaji wanaomba kwamba mahakama itoe tamko kwamba bunge lilifanya makosa kuridhia kinyume na sheria za nchi.

Anaendelea senior Mpoki kwamba; Mkataba huu vile vile haukuhusisha kikamilifu ushirikishwaji wa wananchi. Na kwamba waleta maombi Wanaomba tamko la mahakama kwamba vifungu vyote vinavyoathiri usalama wa taifa, rasilimali za nchi na uhuru wa nchi. Viondolewe.

Adv. Mpoki: Na baaada ya hapo upelekwa mkataba ambao utakuwa na manufaa kwa wananchi, upelekwe kwa Wananchi na baadae uridhiwe na Bunge kwa mujibu wa sheria. Katika kushawishi mahakama hii tutatumia

1. Katiba ya Tanzania, 1977

2. Sheria ya Manunuzi, iliyorejewa 2022

3. Kanuni za Bunge 2022

4. Sheria ya Mkataba sura 345

5. Sheria ya ufafanuzi wa sheria sura Na .1

6. Katiba ya umoja wa falme za kiarabu ya mwaka 1996

7. Viana convention 1966

8. Montevideo convention on rights and duties of state

9. Natural Wealth, sura 6 ya mwaka 2017

10. Natural Wealth, Sura na.5 ya 2017

11. Tutatumia Hukumu za mahakama za ndani na mahakama za nje mbalimbali kushawishi mahakama

11. Tutatumia maandiko ya maandishi nguli ya sheria ambayo yameandikwa kuhusiana na masuala yanayobishaniwa

12. Tutatumia taarifa rasmi za bunge (Hansard)

Adv. Mpoki: Baada ya kusema hayo naomba nianze na issue na. 1. On whether the public were notified and given reasonable time to participate

Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji, IGA ilisainiwa tar 25.10.2022. na chini ya ibara ya 25[2] wahusika walikubaliana kwamba mkataba huu upate ridhaa ya mahakama au bunge ili uwe na nguvu ya kisheria

Kwa takwa la kifungu hiki, Mlalamikiwa na 4 mnamo tar 5.june 2023 saa saba mchana alitoa taarifa kwa umma kutaka umma ufike kwa ajili ya public hearing kesho yake 6.june 2023[ masaa 24) tu. Masaa 24 tu wananchi walitakiwa kwenda ukumbi wa msekwa bungeni kutoa maoni. Tangazo hilo halikuambatana na Mkataba wa IGA hivyo wananchi waliombwa kutoa maoni kwenye kitu wasichokijua.

Adv. Mpoki: Logic ni kwamba hilo tangazo lilipaswa kuambatanishwa na mkataba wa IGA hicho hakikufanywa.

Adv. Mpoki: Mbili, Kutoa tangazo kwenye mtandao sio njia sahihi kuwafikia watu wengi kama Taifa. Na masaa 24 waheshimiwa majaji, ni muda mfupi wa wananchi kuona Tangazo, kutafuta mkataba IGA, KUsoma, kuelewa na kwenda kutoa maoni Bungeni dodoma Ukizingatia walalamikiwa walikuwa na mkabata tangu October na wao wamekaa na mkataba miezi 8 halafu wananchi wanapewa masaa, 24 tu. Sio sahihi.

Adv. Mpoki: Bahati nzuri , wakati wanajibu kiapo cha waombaji katika paragraph ya 5 na 6 cha kiapo cha Maria, mjibu maombi anakubali kweli tangazo lilitolewa tar. 5 June 2023 kwa kutumia media platforms, Hawajasema hizo media ni zipi na wanakubali kwamba hawakuweka Mkataba wa IGA na waliita watu kwenda kuangalia Mkataba. Hili ni kosa kubwa kwa wajibu maombi.

