NI LIPI LA KUJIFUNZA JUU YA KUMBUKUMBU YA MUUNDO WA KATIBA YETU NA HISTO…
To leave a comment, click the button below to sign in with Google.
To leave a comment, click the button below to sign in with Google.

Tuanze kiduchu hii
[13:11, 19/05/2023] T:Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ambao umeshirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa nchini Tanzania kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba huweza kuchangia mabadiliko makubwa ya kitaifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya Uchumi, Siasa na jamii kwa ujumla.
Mchakato unapokwama pasipo muafaka wa kitaifa huweza kuzalisha mazingira ya kufifia kabisa kwa umoja wa kitaifa na hatimaye kudumaza maendeleo ya nchi.
Na hapa sasa ndio sifa zangu zinamwangukia Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan,anayaona haya kwa mapana sana..
Swala la Maridhiano na kuanza upya ni Maono ya juu mno ya Dr Samia binafsi…
Tanzania iliamua kuanza uandishi wa katiba mpya kutokana na kua katiba zote tano zilizopita tangu katiba ya uhuru ya mwaka 1961 mpaka katiba ya kudumu ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake yote 14 vimekuwa vikilalamikiwa kwa kutoshirikisha wananchi kikamilifu.
Hivyo ukaundwa mfumo ambao ungeruhusu ushiriki wa wananchi katika kupata katiba bora.
Pamoja na kukwama kwa kwa mchakato wa mabadiliko ya katiba mnamo mwezi Aprili 2015 ambao ulianzishwa mnamo mwaka 2011,
Ukifuatilia hotuba nyingi za Dr Samia ambae alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la katiba wakati huo anataka wananchi waelewe wafafanuliwe watambue mambo mawili tu
MOJA
Sababu kuu za kukwama kwa mchakato wa katiba;
PILI
Mapendekezo ya njia nzuri za kuufufua na kuendeleza mchakato wa Katiba ambao unabeba maoni ya wananchi.
Na hata ukiyasoma matakwa ya wanaharakati na asasi za kiraia utakuta wanaunga mkono hili hiki ndio wadau wengi hapa wamesisitiza tukianishe…

Tarahe 31 Disemba 2010 aliyekuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza nia ya Serikali ya kuanzisha mchakato wa Katiba. Hatimaye mwaka 2011 Mchakato huo ulianza kwa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 na baadaye kufuatiwa na Sheria nyingine ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitamka kuanzishwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo iliratibu mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya katiba ambayo pia ilihaririwa na Mabaraza ya Katiba na hatimaye kupatikana kwa Rasimu ya Pili ya Katiba. Rasimu hiyo
iliwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba (BMK) ambalo kwa kiasi kikubwa lilitawaliwa na wanasiasa wakitokana na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar.
Mchakato wa Bunge Maalum kujadili na kutunga Katiba Inayopendekezwa kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na mivutano ya kisiasa na kusababisha baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujitoa kwenye majadiliano na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Kujitoa kwa wajumbe
hawa kulisababisha kutungwa kwa Katiba Inayopendekezwa iliokosa muafaka na kuidhinishwa Mwezi Oktoba 2014.
Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11/2013, Tume ya Uchaguzi ilipanga tarehe 30 Aprili 2015 kuwa ndiyo siku ya wananchi kupiga kura yamaoni. Zoezi la kura ya maoni lilikwama kufanyika kwa sababu mbalimbali….KONGOLE SANA DR JAKAYA KIKWETE
[13:27, 19/05/2023] T:SABABU ZA KUKWAMA KWA MCHAKATO WA KATIBA ZILITAJWA TAJWA MARA KADHAA
Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni na Maelekezo ya Tume ya Uchaguzi (NEC), zoezi la kura ya maoni lilipangwa kufanyika tarehe 30 Aprili 2015. Lakini kutokana na sababu mbalimbali zoezi la kupiga kura ya maoni lilishindikana na kuahirishwa kwa kipindi kisichofahamika.
Sababu mbalimbali zilizopelekea kuahirishwa kwa zoezi la upigaji wa kura yamaoni juu ya Katiba Inayopendekezwa ni pamoja na;
i. Kutengwa kwa muda finyu na usio halisi wa kisheria kutekeleza zoezi la Upigaji kura ya Maoni. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura yaMaoni, Rais aliiagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa kura ya maoni kufanyika tarehe 30 Aprili 2015, lakini wakati huo huo Tume ya Uchaguzi ilikua ikiendesha programu ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa njia ya kielektroniki ili kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kinyume na ilivyokua imepangwa, zoezi la kuboresha daftari lilichelewa kumalizika kwa muda muafaka, hivyo kupelekea muda kuwa finyu na hatimaye tarehe za kura ya maoni zilizopangwa kisheria kupitwa na wakati.
ii. Sababu nyingine ni kutokuwepo kwa muafaka wa kikatiba ndani ya Bunge Maalum la Katiba na hivyo kupelekea baadhi ya wajumbe wa BMK hususan waliotokana na Vyama vya Upinzani – Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kijitoa na kutoshiriki katika kuipitisha
Katiba Inayopendekezwa na kuchangia kujitokeza kwa mgawanyiko mkubwa katika jamii na kuathiri mwenendo mzima wa mchakato wa katiba.
Kwa kiasi kikubwa mpasuko wa BMK ulichangiwa na uwepo wa idadi kubwa ya wanasiasa ambao waliteuliwa kuwa wajumbe huku wakiwa bado ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar.
Lakini nakumbuka wakati ule kamati iliyokuwa ikiongozwa na Dr Khoti Kamanga ilichambua kwa kina kukwama kwa mchakato mzima..Twendeleeeeee

“Chimbuko la mamlaka ya dola ni wananchi wenyewe. Serikali hupata uhalali wake kutokana na wananchi kupitia Katiba. Vilevile kushiriki kwa wananchi katika maamuzi kuhusu mambo yanayogusa maslahi yao ni msingi mkuu wa utawala wa ki-demokrasia. Kwa misingi hiyo,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko katika mchakato wa kupata Katiba mpya. Kwa kuwa Katiba ni uamuzi wa wananchi jinsi wanavyotaka kuishi, kujiongoza na kuendesha nchi yao,
mabadiliko ya Katiba yanawapatia Watanzania fursa kubwa ya kuzaliwa upya kikatiba, kisheria, kisiasa, kiuchumi na kijamii”.-@Pasta Martin akihojiwa rfikiswahili 2011 hayo ya mbele uliyoyasema wakati ule utaya ongezea mwenyewe…Media haifichagi kitu
[13:52, 19/05/2023] A: Kutoka Maktaba! 😀💪🏽 [13:52, 19/05/2023] T: Na maneno haya yalitumika katika utangulizi wa mwongozo wa ELIMU KUHUSU KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANOWA TANZANIA YA MWAKA 1977
(KWA LUGHA NYEPESI) uliotolewa na TUME YA MABADILIKO YA KATIBA wakati huo Kudos @Pasta Martin
[13:53, 19/05/2023] K: Teknolojia ni ya kuheshimu
SHERIA ZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA
Kuna sheria kuu mbili zilizoongoza mchakato wa mabadiliko ya katiba ambazo ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83 ya mwaka 2011 pamoja na Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11 ya mwaka 2013.
Sheria ya Mabadiliko ya katiba ilitoa muongozo wa kuundwa na mamlaka ya vyombo vyote vya kuratibu mchakato wa katiba, vikiwemo; Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba.
Sharia hizi pia zimeainisha namna ya ushiriki wa wananchi katika hatua zote za mchakato wa katiba, utaratibu wa wananchi kuipigia kura ya Maoni Katiba Inayopendekezwa pamoja na vyombo vitakavyosimamia haswa Tume ya Taifa Uchaguzi. Kwa kiasi kikubwa hatua zote za mchakato zinazotamkwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba zimekwisha kamilika. Kwa upande wa Sheria ya Kura Maoni, hatua pekee ambayo haijakamilika mpaka sasa ni kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa kupitia kura ya maoni na kuanza kutumika rasmi.
Wakati wa kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni, ilizaniwa kuwa mchakato wa katiba utakamilika ndani ya muda uliokuwa umekusudiwa kisheria.
Kwa bahati mbaya muda ulikwisha kabla ya Katiba Inayopendekezwa kupigiwa kura ya maoni kutokana na sababu mbalimbali zilizoanishwa awali, ikiwemo uwepo wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa njia ya kielektroniki kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kutokana na kupita kwa muda kisheria, maboresho ya Sheria ya Kura ya Maoni hayaepukiki ili kuruhusu mwendelezo mzima wa mchakato wa kupata katiba mpya. Ref. MCHAKATO WA KATIBA MPYA NINI MWISHO WAKE? Lhrc -2018


MJADALA UNAENDELEA

Julai 2, 1992, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya kuruhusu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
tumepiga hatua, lakini, mpaka hii leo, bado upinzani kwa wengine unatafsiriwa kama ni uadui, na wakati mwingine ni uhaini.
Ni busara kutambua, kuwa wakati umebadilika. Mtanzania wa mwaka 1977 si Mtanzania wa mwaka 2023. Ni Zaidi ya miaka 40 atiii..
Hoja hii ya Katiba si kama inzi anayetua na kuruka. Hoja ya Katiba kwa sasa inaongozwa na kundi kubwa la vijana wanaotaka mabadiliko.