Adv. Mpoki: Katika aya ya 7 ya majibu yao wamesema watu 72 walitoa maoni yao kati ya watu milion 60 kuhusu rasilimali zao. Tunaomba mahakama ijue kwamba kutokea kwa watu 72 ni kutokana na muda mfupi waliotoa ila wangepewa miazi miwili au mitatu tungepata response kubwa sana. Kwenye majibu yao, wameonyesha waty 72 ya waliotoa maoni na majina yao. Nadhani hii haitoshi kuwa shahidi kwa kuwa hakuna kiapo cha hao watu 72. Hakuna kiapo chochote katika mahakama hii kitu ambacho ni jambo la kusemekana na sio halisi pale ambapo hakuna kiapo.

Waheshimiwa majaji Katika kesi Diana Rose Spare part ltd v commissioner General of TRA,Kesi Na.245/20/2021 katika ukurasa wa 9 Mahakama ilisema: Kama kuna nyaraka imemtaja mtu, mtu husika lazima ale kiapo kuhusu nyaraka husika. Kanuni ni kwamba; unapoandika kiapo na unamtaja mtu mwingine, yule mtu mwingine lazima atoe kaipo kinyume na hapo kiapo husika hakitakiwi kutambulika na mahakama.

Anaendelea Mpoki: Wahemshimiwa, Notice inazungumziwa Katika Kanuni 108[2][Quote as its) lengo la notice ni kusaidia katika uchambuzi wa Mkataba husika. Uchambuzi ni vitu hivi tunaongea sasa hivi, kama nafasi ingekuwa kubwa tusingekuwa hapa mahakamani. Waheshimiwa naomba tusome kesi; supreme court of UK kuhusu umuhimu wa NOTICE. REPORTED in textimile.Law report ya uingereza. Nianze kwa kusema Notice is a process ambayo anayetakiwa kutoa ushauri anapaswa kjelezwa kitachozungumzwa, apewe muda wa kutosha, aruhusiwe kushiriki na hata maoni yake yanapaswa kuonyeshwa. Waheshimiwa Mkataba huu unahusu, sea port, lake port na economic zone na inahusisha maeneo yote ya nchi na ilipaswa kuwahusisha watu wa kanda za maziwa katika hili. Na ushirikio ulikuwa muhimu kwa sababu wao ni wadau katika rasilimali zao. Na ushirikishwaji kwa wataoathirika ni sehemu ya Haki ya asili. Bila kuzingatia kanuni ya haki ya asili ni kitendo kibaya na wananchi hawakuhusishwa. Hivyo ni rai yangu kwamba wananchi hawakuhusishwa, hawakupewa muda na tunaomba mahakama iseme au itamke kwamba kitendo hiki ni kitendo batili.

Anamaliza senior Mpoki sasa anamkaribisha wakili Boniface Mwabukusi ili aendelee kuwasilisha hoja.

Sasa ni zamu ya wakili Boniface Mwabukusi.

Adv.Mwabukusi: nitawakilisha issue na.1 kwa idhini yenu naomba kuzungumza issue Na4. Na 5 kwa pamoja. Waheshimiwa majaji, nitaongozwa na sheria ya utafsiri wa sheria[Cap1 RE2019) kifungu cha 25(1][2]ambavyo kifungu cha 1 kinasema; Utangulizi katika sheria ni sehemu ya sheria na itakusudiwa kwamba ni sehemu inayochagiza kusudio na lengo la Sheria. Kifungu 2 kinasema: Jedwali katika Sheria pamoja na Notice inatengeneza sehemu ya Sheria.

Adv. Mwabukusi: 

Waheshimiwa; nikijikita katika sababu ya kwanza; naomba mahama iende kwenye Utangulizi wa Natural Wealth and Resources, Sura 5 ya 2017 katika paragraph ya 1 na 2 Paragraph ya 1: inahusu msingi mkuu wa malengo na maelekezo ya kisera katika ibara ndogo ya 1 ya sura 5 na ibara ya 9(f) ya Katiba ya Tanzania inatambua mamlaka ya umma. Na kupitia umma huo, serikali itapata nguvu na mamlaka kutoka kwa watu na huku msingi mkuu ikiwa ustawi wa watu. Na paragraph ya 2 inaeleza kwamba; sheria za kimataifa zinatambua haki yetu ya jamhuri katika permanent sovereignty ya kufaidi, kutumia maliasili yake.