Hawa si inzi wanaotua na kuruka, ni siafu wanaokuja kwa kuongezeka idadi yao. Na hili Rais wa sasa ameliona hili na ndio maana ameridhia tuanze tu..
Na harakati za Watanzania kutaka marekebisho ya Katiba zina muda mrefu. Hizi si harakati mpya. Si harakati za chama au kikundi kidogo cha ’wapinzani’ wasioitakia mema nchi hii naamini hapana..
Siku zote, yamekuwa ni madai ya msingi ya Watanzania, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, rangi na makabila.
Kama ni shauri mahakamani, basi, lilishafunguliwa zamani. Kinachofanyika sasa ni mwendelezo tu wa shauri lenyewe
Si wengi, miongoni mwetu vijana wa sasa, wenye kumbukumbu ya ukweli huu ama kuyasoma na kuyatambua haya..
Ninachoomba katika forum hii ya KATIBA YA WATU, baada ya kupitia Nondo zinazoshuka hapa hebu kwa uchache tukumbusheni sisi wengine nini kilitokea miaka ya tisini, ilikuwaje hadi Julai 2, 1992 bunge likaridhia? Nani waliendesha harakati hizi za kudai mabadiliko? Na walipata kashikashi na upinzani wa namna gani?
[10:22, 17/05/2023] T: Nasoma Neno kwa neno script safi hii ngoja niifanyie kazi….Wadau wote wako hapa Duuuh! hoja imejengwa hii haya twende sawa 👍🏼MAJIBU…
[15:04, 17/05/2023] T: Tayari mwaka 1991 vuguvugu la kudai vyama vingi na Katiba mpya lilikwishakuanza.Wakati huo madai makubwa yalikuwa mawili;
Vyama vingi na Marekebisho ya Katiba.
Wapo hapa mnaokumbuka ’ KAMAKA’- Kamati ya Marekebisho ya Katiba iliyoundwa na wanaharakati.
Ikumbukwe, kuwa hayo yalikuwa ni madai ya Watanzania ndani ya mfumo wa chama kimoja.
Chifu Abdallah Fundikira aliongoza Kamati iliyoundwa, si na Serikali, bali wanaharakati, kuratibu mchakato wa kudai vyama vingi na Katiba mpya.
Hata wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kama Rais, aliweka ‘ mkwara’, kuwa madai hayo yasiendeshwe na watu au makundi ya watu bila kibali cha Serikali. Presha ya madai ilipoongezeka, wapo wazee wanakumbuka jinsi Mzee Ali Hassan Mwinyi aliweza kusoma alama za nyakati.
Mzee Mwinyi Alizungumza pale Chuo Kikuu Mlimani na kuweka bayana dhamira ya Serikali ya kuunda ‘ Tume ya Nyalali’ . Tume hiyo ilizunguka nchi nzima kuwauliza Watanzania kama wanataka kuendelea na Chama kimoja au Vyama vingi.
Chifu Fundikira alipata kutamka; kuwa huko ni kupoteza muda na fedha za wananchi. Itakumbukwa pia, Mabere Marando alikuwa Katibu wa Kamati ile ya wanaharakati ya kuratibu mchakato wa madai ya kuwapo na vyama vingi na marekebisho ya Katiba.

……………… Twendelee Sasa
[10:30, 17/05/2023] A: Kwa katiba yetu ya sasa wabunge wanawajibika kwa nani?Nimejaribu kusoma waliotangulia hapo kuangalia mgawanyo wa majukumu katika mihimili yetu hii mitatu.
Ni kweli chanya ni chache sana ukilinganisha na hasi. Mimi nitajikita kujaribu kujua kwa katiba yetu ya sasa hawa wabunge wanawajibika kwa nani? Je, mwezi kwa mwezi hawa watu wanatoa ripoti ya shughuli zao kwa nani? Je boss wa wabunge ni nani?
Maana kwa sasa hapa nchini ikiwa mbunge wewe tayari ni tajiri mkubwa na hakuna wa kukugusa. Na isitoshe kwa sasa ubunge imekuwa ndiyo mafanikio na siyo utumishi tena. Watu wananunua magari ya bei za juu na vitu vingine vya bei kubwa sana. Ubunge kwa sasa imekuwa ni kitega uchumi na siyo utumishi wa wananchi tena.
Na kwasababu wananchi hali zao ni duni wabunge wamekuwa Miungu watu kwenye majimbo yao. Mbunge anaweza kupita na kugawa chumvi ili kuwapoza wananchi. Na baada ya miaka mitano atapota tena kuomba kura. Hakuna wa kumpima hakuna ripoti yoyote ya alichokifanya.
Na kwa sababu ya vyama vingi wabunge sasa hawaondolewi kuhofia kushindwa kwenye uchaguzi.
Kwenye katiba hii napendekeza pawepo na check and balance kwenye bunge.
Pawepo na aina mbili ya Assembly
1. Lower Assembly
2. Upper Assembly
[10:33, 17/05/2023] A: Lower AssemblyHawa wawe ni hawa wabunge wanaochagulia kwenye majimbo na hawa ndio wanaowakilisha wananchi moja kwa moja. Hawa ni mdomo wa wananchi. Huku ndiko watakako toka mawaziri. Lakini mienendo yao itakuwa monitored na Upper Assembly
[10:37, 17/05/2023] A: Upper AssemblyHawa watapatikana kutokana na utaalam wa aina tofauti tofauti. Watakuwepo wawakilishi wa tasnia hizo na kutoka katika kundi hili tutapata makatibu wakuu wa wizara.
Makatibu watakuwa watendaji wakuu wa Wizara lakini mawaziri watakuwa viongozi wa wizara.
Hiyo itafanya mawaziri wawe wakuu kwenye wizara lakini Bunge la Lower Assembly litakuwa monitored na Upper Assembly
Tukitaka kuweka check and balance ya uhakika. Expenses haziepukiki.
Hata ni mawazo yangu
[10:40, 17/05/2023] +255 67: Samahani: Umelielewa swali langu? [10:42, 17/05/2023] T: fafanua swali ueleweke zaidi wadau watalijibu..lakini Msajili huteuliwa na Rais [10:50, 17/05/2023] A. Na ninavyoona upande wa Mahakama hakuna changamoto nyingi. Lakini huku kwenye Bunge na Serikali naweza kuliita hili bunge la katiba ya sasa ni Bunge la Serikali. Siyo bunge la wananchi.Mbunge anachaguliwa baada ya kuchaguliwa haonekani kwenye jimbo lake. Kila siku tunapishana na wabunge wote huku Dar.
Kilio changu kikubwa kabisa ni kuhusu hawa wabunge. Katiba ya Watu lazima ilete solution katika hili.
Ikiwezekana Mahakama iwe na meno ya kung’ata hawa wabunge.
[10:55, 17/05/2023] +255 : Sasa ulikuwa unazunguka nini? Nilitaka tu kujua anavyopatikana huyo msajili! Kumbe anateuliwa na Rais kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi? Yaani Mwenyekiti wa Chama cha Siasa ndiye anayemteua Msajili wa Vyama vya Siasa? Na Mgombea Urais ndiye anayemteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi? Sina maswali ya ziada kwa leo.
Vile vile usisahau kupitia malalamiko ya uchaguzi kwenye baadhi ya nchi kama Marekani zenye ‘katiba bora’. Mwisho unaweza kuangalia uapishwaji wa Mfalme hapo Uingereza na mapokeo yake
[12:01, 17/05/2023] K: Natofautiana na wewe kwa asilimia kubwa ; umekiri kuwa Wabunge uwajibikaji wao una maswali (**hili ni la kujadili lirekebishwe )Pia umependekeza mabadiliko ya mfumo wa Bunge (**sio vibaya tu kujadili hili pia )
Hoja yako ya pili imeambatana na kauli za vijembe juu ya ukwasi wa wabunge kuonyesha namna “unavyoumizwa “ na matumizi yao.
Ila pia umependekeza muundo ambao utaathiri “separation of powers” kwa kuleta mkanganyo wa Katibu mkuu kuwa bosi wa waziri kwenye upper assembly lakini wakiwa wizarani bosi ni Waziri anaye tokana na lower assembly nadhani unaona mkanganyiko huo.
Umehitimisha pia kwa kusisitiza kuwa gharama haziepukiki katika uongozi wa nchi ( ingawa nadhani Unamaanisha ilimradi wabunge waishi kimaskini )
Tukitaka Tanzania iliyoendelea Kiuchumi haya mawazo lazima yachakatwe kwa umakini
Tufikiri miaka 200 baadaye ambapo kizazi chetu cha tano ndio kitafaidi
[12:28, 17/05/2023] +255 76: Kwa hoja hii kumbe shida ni watu wanaochaguliwa na sio Bunge [12:53, 17/05/2023] A: Katika nchi nyingi zilizofanikiwa duniani zinatumia mfumo wa Bicameral legislature than Unicameral legislatureNitaeleza zaidi kuhusu mambo haya mawili. Lakini kwa sasa ngoja nilitolee ufafanuzi suala ambalo umeliiya ni vijembe
Ni kweli kabisa mbunge ni mtumishi wa umma hatakiwi kuonesha kiburi na kuvimba. Na pia sijasema wabunge wawe masikini bali nimesema kuwa ubunge kwa sasa imekuwa kama kitenge uchumi na sio utumishi.
Sasa nakuja kuongelea wazo langu la kuhusu Bicameral legislature
Kwa sasa hapa Tanzania tupo na bunge la aina moja tu kwamba hakuna anayewamulika hawa wabunge wanajiongoza wao wenyewe tu. Lakini tukiwa na mfumo wa Bicameral legislature tunakuwa na mmoja anamsimamia mwingine kwa namna nyingine.
[12:58, 17/05/2023] D: Hivi kuna mtu anaijua Katiba na Mfumo wa Bunge la China? [13:07, 17/05/2023] A: Kwa kiasi kidogo nimejaribu kufuatilia maandiko kadha wa kadha kuhusu bunge la china.Bunge la china linaitwa National People’s Congress
Hawa huchaguliwa kisha huingia kwenye congress na hawalipwi maana ni kazi ya utumishi. Mwaka 2018 lilikuwa na watu 2,980.
Huwa wanakutana mara in full mara moja kwa mwaka kwa muda wa wiki mbili. Lakini wamekasimu madaraka yao kwenye Standing Committee of the National People’s Congress
Hawa wapo kama watu 170 hivi.
Mfumo wa china ni unicameral legislature hii ni kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kuwa na Chama kimoja

Sisi bado tuna hungovers za mfumo wa chama kushika hatamu, ambapo Rais (the executive branch) hutakiwa kuwa overpowering ya mifumo mingine, albeilt implicitly. And it is by design and deliberate ili kumpa Mwkt wa chama dola kubaki supreme, indeed.
Huko tunakotoka mpaka hapa tulipo, hii separation of power ilifanywa kinadharia zaidi kuridhisha uwepo wa serikali inayoeleweka katika anga za kimataifa, but in reality, tuna mfumo wa kijanja sana ambao unampa Rais na Serikali, too much power to always arm-twist the other two branches of govt to comply with whatever the executive branch desires.
Yes, kwa Tanzania, checks and balances is a mere gimmick to fool the unlearned minds but it’s rarely practised in a real sense of the word. Bunge halina chombo cha kuli regulate linapokuwa dhaifu na kupitisha mambo ya hovyo.
Bunge letu ni extention of the executive branch zaidi kuliko kuwa a regislative assemby inayowakilisha wananchi kutunga sheria za kujiongeza wenyewe kama wenye nchi.
Bunge letu linaheshimu, kutii, a kuopa zaidi Rais na Serikali yake kuliko wananchi waliowachagua.
And you know why? Because our MPs aree too politically minded. Always thinking and calculating about the next election!
Wanamwogopa n kumsifia Rais muda wote kwa sababu Rais ndiyo pia Mwkt wa chama kinachowapa nafasi wabunge wote nafasi kugombea na kupata hizo nafasi. Usipo mwogopa na kumsifia Rais bungeni na popote unapoenda kama mbunge unajiweka kwenye hatari ya kuwa booted out kwenye teuzi za baadae.
All this goes back to mfumo uliowekwa kijanja tangu mwanzo; wa kubakiza Rais na Serikali yenye nguvu mno juu ya branches nyingine za kiutawala.
With this approach, you can forget good governance, and you can definately forget maendeleo ya nchi na watu wake for the next 200 years!
Na kuhusu tofauti ya mishahara ya wabunge na Mawaziri kutosogeleana na ya watumishi wengine wa chini, tatizo ni lile lile. Nani atam regulate nani??
Fikiria Bunge hujipangia mishahara yake na kumtega Rais apitishe. Akiwagomea na wao wanamsubiri akiwapelekea mapendekezo yake wamshughulikie!
Hakuna chombo cha tatu cha kucheck na kubalance off hii power struggle kwenye mambo yenye adverse consequences kwa nchi.
I mean, it’s just a mess.
Live Long Tanzania. God bless the URT🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Mimi sitaki niongelee sana kuhusu vyama vya siasa. Maana vyama vya siasa vilianza kwenye karne ya 17 huko uingereza na vikasambaa sehemu mbalimbali karne ya 18 baada vikaimarika kwenye karne ya 19. Lakini dunia ilikuwepo kabla ya hapo na watu walikuwa wakiongozwa na Ideology za kidini.
Lazima turudi kwenye drawing board tujiulize je, ni nini lengo letu hasa kama nchi kuwa na vyama vingi?
[14:17, 17/05/2023] A: Tangu 1992 Tumepiga hatua zipi? Je, ni muhimu tuendelee na mfumo huu wa vyama vingi? Je, hatuwezi tukaenda na mfumo wa China kisha tukauboresha? Kwamba tunakuwa na chama kimoja lakini ndani ya chama hicho kukawa na namna ya watu kushiriki na kutoa maoni yao? [14:17, 17/05/2023] P: Si umesema vyama tuviache? Sasa tena mbona unauliza kuhusu vyama?🤣🤣🤣🤣🤷🏾♂️🤷🏾♂️Mfumo wa chama komoja au vyama vingi tunaweka kwenye National vision yaani kiwepo chama kisiwepo chama lazima vision itekelezwe.
Kwahiyo kwangu tukiwa na Chama kimoja hakuna shida as long as National Vision ipo vizuri na Check and Balance imekaa vizuri.
National Vision inatengeneza national Ideology. Yaani Taifa tunakuwa na imani yetu na kila mmoja anajua wapi tunaenda.
So kuhusu vyama hata kama tukiamua tuwe na chama kimoja na ndani ya chama hicho wanasiasa wanapambana na kuonesha namna gani ya kuweza kufikia National Vision.
[14:29, 17/05/2023] A: Mimi huwa nawaangalia wachina kwenye kizazi chetu hiki wameweza kuonesha kuwa maendeleo hayatokani na vyama vingi bali ni National Foundations and National Pillars then vyama vingi vya siasa ni kama mapambo ndani ya nyumba yanaoonwa na na watu wa nje kupitia dirisha dogo la FDI, Loans and donations [14:38, 17/05/2023] K: Maono …..maono maono!Katika Kitabu cha Kale nimemsoma Mfalme Suleiman Alisema “pasipo MaONO watu(a people) huangamia…
Wakati tunaelekea kutengeneza namna ya kuiweka Katiba yetu vizuri ….tuainishe MAONO ya TAIFA letu…kwa kipaumbele!
[14:39, 17/05/2023] P: Chinese? Tuna aspire kuiga China kwa mara nyingine baada ya kuwaiga mara baada ya uhuru na matokeo ndio haya?OK, kama huko ndio unataka twende, basi I reserve my comments in this discussion mpaka tutakapopata tunachotaka kuwa.🙏🏽
[14:45, 17/05/2023] T: Kuhusu mfumo wa Katiba wa China, ina Katiba ambayo ilitungwa mwaka 1982 na kufanyiwa marekebisho kadhaa tangu wakati huo. Ina mihimili mitatu ya Serikali: Rais, Waziri Mkuu, na Bunge la Watu. Rais wa China ni Mkuu wa Nchi na Mkuu wa Majeshi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Watu, anachaguliwa na Baraza la Kitaifa la Watu wa Congress ya Watu. Waziri Mkuu wa China ni Mkuu wa Serikali na mtendaji mkuu wa Baraza la Serikali la Watu. Bunge la Watu wa China, ambalo linajulikana kama Congress ya Watu, linajumuisha wajumbe kutoka kwa majimbo yote ya China, ambao huchaguliwa na raia wa China…Sijajua lengo la swali hili lakini sawa tunapaswa kujifunza kwa wengine naomba mtupitishe maeneo ambayo ni mapungufu yetu na tunatokaje huko tuendako…
Vyama vya siasa ni kuruhusu mawazo tofauti tofauti kupitia siasa. Nimejaribu kuelezea kuwa vyama vya siasa vilizna karne ya 17 huko uingereza lakini kabla ya hapo dini ndizo zilikuwa zikishughulika na maoni na wafuasi. Na mpaka leo ukiangalia dini bado zinanguvu sana.
Nikasema kwanini sasa tusiende kwenye drwing board ili tujue tangu 1992 pale vyama vingi vya siasa kurudishwa miaka 31 imepita tunaweza kujitafakari je, kuwa na vyama vingi ni nini tumefaidika?
Nikasema wachina wamewezaje maana wapo na chama kimoja na uchumi wao kwa sasa ni mkubwa mno. Ukiongelea Technology, Infrastructure nk, wachina wamepiga hatua sana.
Nikapendekeza kuwa lazima kwenye katiba yetu ya sasa ielekeze National Vision than kuelezea kuwa nchi yetu ni ya vyama vingi.
Na hiyo National Vision itazaa National Ideology so viwepo vyama vingi au visiwepo As long as direction inaeleweka.
Kwenye katiba ya sasa imesema nchi yetu ni ya Kijamaa so huo ujamaa uliosemwa kwenye katiba watu wanaujua?
Natumaini nimeeleza vizuri…..
……………….
[15:10, 17/05/2023] P: Nadhani tunatumia uwepo wa vyama vingi as distraction to the real problem!Tukitaka ku assess impact ya ama kuwepo na vyama vingi au kibaki kimoja, tusianzie mwaka 1992. Tuanzie 1961 mpaka 1992 kabla ya vyama vingi, tulifanya nin? Tulikuwa chini ya chama kimoja. Serikali toka chama kimoja. Na tulikuwa chini ya ujamaa proper. Je, kuna cha tofauti tulicho achieve wakati ule ambacho tunatamani to turn the clock back?