Adv. Mwabukusi: 

Waheshimiwa, naomba msome ukurasa wa 4, paragraph 4 inaeleza Mamlaka na nguvu ya watu ya kuhakikisha kwamba mipango yote, makubaliano yote yanalinda maslahi ya watu na jamhuri yetu. Ukurasa huohuo, paragraph 5, inaeleza kusudio la kuweka sheria madhubuti ili kuhakikisha umiliki, udhibiti wa Rasilimali asili na kulinda ukuu wa nchi kuhusiana na mali asili zake.

Adv. Mwabukusi: 

Waheshimiwa majaji, kifungu cha 11 (1][2]cha sheria( Natural Wealth, Sura na 5) Kifungu kinasema kwa mujibu wa ibara 27(1] ya Katiba ya Tanzani, 1977 kinasema; ukuu wa nchi katika rasilimali zake utahakikisha migogoro yote ya maliasili haitapelekwa kwenye mahakama au mabaraza ya kigeni.

Adv . Mwabukusi: 

Kifungu cha 11[2] kinaeleza: kwamba migogoro inayotokana na suala la rasilimali zetu itaamuliwa na mahakama au chombo chochote kilichotebgenezwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kifungu hiki kinakataza kabisa masuala ya maliasili ya taifa letu kusikilizwa na kuamuliwa na sheria za kigeni na mahakama za kigeni.

Adv. Mwabukusi: 

Waheshimiwa majaji, wakati mkitafakari kuhusu ukuu wa nchi(Sovereignty) naomba muende kwenye jedwalli la pili la sheria. Imeweka mamlaka ya nchi kuhusu usimamizi, Uratibu na kuweka haki ya nchi kutokulazimika kupitia mkataba kufanya jambo linaloathili ukuu wa nchi(Sovereignty)

Adv. Mwabukusi: 

Sheria ya pili ni Natural Wealth, Sura Na.6 ya Mwaka 2017. Katika kifungu cha 5(1] cha sheria hii kinatamka: kwamba mipango yote, au makubaljano katika masuala ya rasilimali za nchi ndani ya siku 6 kuripotiwa katika Bunge la JMT

[7/26, 10:53] Wakili Livino Ngalimitumba: 

Waheshimiwa kifungu cha 6(2] cha sheria husika kinatamka; makubaliano yapi yatakuwa na utata. Kifungu cha 6(2)[a) kinasema; kuhusu ukuu wa nchi katika utajiri wake na rasilimali zake za nchi

[7/26, 10:55]. Kifungu cha 6(2)[e] (quote as it is)

[7/26, 10:57]. Kifungu cha 6(2)[i) quote as its

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa majaji kwa ufupi, vifungu hivi vinaeleza kwamba kama mkataba utakuwa na changamoto dhidi ya ukuu wake (Sovereignty) kama unapendelea wawekezaji wa nje na kuzipa nguvu sheria husika, maana yake mkataba huo ni tata.

Adv. Mwabukusi; 

Waheshimiwa majaji wakati mkiangalia hoja yetu katika hili, naomba muone annexture A2, ukurasa wa 5 utangulizi “J” Isomwe pamoja na ibara ya 2(1) ya Mkataba wa IGA Kwamba lengo la wahusika katika huu mkataba walitaka uwe Binding. Ukiangalia Utangulizi wa IGA, Paragraph a, b, na c zinazoonyesha kwamba; Mchakato huu ulianza tar 28 February 2022. Na climax, mwisho ilikuwa tar 25 October 2022 lakini kinyume na matakwa ya sheria inavyotaka ikapelekwa katika kikao cha 45 cha Bunge cha tar 10 June 2023. Kifungi kingine kinachohatarisha ukuu wa nchi ni ibara ya 4(2] Ambayo inatusubject taifa kama massanger.

Adv. Mwabukusi: 

Kifungu hiki kinaondoa ukuu wa nchi katika kufaidi rasilimali za nchi kama sheria zote mbili nilizotaja hapo juu na kuipa Dubai mamlaka Quote ibara 4(2). Kifungu hiki 4(2) kinainyima nchi yetu kuachana na haki ya kutafuta fursa kwingine zaidi ya Dubai hivyo kukinzana na sheria zote nilizotaja hapo juu.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa ibara ya 21 ya IGA, inakinzana na Sovereignty ya nchi yetu.