Kwa maoni yangu, vyama vingi Tanzania hata si vya ujadili kwa sababu kwa Katiba hii na muundo wa utawala uliopo, hawana impact popote zaidi ya kwenye uchaguzi. Kuna vyama hawajawahi kuunda serikali, na hawajawahi kupiitisha sheria au sera yoyote yenye ku affaect Taifa. Vitu vyote tangu uhuru, vimefanywa na chama kimoja au viongozi wanaotoka chama kile kile. So kama tunataka kutafuta tatizo tuliangalie kwa watu au mfumo uliodumu muda wote huu, ambao matokeo yake tunayajua.
Lakini huwezi kuniambia unataka checks and balances lakini kwa kutaka kuiga Commuinist China. Hapo tutalazimika ku drop vitu vingi sana kwenye hii Katiba na sheria zetu.
Lazima tufungulie kiwango fulani cha ukatili, secrecy, brutality, na complete disregard of human rights.
Kama tunataka kurudi huko mimi simooo…🙆🏾♂️
Kisha ndio

MJADALA UNAENDELEA……
[06:59, 13/05/2023] A: Nimejaribu kufatilia kwa kina mjadala bado nimeona ipo haja kubwa mno wanachi kupewa elimu ili kuielewa kwa upana katiba tuliyonayo kuelekea ktk mpya kimsingi wananchi hawana uelewa mzuri wa katiba iliyopo kwa mantiki hiyo kutakuwa na ugumu wao kuchangia ktk upatikanaji wa katiba mpya ikiwa ya zamani hawaielewi [07:35, 13/05/2023] +255 783 157: Sisi tunataka katiba ile ya warioba. Anania njema kuliko ile rasimu ya Bunge iliyojaa maslahi ya wanasiasa. [07:41, 13/05/2023] A: ktk kupata kuna michakato ambayo ipo kisheria ktk kuchakata kuanzia ukusanyaji wa maoni hadi bunge la katiba,ndipo nikasema ipo haja ya wanachi kupewa elimu ili kuielewa katiba hii tulioonayo ili waweze kutoa maoni kwa ufasaha baada ya kuona mafungufu ambayo yakipatiwa ufumbuzi kwa faida ya afya ya Taifa kwa ujumla [07:58, 13/05/2023] +255 62: Mpaka watu tukaenda kutoa maoni kwenye ile ya jaji wariomba bado tulikua hatuelewi tu?
Hata ukianza saiz kuelimisha watu kuhusu katiba bado kunawengine kwa makuaudi kabisa wataamua wasichukue hiyo elimu ila kwakua wengi kwasasa wanayo iyo elim na watu wameshiriki kutoa maoni Yao tusipoteze muda ikashindwa kukamilika kwa wakat tuendelee na ile ya Jaji Wariomba
[08:13, 13/05/2023] P: Ukisema hivi, na mimi naomba niulize; kwani hiyo katiba ya zamani wangapi wameiona? Wangapi wameisoma? Lini Iliwahi kusambazwa kwa wananchi wakashindwa kuisoma?Na hao “wananchi wengi” tunaosema “hawajui katiba” ni akina nani hasa? Je, ni sisi tuliopo hapa mtandaoni au watanzania kwa ujumla?
Maana kama wengi wetu hapa hatuijui na hatuwahi kuiona ya zamani, achilia mbali kuisoma na kuielewa, je, hao wananchi wa kawaida huko mtaani inakuwaje?
Kwa mantiki hiyo ya “universal ignorance ya katiba”, wanaotegemewa kujadili na kutoa maoni yao na yachukuliwe serious, ni akina nani hasa? Maana sehemu kubwa ya watanzania watakuwa hawajui katiba ya zamani, na hata hii ya sasa ni wachache wamewahi kuisoma seriously kifungu kwa kifungu.
Kwa uzoefu wa kawaida, Katiba nzuri, huandaliwa na watu wacheche sana wenye weledi wa kiwango fulani cha mambo sheria, siasa, na utawala. Sehemu kubwa ya wananchi wa kawaida hushiriki m kutoa maoni yao tu wkt wa kukusanya maoni. Baada ya kukusanya maoni ya wenye nchi, hakunaga tena hizi gimmicks za kujizungusha zungusha.
Hata sisi Tanzania tumefanya haya, tena kwa ushirikishaji mpaka sana wa wananchi nchi nzima. “Rasimu ya matakwa ya wananchi” ipo intact kabisa.
Kinachotakiwa sasa hivi siyo kurudia tena kukusanya maoni, kwani tunataka maoni gani zaidi, ya nani, na kwa ajili gani?
Kinachobaki hapo ni timu ya watu wachache tu wenye sifa nilizotaja hapo juu, kujifungia mahala; kuchambua, kuchakata, kudadavua, na kuja na majibu ya kutukwamua tulipokomea last time, that’s it.
Nilidhani lengo la Rais kuunda Timu Kazi, na baadae kum task Msajili wa vyama na kazi ya kuwaita wanasiasa ili wakae na (timu kazi?) Ilikuwa ni kufufua tu kilichokuwa kimetaka kufishwa ili kiendelee kupumua na kuidhi.
Leo tunapianza mijadala ya kuhimizana kutoa maoni tena najiuliza: kumbe tayari imeshaamriwa kwamba mchakato wa kwanza ulikuwa batili, na kwa hiyo muda na gharama iliyotumika tuhesabu ndio tumeliwa?
Au kuna nini ambacho mimi sielewi? 🤷🏾♂️

Wazo langu bado elimu ya uraia inahitajika sinauhakika kama wananchi tunaijuwa katiba kutoka kava yake mpaka ukurasa wa mwisho,
1. Katiba ni nini
2. Kunaumuhimu gani wa kuwa na katiba
3. Je katiba iliyopo ina matatizo gani
4. Kwa nn tunahitaji katiba mpya
Najaribu kuyaeleza haya kwan masuala mengi yakiwemo haya wananchi wengi wanajiliza na kwa bahati mbaya hakuna jibu ambalo litamuezesha mwananchi wa kawaida kutoka hapa tulipo na kuingia katika hiyo mijadala ya katiba.

Elimu inahitajika na nishauru serikali zetu zote mbili kuvihusisha vyombo v…
[10:22, 13/05/2023] A: Hayo maswali manne ni muhimu mno lkn hata ukifatilia hao wanaojita wana harakati wote ni watu Dar Mjini ukiukiza uwakilishi wa wakulima huko vijivini uko wapi hupati jibu na hakuna mwaharakati hata mmoja wa nyamisati au kibondo wote ni wamjini wapiga dili [10:26, 13/05/2023] +255 : wakibondo tupo wasomi… tunawakilisha… ila naonga mkono hoja… wafikiwe wote kama zinavyopitishwa sheria ndogo za halmashuri inamaana mikutano ya wananchi kwenye vijiji na mitaa ifikiwe na kwenye kata. Maana sio wote wako kwenye mitandao wala kusikiliza radio.. [10:29, 13/05/2023] A: sasa nini tufanye ili kufikia malengo?..Mjadala unaendelea………….

Katiba mpya ni muhimu mno kwa kuwa kiuhalisia ina mapungufu kadhaa kama wengi walivyoainisha ila ninashauri kuwe na Ilani ya Taifa pia
[15:41, 16/05/2023] P: Excellent thinking…👍🏽👍🏽👍🏽 [16:12, 16/05/2023] +255 68: Mawazo yangu ni bora tukawa jamhuri ya muungano kama ilivyo sasa ingawa maboresho ya katiba yanahitajika sana kwa mustaksbali was taifa letu [16:20, 16/05/2023] T: Walioukwamisha mchakato ule ni wanasiasa..na ndio maana Rais Samia suluhu Hassan akamtaka Msajili akutane nao waliotukwamisha kwa ummoja wao na mlezi wao..kuyajadili kwa mapana mapendekezo ya kamati na kukubaliana kwa dhamira njema namna ya kuendelea na mchakato kwa ustawi wa Taifa letu..hapa sasa ni nia njema kama muhimili wa yote na sisi tukasema wakati haya yakisubiliwa Tujikumbushe na tuone kwa kiwango gani wanasiasa watajongea na hiyo nia njema….kwa maaana hiyo tiunaendelea piakuyaona kwa ufupi yaliyomo hadi tutafika yaliyojadiliwa na kupendekezwa na kuishia njiani 2015 [16:33, 16/05/2023] +255 68: Mama kafanya jambo kubwa na huenda kaona mbali sana [16:35, 16/05/2023] K: hapa umejibu swali la wengi la “tulifeli” wapi…maana isipokuwa tumekubaliana ; MOSI kwamba tulifeli na PILI sababu ya kufeli tutapata shida kukubaliana kwamba TUNAPOANZA UPYA nini tukwepe na wapi tusiende na kwa vipi tukubaliane kutokubaliana maana ni ukweli usiopingika kuwa hatufurahishana kwa asilimia 100 katika mchakato huu hii ni KANUNI ya ubinadamu hivyo basi naunga mkono hoja kwa kuzingatia Historia twende PAMOJA na TUFUNGUKE [16:50, 16/05/2023] K: Nataka KUAMINI kwamba hatuta “reinvent the wheel” kwenye mchakato huu, tayari KATIBA TUNAYO ila mchakato uliofeli Ulijaribu kupata maoni ya Wananchi na kuchakata na Bunge maalum likaanza Kujadili, wakati wa Mjadala kundi moja la wadau likakasirishwa na jambo wakatoka katika mjadala na hili likatia dosari mchakato mzima; pamoja na kwamba uliendelea na kufikishwa “mwisho” LEO Mh. Rais ameona kuna umuhimu wa kurejelea hili jambo na labda Yeye awe wa kuweka Historia ya Pili (a record) ya kulileta Taifa Pamoja kwa Katiba Mpya yenye Ridhaa ya Asilimia Kubwa ya wananchi *bila ya shinikizo la wanasiasa
Baadhi ya mifano ya ILANI YA TAIFA ni pamoja na mipango ya maendeleo kama vile Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Tanzania (TDSP), Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Zanzibar (PZDP II). Ilani hizi zinalenga kuleta maendeleo ya kiuchumi, kuondoa umaskini, kuimarisha huduma za jamii, kuboresha miundombinu, kukuza ajira na kuleta ustawi wa wananchi kwa ujumla. Sasa hapa sasa ndio
Najaribu tu kutafakari juu ya
Uwajibikaji
Uadilifu
Usawa
Uwazi na Uhuru katika kufanya kazi
Ilani ya chama, kwa upande mwingine, ni mpango wa maendeleo wa kisiasa ambao unalenga kuelezea sera, malengo, na mikakati ya chama cha siasa kwa kipindi cha miaka kadhaa ijayo. Ilani hii inaandaliwa na chama cha siasa, na huwa inashirikisha maoni ya wajumbe wa chama, viongozi wa chama, na wadau wa masuala ya siasa kwa ujumla.
[18:23, 16/05/2023] Tandawili : nilikuwa na jaribu kuona touti kati ya yale mdau aliyoyaona kwa umbali kuwa na Ilani ya Taifa [18:24, 16/05/2023] K: ILANI yaani MANIFESTO? [18:25, 16/05/2023] T: Maono ya Taifa letu Tanzania yanajumuisha kuwa na Taifa lililoendelea kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Tanzania inatarajia kuwa na uchumi imara unaotokana na sekta zote za uchumi pamoja na kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi mkubwa. Pia, Tanzania inalenga kuwa na jamii yenye usawa, yenye afya bora na elimu bora kwa kila mtu. Mbali na hayo, Tanzania inajitahidi kuwa na utamaduni imara, kuhifadhi mazingira na kufanya kazi na mataifa mengine kwa amani na ushirikiano.

Putting it bluntly, ‘Serikali’ ina upungufu mkubwa sana wa ‘quality human resources’ yenye ‘high quality skills set’ wenye kiwango cha ubunifu wa karne ya kiushindani ya 21.
Kwa approach ya sasa ya serikali kuendelea kuandaa mipango ya maendeleo kwa kukusanya vi maoni vya hapa na pale (sijui toka kwa nani, mwenye uelewa na uzoefu toka wapi, God knows) tutaendelea kupata matokeo yale yale huku resources za nchi ziendelea kuwa expended.
We need a different approach. We need specified time and resour…
[19:34, 16/05/2023] P: @P leo umeswich on ! Unelectable hoja tunduizi a forward thinking approach kuleta solutions/suluhishi endelevu za vizazi vya kitanzania #200yearsthinking 🤔 [19:45, 16/05/2023] A: Nimesoma kila neno, haya ni mawazo chanya na yenye nia na maono ya kusonga mbele bila kujali vikwazo duni. [19:56, 16/05/2023] T: huwa nafarijika sana na kuongeza maarifa mno nikisomaga vituvyako walah nasoma neno kwa neno halafu kwa sauti tukifika kwenye ile ya Warioba tutatambua haya mambo yalipangwaje [19:59, 16/05/2023] T: huyu atafutiwe nondo wadau [20:02, 16/05/2023] A: Theory hii ya “separation of power” ina athari kubwa za kiuchumi, kisiasa, na kiusalama.Kiuchumi, inawezesha uchumi kukua kwa kuweka mamlaka tofauti katika mikono tofauti, kwa mfano, serikali inaweza kuweka sheria zinazohusiana na uchumi wakati bunge linahusika na bajeti za serikali.
Kwa upande wa kisiasa, kuwa na mamlaka tofauti kunaweza kusaidia kuepusha madaraka yote kukusanyika katika mikono ya watu wachache. Hii inaweza kusaidia kuzuia ufisadi na kutokuwepo kwa utawala wa kiimla.
Kiusalama, theory hii inaweza kusaidia kudhibiti vitendo vya ukandamizaji wa kisiasa na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuweka mamlaka tofauti na madaraka
[20:37, 16/05/2023] A: Nimesoma Comment yako hii mpaka mwili wangu umesisimkaNakumbuka mwalimu wangu katika somo moja kwenye topic ya
THE ESSENTIAL AND MOST CRITICAL FACTORS FOR NATIONAL DEVELOPMENT
Kuna msingi na nguzo zinazojenga taifa. Kisha mambo mengine yawekwa
Foundation (Msingi)
1. Patriotic and Ethical Leadership at all levels
2. National Unity of Purpose everyone and all resources dedicated to building one “ NATION HOME
3. Strategic Resources – People, Natural Resources and Financial Resources
Pillars (Nguzo)
1. Production – Agriculture, Livestock, Fisheries, Forestry, Mining; Industrial Manufacturing
2. Commerce – Trade, Tourism, Financial Services ( Banking, Insurance, Brokerage ), Media, Marketing,
3. Infrastructure Economic and Social Services;
4.Institutions – Academia, Political Parties, Legislature, Judicial System Courts Statutory and Traditional Community systems of Justice ) Government, Business, Organized Labour, Faith Based Organizations
[20:50, 16/05/2023] A: Huwa inanishangaza sana watu wanapoenda kwenye nyumba za ibada hawalazimishwi na mtu kutoa sadaka na fungu la kumi.Lakini watu wanakuwa waaminifu sana, hii ni kutokana na kwamba wahubiriwa Ideology na wameielewa vizuri sana.
The nation which does not its own Ideology ni kama kipofu anatembea kwenye taa na hajui anapoelekea.
Tukiwa na Ideology as a Nation kila kitu tutakijenga juu yake. Plans, Ethics na vitu vingine vitajengwa kutokana na Idelogy yetu
Kwenye katiba ya sasa imeelezwa Tanzania ni nchi ya Kijamaa inaendeshwa na vyama vingi. Lakini ujamaa wenyewe hatujaueleza ni ujamaa upi huo?
Lazima tueleze ujamaa wetu ipoje kila mtu aujue.
[20:52, 16/05/2023] Asia Mohamed: TUME YA KUDUMU YA MIPANGO, UCHUMI, NA MAENDELEO YA TAIFA ina jukumu la kutekeleza mipango ya maendeleo ya miaka mitano katika nchi ya Tanzania. Tume hii inajumuisha wataalamu wa uchumi, sera na mipango ya maendeleo. Baadhi ya majukumu ya Tume hii ni pamoja na:Kukusanya, kuchambua na kutoa taarifa za kiuchumi, kijamii na kimazingira
Kukusanya na kuchambua data za kiuchumi na kijamii na kuandaa mipango ya maendeleo ya taifa
Kutoa miongozo na ushauri kwa serikali na taasisi nyingine kuhusu sera na mipango ya maendeleo ya taifa
Kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa na kutoa tathmini ya utekelezaji wake. Tujivunie Kuwa Watanzania tuendeleze uzalendo katika kuhakikisha Tunaijenga Nchi yetu kwa maarifa na nguvu zetu zote🇹🇿🇹🇿🇹🇿
[20:55, 16/05/2023] K: Maono….Vision….ya Taifa la Tanzania ni kuwa Taifa lililoendelea kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.👆🏻Wadau mnaonaje hii kama Maono(Vision)
Hili tamko la maono Haitakiwi kuwa mambo mengi, maana ndiyo inatutengenezea Dira na Malengo ya muda mfupi na Mrefu.
Halafu sasa ndipo tunaiweka Katiba ituratibu kufikia maono haya
[12:07, 11/05/2023] P:
Ndugu zangu,
Uzalendo wa kweli huwa haufundishwi darasani kwenye makongamano, warsha, au semina.
Uzalendo wa kweli hufundishwa na Serikali/nchi kuwafanyia wananchi wake vitendo chanya vyenye kuwawekea mazingira sahihi na bora ya kujitegemea na kufikia ndoto zao ndani na nje ya mipaka ya nchi yao.
Mimi sijawahi kufundishwa uzalendo na mtu darasani au mtaani.
Lakini mtu akihoji uzalendo wangu kwa nchi yangu niko tayari kumtoa roho!