Wakili wa serikali: Mh. Judge wakili Mwabukusi alisema anadeal na issue na moja lakini anasubmit tofauti na issue zingine.

Adv. Mwabukusi: waheshimiwa majaji mimi nazungumzia process nzima ya ratification na kutaja vifungu ambavyo mahakama ivitazame kwa kina. This is my floor.

Jaji: mkataba wa IGA inavifungu ndani yake na Mwabukusi anatualika mahakama kuvitazama vifungu husika nadhani tuendelee

Adv.Mwabukusi: 

nimesema masuala ya utatuzi wa migogoro ya rasilimali za nchi kwa kutumia mahakama za ndani na sheria za ndani. Lakini kifungu cha 21 kimeondoa hayo mamlaka. Kifungu cha 23[4] cha IGA kinaondoa kabisa ukuu wa nchi [sovereignty ) katika kujiondoa au kushiriki na wengine. Hivyo kinakiuka ulinzi wa rasilimali za nchi yetu. Waheshimiwa nitajikita katika issue 4 na 5 kwa pamoja. Swalii ni je IGA ni mkataba au mazungumzo ya kawaida? Kwakile kilichojili katika kikao cha 45 cha bunge cha tar 10.06 2023, Waziri wa ujenzi na uchukuzi aliwasilisha Bungeni azimio kuhusu pendekezo la kuridhia mkataba.

Adv. Mwabukusi: 

Waheshimiwa majaji hili suala halijabishaniwa na upande wa pili katika majibu yao. Tutawasilisha kwamba mkataba huu hauna sifa za kisheria za kuwa mkataba. Nitazungumza maeneo mawili Waheshimiwa: 

1. Kifungu cha 25 cha sheria ya mkataba, Sura 345. Mkataba huu unahusu uwekezaji lakini haujaambatishwa na nyaraka yoyote au kifungu chochote kjnachoonyesha, huyu DP WORLD anawekeza kiasi gani. Hata kwenye appendix,1 ya IGA katika phase 1 ya project. Hakuna kjnachoonyeshwa anawekeza nini au kiasi gani zaidi ya kueleza kitu anachopewa. Hiki ni kinyume cha kifungu cha 25 cha sheria ya Mkaba, Sura 345. This is serious illegality juu ya uhalali wa Mkataba.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa majaji: kuhusu Capacity/ Competence to contract. Kifungu cha 11[1][2] cha sheria ya Mkataba (Quote)

Is not disqualified from contracting by any law( maneno kwa uzito)

Waheshimiwa, Ibara 123 ya Katiba ya umoja wa kiarabu (Quote) kinaeleza bayana kwamba: mshiriki wa umoja wa kiarabu atathibitisha makubaliano na nchi nyingine na makubaliano husika kama hayata kinzana na maslahi ya umoja.

Waheshimiwa majaji DP WORLD hawana capacity to contract na hakuna instrument yoyote ambayo DP World imeruhusiwa na umoja wa kiarabu kufanya makubaliano na Tanzania.

Ibara ya 1 ya Montevideo Convention inatoa sifa ili nchi uweze kutambukika kufanya makubaliano ikiwemo kuwa na uwezo wa kufanya makubaliano kama nchi. Kitu ambacho DUBAI haina hiyo capacity.

Anaendelea wakili Mwabukusi kwamba; Waheshimiwa majaji, Katika kesi ya Day care Vs. Commercial bank Tanzania Ltd ukurasa wa 10 par 2 mstari wa pili. Kunamaneno yanasema. Ili mkataba kuwa na nguvu ya kisheria: free consent of the part, competent to contract and lawful consideration. Kwakua DP WORLD sio competent by virtue of Section 2,10,11(1] of the law of contract. Tunaomba muone kwamba mkataba huu unakosa sifa za kisheria. Na kukosekana kwa issue hizo kunathibitisha mkataba huu ni batili. Its void abuinitial.