Mimi nilijikuta NAIPENDA NCHI yangu na NIKO TAYARI kuipigania, kuilinda, na kuitumikia kwa moyo wangu wote na hata kwa uhai wangu…kutokana na jinsi serikali/nchi yangu ilivyonionesha upendo, kunijali, kunilinda, kunitetea, na kuniwekea mazingira wezeshi ya kuja kuwa hivi nilivyo
[12:23, 11/05/2023] +: Hili neno UZALENDO nadhani linapaswa kutafsiriwa kwa upana once and for all. Tunapaswa tulijue kwa upya na katika tafsiri pana zaidi. Watanzania waliowengi, hasa wenye madaraka wanapaswa ku “unlearn and relearn” maana sahihi ya neno UZALENDO ikibidi liwe defined kwenye katiba.Why? Kwasababu neno uzalendo lilitumika vibaya sana regime iliyopita na kuumiza watu wengi. Kila aliyehoji chochote kama raia huru alikuwa branded kuwa siyo mzalendo, na wengi walipata “taabu sana”
[12:26, 11/05/2023] T: Tutajadili kwa mapana kila jambo hapa lakini mjumbe mwenzetu alikuja hapa na hoja hii na huko nje wadau wa mlezi wanamlalamikia mlezi wao yaani msajili..hoja hii haijaisha..na Msajli yuko hapa… [12:36, 11/05/2023] P:Huenda hata Msajiri akawa hajui maana halisi ya “uzalendo” kwa nchi.
Tusipuuze hili nalo neno..😂😂🇹🇿🇹🇿✅
[12:59, 11/05/2023] Pr:Naomba niulize wawezeshaji wa hili jukwaa : je mchakato huu tunaanza upya kana kwamba uliositishwa haukuleta mambo yaliyokubalika ? Tutawajibikaje na Rasilmali iliyowekezwa kwenye mchakato uliyositishwa dakika za mwisho kwa sababu za kisiasa a a??? Kama kuna mambo ambayo hayakuwa na utata hayawezi kubebwa ili mchakato huu usimbebeshe mlipa kodi mzigo wa ziada? Naomba mwongozo🤷🏽♂️
[13:07, 11/05/2023] T:Hii ni Mada mpya kutoka kwa Mdau..Tunaweza kuendelea nayo tukisubili Nondo za Ofisi ya Msajili? wajumbe mnasemaje? Lakini kwa kifupi Hali ya uelewa wa hili jambo Tangu 2014 ni ndogo mno ukizingatia Vijana wetu wa sasa ambao kwa maelfu walikuwa wadogo kudadavua mambo yale,sasa jukumu kubwa kama wadau ni kujadili kwa mapana hapa na kuwaelimisha wengine juu ya Historia yote ya michakato ya Katiba Yetu na mustakabali wa baadae..wakati jukumu hili la uratibu liko kwa Msajili..wajumbe walipendekeza awali tumjue kwanza Msajili na ofisi yake na majukumu yake..wengi hawajui..hapo ndio tulianzia jana..Prof.
[13:28, 11/05/2023] Dr.:Asante! Baada ya kujua maana ya Katiba tungepata pia historia ya Katiba ya nchi yetu.
[13:36, 11/05/2023] Dr.:Wawezeshaji, naomba kama inawezekana tuwe na muda maalum wa kujadili kila mada. Mfano maana ya Ijue Katiba tujadili kwa siku mbili au tatu. Pia wajumbe wa hili group tuhimizane kutenga muda wa kufuatilia mijadala ya Katiba ndani na nje group 🙏
[13:36, 11/05/2023] A:Nimepitia mada hii vizuri sana na nimeptia kipenegere kwa kipengere.
Nadhani inatupidi tuanze kutazama Katiba kwa mtazamo mwingine. Badala ya kuwaza kitu cha kwanza kuhusu utawala, tuanze kuwanza kuhusu “How to manage our resourse”. Kwa mtazamo wangu msingi wa kwanza ni kuongelea Management of our resource.
Tuanze kuongelea kwanza our National Interest, Kwamba maslahi yapi ya Taifa letu tunataka tuyalinde baada ya hapo ndipo tuweze kuanza kuongelea Utawala, Haki na wajibu.
NB: wazo langu ni kwamba tuanze kwanza na “Management of Our Resources and Defining of our National Interest”
[13:38, 11/05/2023] K:Ikiwa kuna matumizi mabaya/yasiyo ya lazima n.k n.k n.k
Je tufanye Kesi kwanza? Au Tuchukue yatokanayo yanayofaa ili yatumike kwenda mbele kwa ubora? Au tusubiri tuwakamate waliotumia fursa vibaya kwanza…..choices…choices! 🤷🏾♂️
[13:45, 11/05/2023] M: Lisu na Silaha wakilalamika kuwa Rais anaonekana kuuteka mchakato wa Katiba na kuuweka mikoni mwa wale wale. Sijui walitaka afanye nini!! Rais kama taasisi vipo, vyombo chini yake vya kumsaidia kuhahakisha kuwa Katiba inayokusudiwa, inapatikana na kuridhiwa na Watanzania kwa ujumla wao. Hivyo naamini Msajiri wa Vyama vya Siasa ndiye mtekelezaji mkuu wa mchakato huu. Nadhani tusubiri kuona hatua atakazochukua kutekeleza jukumu hili. [13:52, 11/05/2023] T: Ndio maana akamleta Msajili kama mlezi wao aongoze jahazi walitaka aanzie wapi? [13:53, 11/05/2023] A:1. Kwanza kabla ya kuanza kuongelea utawala. Nimuhimu kuongelea Lengo letu sisi kama watanzania kuwa pamoja (The purpose of Nationa)
2. Foundations of our nation. Je, Taifa letu lina misingi ipi? (Philosophical, Moral, Cultural) Hii ndiyo misingi.
3. What is our national interest (Sisi kama Taifa maslahi yetu ni yapi. Kutokana na maslahi yetu tunataka tujenge taifa la namna gani?)
3. Lazima tuangalie hustoria yetu. Yaani tunataka Tanzania ya sasa lakini ni vizuri kuikubali historia yetu.
ALL NATIONS HAVE FUNDAMENTAL INTERESTS THAT THEY WOULD LIKE TO DEFEND AND PRESERVE
[13:55, 11/05/2023] T:Muda tutaupanga sisi hapa nashauri kwa vile kunauchambuzi kwa sauti pia ni vema wadau kuwe na mpangilio kwa kifupi Tumeanza vyema na sasa tuweke bayana nini tunapaswa kukiweka awali HISTORY KWANZA
[13:57, 11/05/2023] P:Kwa vile Mwenzeshaji ameshauri tuairishe hii mada basi ngoja nisubiri wakati Mwafaka. Kwa ufafanuzi wangu nilieibua hii mada niseme tu kwamba kwa vile katiba ni Sheria mama/Sheria kuu inayobainisha misingi mikuu inayoelekeza mamlaka na mipaka ya wenye dhamana ya kuongoza na kubainisha haki za raia na wajibu wao pamoja na misingi ya uwajibikaji, basi bila Shaka mchakato uliyositishwa kulikuwa na misingi ambayo haikuwa na utata🤷🏽♂️je hatuwezi kuibeba? Hilo ni swali kuhusu mchakato🤷🏽♂️
[14:07, 11/05/2023] P:Hii ya kuanza kuelimishana kuhusu Katiba Mpya ni tactical maneuvre ya irresponsible stakeholders kuchukua hatua stahiki kumaliza hii deadlock.
Kwani tunataka wananchi waelimishwe juu ya Katiba kwani wao ndio waliokwamisha mchakato kukamilika?
Kama wananchi walizungukiwa nchi nzima wakatoa hadi maoni yao juu ya Katiba Mpya kweli walikuwa hajui wanachokifanya?
Unajua kuna vitu vinfanywa mpaka unacheka.
We are an independent nation of more than 60 years. Lakini kuna vitu tunafanya kama watoto wa miaka 6.
We wasted taxpayers money on a sham exercise. We should be ashemed and apologize to the public.
Badala yake tunataka kuwarudia waliokwisha kutupa maoni yao juu ya Katiba kuwaelimisha nini?
How absurd..
[14:10, 11/05/2023] P:Watu wengi kina nani? Kwani hao watu wengi wasioelewa huwa tunasubiri waelewe kwenye mambo mengine yote yanayoamriwa bila uelewa au consent yao?
The rest is same old staff that have gotten this nation into this s**t
[14:42, 11/05/2023] M:Tusiyumbishane bure hapa. Ushiriki wa watu kwenye jambo lolote lile kote duniani, ni kupitia uwakilishi. Ndio maana tuna vyama vya siasa wanaowasilisha itikadi za vyama vyao kwa umma, na wabunge katika ngazi ya kuisimamia serikali na kutunga sheria. Hivyo mtu kusema watu wengi waelewe kwanza ndipo hatua zaidi zifuate, huo uwingi unaupima vipi kama sio kwa njia za kiuwakilishi zilizopo kufutana na Katiba na sheria za nchi! Group hii ni uwanja wetu kuchangia kile mtu anachokiona kingefaa kuzingatiwa au kuangaliwa katika mchakato huu wa sasa wa kutupatia Katiba itakayoridhiwa na umma wa Watanzania kupitia uwakilishi kwa njia moja au nyingine. Tushiriki kutoa mawazo/maoni humu ambayo naamini wahusika watayatumia katika ngazi zao za uwakilishi.
[14:47, 11/05/2023] T:Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 Ongezeko la watotoni Mil 16 baada ya miaka 10 wengi wao watakuwa watu Wazima Rudi nyuma sensa ya 2012 mwaka mmoja baada ya mchakato kuanza..watoto wale ambao ni more than 40% ya raia wote leo ni watu wazima wala hawakuhusika kabisaa na hayo maoni na ndio kizazi kina hoji nini kilitokea
[14:49, 11/05/2023] T:Na ndio maana hata wewe leo huelewi kwanini Msajili anajukumu hili leo…
[14:51, 11/05/2023] P:Ufikiri wa aina hii ni very mediocre. Tukianza kusubiriana kila mtu ashikishwe basi hata hii Katiba iliyodumu kwa mingo zaidi ya 4 sasa ni uhalifu kwa wale ambao hawakushirikishwa?
[14:57, 11/05/2023] T:Ndio maana uko hapa kujadili namna bora ya kupata katiba bora kama Rais alivyoainisha na kumtaka Msajili kutekeleza jukumu la msingi kuwaita washirika wake wakuu vyama vya siasa wewe na walioleta mada wakataka kujua nini wajibu na jukumu la msajili katika hili Tuendelee kutoka hapo
[15:00, 11/05/2023] P:Nina hofu wadau wenzangu kuhusu mchakato wa Katiba ya Wote kuendesha na vyama vya siasa.vyama hivi ni wadau wanaowakilisha sehemu ndogo tu ya Watanzania. Hivyo Vina uhalali wa kushiriki kama wadau wengine , asasi au mashirika mengine: kwa maoni yangu Vyingi haviongozwi na misingi ya demokrasia( internal democracy) Mimi najiuliza kwanini Asili Mia tisini ya vyama tangu viundwe hadi Leo vinaongozwa na watu walewale tena wanaume 🤷🏽♂️Ni vyama vingapi vimefungua milango ya demokrasia shirikishi? Kwenye uongozi?? Kwangu mimi kuwe na tume huru ya kuongoza mchakato ili dhamira ya Rais wetu ya kuleta mabadiliko katika mifumo kandamizi na ya ubaguzi.
👆👆👆👆👆Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.
[15:08, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU:
1. Napongeza Mwanzilishi wa Jukwaa hili kwa maana litasaidia kupata mawazo mapya; mbadala; kujikumbusha tulikotoka, tulipo na tunakokwenda ni wapi kuhusiana na suala la Katiba.
2. Mimi ninavyojua ni kwamba, Mchakato kuhusu mwendelezo wa Mabadiliko ya Katiba mpya ya Tanzania “Bado haujaanza rasmi katika kuuendeleza.” Kwa sababu:-
2.1: Tangazo la Serikali bado halijatolewa tena kuhalisha Mwendelezo wa Mchakato.
2.2: Bado hakuna na haupo Mwongozo wowote juu Mwendelezo wa suala hili maana siku zimepita nyingi saana tangu kukoma kwa Mchakato wa Katiba na Tangazo la Serikali likatoka juu ya kukoma kwake.
2.3: Tangu kukoma kwake, imepita takriban miaka 9 (hii ni miaka mingi) ambayo inatutaka kama taifa pengine Mchakato uanze upya ama uwe na mwendel…
[15:09, 11/05/2023] P:Naelewa mno ndio maana naona this is yet another waste of the Tanzanian people’s time and tax money.
It’s time tuwaheshimu watanzania na kuwaona wana akili timamu. Wanajua kinachoendelea wa sehemu kubwa tusema hawana tabia a ku protest kwa kila kitu.
Why these gimmicks every now and then?
The country has a lot of more pressing issues to deal with than keep tip toeing around Katiba Mpya wakati tunajua kinachoweza kufanywa na tunaweza kukifanya without all these back and forth drama.
[15:11, 11/05/2023] M:Mimi nadhani kazi kubwa ilifanyika chini ya Tume ya Warioba. Jambo la kuangalia tulikwama wapi na nini kifanyike kukwamua mchakato huu. Kwa wale wenye muda, tuipitie Rasimu hii na kutoa maoni yetu.
[15:15, 11/05/2023] T:Wazo la kujadili pamoja kwa staha ni jema.. na ndio maana mijadala hii ipo tumeanza na namna tunaovyona Msajili na majukumu yake anatakiwa atupitishe wapi Mjadala huu unaendelea na tutafika kote wajumbe wanakotaka tupite na uzuri wadau wote wako hapa..nashauri Lugha za staha na kuepuka mihemko ili tuwe na mawazo yenyetija kwa mustakabali wa pamoja…
[15:26, 11/05/2023] Pasta Martin: Precisely!Tume ya Warioba walifanya kile ambacho hakijawahi kufanyika katika historia ya nchi hii nzuri.
Kwa mara ya kwanza maoni ya wananchi yalikuwa broadly collected and accurately documented.
Tunajua wananchi (wenye nchi yao) walichotaka. Tatizo hatujawahi kuwa na utamaduni wa kuheshimu wanachotaka wananchi!
Demokrasia yetu ni ya kijanja janja hivi. Hata pale tunapojua wananchi wanataka nini lazima tu edit kidogo ili kuingiza matakwa yetu binafsi.
Even on this attaempt, we are commiting the same sin of arm twisting the public to bend to our tune.
Mchakato ulishaisha. Msimamizi wa mchakato bado yupo hai. Mzee Warioba bado yupo timamu kabisa. Kama nia yetu kweli ni kuheshimu maoni ya watanzania, kwa nini asiitwe msimamizi wa ukusanyaji wa maoni pek…
[15:31, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 2:
1. Msajili wa Vyama vya Siasa yuko chini ya Mamlaka katika Mhimiri mtambuka. Kwa hiyo, sio Mhusika Mkuu wa kuuendeleza Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba mpya ya Tanzania.
2. Ninavyojua Mwendelezo wa suala hili liko chini ya “Wizara ya Sheria na Katiba” ndo wanaotakiwa kutoa Mwendelezo na Kutuongoza tunaanzaje na tunaendaje.
3. Kiongozi wa Jukwaa letu hili, ajikite katika kushinikiza Mwendelezo na uhalalishaji wa Mchakato husika.
[16:21, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 3:
1. Hoja/Mada ya kwanza iwe KUJIKUMBUSHA KUHUSU, “Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mchakato ulianzaje, Ulifanyikaje na Uliishia wapi!?.”:-
1.1: Kwa nini Wananchi walidai Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.?
1.2: Je, Wananchi na wadau mbalimbali walishiriki kikamilifu kutoa Maoni yao!?
1.3: Bunge la Katiba lilifanya kazi yake ipasavyo kuwakilisha makundi ya Jamii yote ya Tanzania kuipata Katiba waitakayo.?
1.4: Nini kilikwamisha kutokuwepo Katiba Mpya licha ya Mchakato kufanyika na ushiriki wa Wadau wa makundi yote kushiriki!?
2. Hoja/Mada ya pili iwe NAFASI NA WAJIBU WA SERIKALI KATIKA KUUENDELEZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:-
2.1: Kwa sasa Serikali ifanye n…
[16:25, 11/05/2023] A:Naona sijajibiwa hoja yangu ipasavyo, pengine tujuzane tu Hali ya sasa na takwimu za sasa juu ya uelewa wa Mtanzania kuhusu maswala ya katiba Tanzania ikoje maana naona kama kuna mkanganyiko baina ya wanaojua na sisi tusiojua..
[16:40, 11/05/2023] K:Mimi Sijaweza kupata takwimu kamili za hivi karibuni juu ya uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya katiba nchini Tanzania. Hata hivyo, ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya katiba ni mdogo. Ripoti ya Jukwaa la Katiba Tanzania iliyochapishwa mwaka 2019 inaonesha kuwa asilimia 62 ya wananchi hawajui kuhusu mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania.
Ripoti nyingine ya Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ya mwaka 2018 inaonesha kuwa asilimia 50.8 ya wananchi hawaelewi kikamilifu maudhui ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ripoti hiyo inaeleza kuwa wananchi wengi hawajui wajibu na majukumu ya serikali na wananchi, haki za msingi za binadamu, utawala bora na demokrasia.
Hata hivyo Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan , amesiskika mara kwa mara akizitaka Taasisi za Kiraia na zile za kidini wasaidie katika kutoa elimu ya uraia katika katika maeneo haya, na wengine waliopewa majukumu naamini kabisa kuwa moderator umewaweka humu.
Ni muhimu sasa kwa serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari, na taasisi nyingine kushirikiana katika kutoa elimu na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya katiba na mchakato wa kupata katiba mpya nchini Tanzania. Hii itasaidia kujenga uelewa wa pamoja kwa wananchi na kuongeza ushiriki wao katika mchakato huu muhimu wa kitaifa.
[16:41, 11/05/2023] K:Ninaunga Mkono Hii Hoja ni sawa sana!!
[16:44, 11/05/2023] K:1. Hoja/Mada ya kwanza iwe KUJIKUMBUSHA KUHUSU, “Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mchakato ulianzaje, Ulifanyikaje na Uliishia wapi!?.”:-
[16:45, 11/05/2023] Pasta Martin: This is a non-issue guys.Watanzania wengi au wachache kujua Katiba au kutojua haizuwii au kusababisha chochote kifanyike au kisifanyike.
Kuna mambo mengi tu watanzania hawajui na yanafanyika lkn hakuna tatizo.
Kwa Katiba, watanzania wanajua sana tu. Na walitoa maoni yao. Sasa hiyo kusema hawana uelewa inatoka wapi. Mi naona wasioelewa au wanaojifanya hawaelewi ni sisi wasomi na wajanja wachache tunaojadiliana humu kwenye mitandao.