Kwa mazingira haya tunaiomba mahakama yako tukufu kuuondoa mkataba huu. Anamaliza wakili Mwabukusi.

Sasa ni zamu ya wakili Livino.

Wakili Livino Ngalimitumba: 

Adv. Livino: 

Nitajikita katika Ukuu wa Katiba ya nchi dhidi ya huu mkataba wa IGA. Waheshimiwa majaji SAMATA J, katika kitabu cha Rule of Law vs Rulers of law, kilichoandikwa na Prof shivji na majamba katika ukurasa wa 128. Kwamba, kuishi kwa mazingatio ya katiba ya nchi hakutakiwi kuchukuliwa kama utumwa bali ni wokovu. Hii inamaanjsha mtu akiwa katika utumwa anapaswa kufanya bidii kujiondoa na akiwa katika wokovu yafaa asiondolewe au kuondoka hapo.

Adv . Livino: 

Waheshimiwa majaji mkataba wa IGA umekiuka vifungu katika ibara ya 1, 8,28(1)(3) ya Katiba ya Tanzania. Kuna ikiukwaji wa moja kwa moja na ukiukwaji katika taathira ya utekelezaji wa mkataba wenyewe. Waheshimiwa majaji ibara 4[2) ya IGA Inayoeleza scope of cooperation na kutoa wajibu katika serikali ya JMT kuwa agent wa Dubai mwenyejukumu la kuifahamisha dubai kila fursa nyingine za bandari. Ili dubai iweze kuelezea utayari wake katika kuwekeza katika Tanzania. Huu sio wajibu rafiki kwani unaathiri sovereignty ya nchi yetu. Na pia inaondoa ukuu wa nchi yetu katika kutafuta wawekezaji bora zaidi ya Dubai wataoweza kufanya uwekezaji bora katika nchi. Tunaomba mahakama ione kwamba ibara husika ya IGA inavunja katiba na tunaomba mahakama itoe tamko kuwa inavunja katiba ya nchi.

Adv. Livino: 

Ibara inaelezea wajibu wa watu wote, kuilinda nchi katika hali yoyote inayoonekana inayoathiri nchi. Waheshimiwa kutoa exclusive rights kwa DP WORLD ni kuikosesha nchi yetu kujilinda na kulinda rasilimali za nchi maana hakuna hata reservation rights.

Adv. Livino: 

Ni maombi yetu kwamba mahakama ione kwamba kifungu 5(1) kinakiuka ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania na ione kwamba hiyo ni sababu ya kubatilisha mkataba wa IGA.

Waheshimiwa ibara 6(2] ya IGA (Quote as its) serikali ya Tanzania imezuiwa constructively kuingilia sehemu ya DP WORLD hata kama kutakuwa na sababu za kiusalama basi wadau wote wawili wanatakiwa kuwa na uelewa wa pamoja

Adv. Livino: 

Waheshimiwa majaji. Ibara hii inavunja ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania na kwakuwa Katiba imetoa wajibu wa chi kama nchi huru na kifungu hiki ni kuifanya nchi iingie kwenye changamoto kubwa za kiusalama. Lakini pia kifungu husika kinatweza ukuu wa nchi (Sovereignty) katika kujilinda na kulinda Rasilimali za nchi. Waheshimiwa Ibara 8(1] a,b,c ya IGA, ibara 8[2], 10[1), 23[3][4], 26,27 inakiuka ibara ya 1,8 na ibara 28 ya Katiba ya Tanzania katika misingi ifuatayo;

Adv. Mwabukusi: 

Waheshimiwa kwanza zinakusudia kuendekeza vitendo vya uvamizi kwa kutoa land rights kwa DP World Exclusively kinyume na ibara ya 28 ya katiba Tanzania. Pia inatoa mianya ya uvamizi wa misingi ya uchumi wa Tanzania kutokana na ubepari uliopo katika mianya ya uchumi. Tunaomba mahakama hii ione kwamba uandishi wa ibara 28 ya Katiba ya Tanzania inaposema wajibu wa kulinda nchi ni pamoja na kulinda mianya ya uchumi wake. Tunailika mahakama yako ione kwamba ibara ya .. ina prejudice haki ya watanzania waliopewa wajibu wa kushiriki katika masuala yanayowahusu. Sasa wananyimwa haki ya kufuatilia masuala yanayowahusu hususani Bandari na economic zone.

Adv. Livino: 

Nawaalika kwamba ibara 23(3) ya IGA imeweka sharti gumu la termination of the contract na kunyima Tanzania kufanya maamuzi ya mipango ya maendeleo kwa watu wake hivyo kupoka sovereignty ya Tanzania. Ibara ya 26 na 27 ya IGA, Zinakiuka Katiba ya 28 Tanzania kwa kuifanya nchi yetu iwe subordinate kwa Dp world hivyo kuondoa ukuu wa Katiba Yetu.

Kwa mazingira hayo tunaomba mahakama kiubatilisha mkataba huu.

Anamaliza wakili Livino sasa anaingia Bwalya Philip Mwakilima.

Sasa anasimama wakili Philip Mwakilima.

Wakili Mwakilima anatajikita katika issue na.6.

WAKILI MWAKILIMA;

Waheshimiwa majaji, kifungu cha 64 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma kinaweka sharti wakati wa kutoa Zabuni (tender), takwa la lazima kwamba Tenda yoyote inayotolewa kwa ushindani. Sheria imetumia neno ‘Shall.’

Lengo lake ni kupata the highest evaluated profit. Pia inataka kupata mzabuni (capable), pia sababu nyingine ni kuleta usawa kwenye soko la uwekezaji. Takwa la lazima kwamba Tenda yoyote inayotolewa kwa ushindani. Sheria imetumia neno ‘Shall.’ Lengo lake ni kupata the highest evaluated profit. Pia inataka kupata mzabuni (capable), pia sababu nyingine ni kuleta usawa kwenye soko la uwekezaji.

Adv. Mwakilima: 

Mkataba wa IGA kwenye Preamble imesema kwamba DPW walikabidhiwa Kazi za Uwekezaji bila kuonekana walishindanishwa na nani. Ibara ya 8 ya IGA inaeleza kwamba DPW amepewa kuendesha Bandari bila kushindana na wawekezaji wengine. Lakini tu kwenye Preamble para ya pili IGA inaeleza kwamba kulikuwa na mazungumzo ya watu wawili huko Dubai wakati wa ziara ya Rais Samia.

Adv. Mwakilima: 

Waheshimiwa majaji, kwenye Preamble kuna maneno mengi ya kuipamba DPW kwamba ni kampuni bora. Lakini haijasema alishindanishwa na nani ili kumpata DPW kuwa bora zaidi ya wengine. Uandishi huo wa Preamble inaonyesha kama walitangaza Tenda Dunia nzima, hata hivyo hawajasema ni makampuni mangapi yaliomba Tenda hiyo.

Adv. Mwakilima: 

Waheshimiwa Majaji, malengo ya kutangaza Tenda yamewekwa na sheria lakini DPW walipewa Tenda bila kufuatwa matakwa ya kisheria. Na Bunge letu chini ya Ibara ya 63(3)(e) walibariki. Mchakato huu kimsingi si tu ulikiuka Sheria ya Manunuzi, bali pia hata umevunja Katiba ya Tanzania. Kifungu 64(2) ya Sheria ya Manunuzi, inaeleza juu ya mambo ya uharaka/dharura yanayokubaliwa. Hakuna kiapo cha Wajibu Maombi kinachosema kwamba walitoa Tenda kwa DPW kwa sababu ya mambo ya dharura.

Adv. Mwakilima: 

Waheshimiwa majaji, Kifungu cha 3 cha Sheria ya Manunuzi ambacho ni Interpretation Provision inaeleza tafsiri ya neno Tenda. Mkataba huu wa DPW ni Tenda for life. Anamaliza wakili Mwakilima kwa kusema anaomba mahakama kubadilisha mkataba huu kwa hoja alizozitoa. Na kwamba bunge lilidhia mapungufu ya mkataba huu na sasa tegemeo lililobaki ni mahakama pekee.

Anamaliza kuwasilisha hoja wakili Mwakilima. Na huo ni mwisho wa hoja za waleta maombi au wananchi wanaopinga mkataba wa bandari.

Jaji anatoa amri kwamba sasa ni saa saba kamili mchana, mahakama inaenda break na itaendelea baada saa 14: 30 mchana.

Baada ya kuendelea itakuwa ni zamu ya mawakili wa serikali kujibu hoja. fuatilia sehemu ya pili

Read More
SAMIA

NUKUU MUHIMU KUTOKA KWENYE HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU TAREHE 26 JULAI, 2023 JNICC – DAR ES SALAAM.

 TAHIMINI YA KINA YA HOTUBA HII INAONYESHA UMUHIMU WAKE KATIKA KUELEZEA CHANGAMOTO NA FURSA ZINAZOIKABILI AFRIKA NA JINSI YA KUTUMIA RASILIMALI WATU KULETA MAENDELEO ENDELEVU. HOTUBA HII INAONYESHA UFAHAMU MZURI WA HALI HALISI YA BARA LA AFRIKA NA INATOA MAPENDEKEZO YANAYOFAA KWA KUBORESHA HALI YA ELIMU, AFYA, NA MAFUNZO ILI KULETA MABADILIKO CHANYA NA USTAWI WA JAMII.

Muhimu Zaidi:

  1. Ushirikiano: Hotuba hii inasisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, asasi za kiraia, na sekta binafsi katika kuleta maendeleo ya rasilimali watu. Ushirikiano huu unahitajika kwa ajili ya kuleta uwekezaji unaohitajika na kujenga mazingira wezeshi ya kukua na kuendelea kwa rasilimali watu.
  1. Kuzingatia Demografia ya Vijana: Hotuba hii inaonyesha umuhimu wa kuutumia vizuri uwezo wa idadi kubwa ya vijana kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii. Inatoa wito wa kuchangamkia fursa ya “Demographic Dividend” kwa kuwekeza katika vijana na kuwapa ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.
  1. Elimu na Mafunzo: Hotuba hii inaangazia umuhimu wa kuboresha elimu na mafunzo katika ngazi zote. Inasisitiza haja ya kujikita katika mabadiliko ya mitaala, ufundishaji, na matumizi ya teknolojia katika kutoa elimu ili kuandaa vijana kwa soko la ajira lenye ushindani mkubwa.
  1. Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango: Hotuba hii inahimiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu ya uzazi na mifumo saidizi kwa vijana. Kupunguza mimba za mapema kunaboresha maisha ya vijana na watoto wanaozaliwa, na kuwezesha familia kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya ya uzazi.
  1. Maono ya Maendeleo ya Afrika: Hotuba hii inakazia malengo ya maendeleo ya Afrika kama vile ukuaji jumuishi wa uchumi, utangamano kisiasa, utawala bora, na kuweka msisitizo katika maendeleo ya watu kwa kutumia vipaji vyao.

Tahimini ya kina inaonyesha kuwa hotuba hii ni mwongozo mzuri kwa viongozi na wadau wa maendeleo kuhusu umuhimu wa uwekezaji katika rasilimali watu na njia za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu barani Afrika. Inatoa ufahamu wa kina wa changamoto na fursa, na inatoa mapendekezo yanayofaa kwa kuimarisha sekta ya elimu, afya, na mafunzo ili kuchochea maendeleo chanya na ustawi wa bara la Afrika. Hotuba hii inasisitiza wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha rasilimali watu ya Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo endelevu na mafanikio ya bara hili.

Read More
CHI

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KWA VIONGOZI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 25 JULAI, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu wakati wa hafla ya Chakula cha jioni, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na wageni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova, Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina pamoja na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Biowakati wakiangalia vikundi mbalimbali vikitumbuiza katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Wonie Bio wakati wa hafla ya chakula cha jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova kabla ya hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Wakuu wa nchi mbalimbali pamoja na Viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi hao wanaoshiriki Mkutano wa Rasilimali watu Jijini Dar es Salaam Julai 25, 2023.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu jijini Dar es Salaam .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe tarehe 25 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali wakielekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi.

Read More