[16:49, 11/05/2023] K:Hoja hii ya uelewa wa wananchi imetokana na ripoti za Utafiti na nadhani wasomi wanatembea na hizi takwimu ….ndicho kinachotatarajiwa kutoka kwa wasomi
[16:49, 11/05/2023] M:Mimi nadhani suala la Katiba kwa mwanchi wa kawaida, kwake is not an issue. Yeye anachohitaji ni utawala bora unaokidhi haki na huduma zake muhimu za kijamii. Zinapatikana vipi sio tatizo kwake. Hapo ndipo linapokuja suala la uwakilishi kupitia kwa wale wanaolewa nini maana ya Katiba ambayo ni sheria mama. Hivi niulize tu ni wangapi kati yetu siku za nyuma tumewahi kuhangaika kutafuta Katiba yetu inasemaje juu ya mambo mbali mbali? Ni kiri mimi sio miongoni mwa wale ambao nimewahi kujighulisha sana kujua vifungu vya Katiba yetu vinasemaje. Na kwa hali hiyo, sishangai sana watu kutoijua Katiba. Kama iliyopo mtu huijui utasumbuka kweli ni hiyo inayopiganiwa!!! Tuelezane ukweli tu kwamba Katiba ni eneo moja la taaluma ya Kisheria. Hata kwenye mijadala ya aina hii tuntegemea wanasheria kushiriki na kutuongoza zaidi. Huu ndio ukweli wenyewe.
[16:52, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 4 KULINGANA NA ULIVYOULIZA:
1. Suala la utoaji wa Elimu kwa Raia kuhusiana na Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lazima utolewe Mwongozo wa Elimu yenyewe, kwa sababu kama Mchakato/Mwongozo toka Serikalini haujaanza rasmi AZAKI na Taasisi mbalimbali zitatoa Elimu gani.!?
[16:52, 11/05/2023] +255:Na ndiyo maana tuna wana sheria, hao kazi yao ni kusoma na kuelewa katiba, sheria na kanuni. Sisi wananchi tunataka utawala bora unaofuata sheria, kwa upande wa wananchi awatakaa waielewe sheria tena hasa hii iliyoandikwa kwa kizungu. Mamlaka zinachoweza kufanya ni kutengeneza uelewa wa haki za watu hayo mengine tutakutana mahakamani😊
[16:53, 11/05/2023] K: exactly [16:54, 11/05/2023] K: Elimu ya aina ya Elimu! [16:54, 11/05/2023] M: 👍 [16:54, 11/05/2023] M: 👍👍👍 [17:02, 11/05/2023] : ipi sasa namna bora ya kutoa elimu ya katiba na mchakato ndio huu uko jikoni [17:05, 11/05/2023] K: 🤔Kwa Kufikiri kwa sauti NINACHOONA, Kutoa elimu ya Katiba kunapaswa kuwa endelevu na yenye kufikia watu wengi iwezekanavyo. Hapa ni baadhi ya njia bora za kutoa elimu ya Katiba:1. Kutoa elimu ya Katiba katika shule: Elimu ya Katiba inapaswa kuanza mapema shuleni. Wanafunzi wanapaswa kufundishwa kuhusu maana na umuhimu wa Katiba na jinsi inavyoongoza nchi yetu.
2. Matumizi ya teknolojia: Matumizi ya teknolojia kama vile mitandao ya kijamii, redio, televisheni, na programu za simu yanaweza kutumika kwa kutoa elimu ya Katiba kwa watu wengi zaidi.
3. Kutoa mafunzo kwa wanasiasa: Wanasiasa wana jukumu la kuelimisha wananchi kuhusu Katiba. Hivyo, mafunzo yatolewe kwa wanasiasa kuhusu maudhui ya Katiba ili waweze kutoa elimu sahihi kwa wananchi wao.
4. Kutoa semina na mihadhara: Semina na mihadhara ya umma yanaweza kutoa fursa kwa wataalamu wa Katiba na wananchi kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Katiba.
5. Kutoa machapisho na vifaa vya elimu: Vifaa vya elimu kama vile vipeperushi, machapisho, na vitabu vinaweza kusambazwa kwa wananchi kama njia ya kutoa elimu ya Katiba.
Kwa ujumla, njia bora ya kutoa elimu ya Katiba ni kutumia njia mbalimbali za mawasiliano ili kufikia watu wengi iwezekanavyo na kuifanya iwe ya kuvutia na inayoeleweka kwa wananchi wote
[17:09, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 5:
1. Niombe kiongozi/viongozi wa Jukwaa hili kutenga muda na saa maalumu ya kuchangia hoja (Mfano Jioni/Asubuhi/Usiku ya siku inayofuata ndio Hoja/Mada itachangiwa na Itatolewa kwa wote ili siku inayofuata kwa muda utakaowekwa kuchangia).
2. Napendekeza Hoja/Mada moja isizidi SAA 1.20.
3. Baada ya Hoja/Mada kujadiliwa, yatolewe Majumuisho na Maazimio.
[17:10, 11/05/2023] K:Ni Haki ya Rais kuwa ndiye ‘custodian’ wa mchakato huu kwa nia njema tu, kwa nafasi yake kama The Executive anatarajiwa kuwa ndiye mjibu maswali pindi mambo yakienda mrama ( of which hatuombi yatokee ) but, Asante Hon Judge kwa insight hii!!🙌🏽
[17:11, 11/05/2023] M: 👍👍👍Safi
[17:12, 11/05/2023] T: Kunamambo ya kujifunza hapa safi sana..mchanganuo wenye tija [17:15, 11/05/2023] +25: Kwani wanamlalamika bila kushauri? Muhimu tuangalie nini kinashauliwa kutoka kwako na sio kutaka watu Woote wasifieMe naona hata hao wasaidizi wake pia wanategemea mawazo yetu na taasisi inajua kutakua na lawama ushauri
[17:15, 11/05/2023] M: Mimi nafikiri katika mijadala itakayofuata na nadhani hata hii ambayo imekwisha anza, ijikite zaidi kutafuta sababu za kukwama kwa mchakato wa Katiba uliopita. Tukivuka ngazi hiyo kwa kuafikiana, then tatakuwa tumepiga hatua mbele ya kupata Katiba tunayoitaka. [17:17, 11/05/2023] M: Safi..!👍 [17:36, 11/05/2023] +255:kwa Kuzingatia Haya. kuwe na utaratibu mzuri wa kuwafikia viongozi wa serikali za mitaa(kata) na viongozi wa vyama vya siasa (kata) nchi nzima hapa ndio mzizi wa fitina wa kujua au kutoijua katiba kwa wananchi utakua ukomo wake na maoni yatapatikana hapa na kila kitu kama sheria zote ndogo au sheria za halmashuri zinavyoshirikishwa kwa wananchi na zinapelekwa bungeni na mwisho kufanya kazi hili muhimu sana…. ngazi ya chini ya serikali za mitaa na vyama vya siasa uko chini linatibu kila kitu…
[17:42, 11/05/2023] P:Kuna nchi nyingi tu duniani ambazo wananchi wake hawajui Katiba yao inasemaje, na hawajali.
Lakini kutokana mifumo imara ya kiutawala na UZALENDO wa viongozi wao husikii watu wakipewa elimu ya Katiba. Ili iweje?
Sisi hata tukifundishana katiba tukatoa na mitihani kabisa. Kama nia ya Katiba mpya haipo haipo tu.
Tutapeana elimu. Tupoteze muda. Tutatumi pesa. Lakini kama nia haipo, itabaki hivi hata miaka 10 ijayo.
[17:49, 11/05/2023] +:Jamani mimi ni mgeni humu ndani, tafadhali msinipige mawe….. Katika huu mchakato mpya wa katiba mpya, ile katiba ya Warioba inawekwa wapi? Au inakuwa kama Research Report!?? Maana kama kumbukumbu zangu ziko sahihi ilikuwa karibu na stage ya adoption. Na kama inakuwa considered, je mchakato utapaswa kuanzia stage gani??
[17:51, 11/05/2023] Kopwe:ni vyema tusifike hapa👆🏾 labda tunapishana namna nina Imani hata kama dhamiri haikuwepo sasa ipo tuanzie hapo! kwa kujenga juu ya “tofali hili”
[17:55, 11/05/2023] T:Nini sasa wajibu wa vyama vya siasa katika mchakato wa katika kwa sasa kunawano laumu na tukirudi nyuma hawa hawa wametufikisha hapa….
[18:10, 11/05/2023] K:Vyama vya siasa jukumu lao ni kubwa sana katika mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania kwa hapa tulipo. Ninaamini wana Wajibu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu, kwanza kwa kutoa maoni yao kuhusu vipengele mbalimbali vya katiba mpya na Pili, kutoa mapendekezo yao kwa ajili ya kuboresha rasimu ya katiba.
Tunaweza kuona mifano ya wajibu wa vyama vya siasa katika mchakato wa katiba ambayo ni pamoja na;
1. Kutoa maoni yao kuhusu vipengele mbalimbali vya katiba: Vyama vya siasa vinapaswa kutoa maoni yao kuhusu vipengele mbalimbali vya katiba mpya, kama vile mfumo wa serikali, muundo wa bunge, muundo wa vyombo vya dola na masuala mengine yanayohusiana na demokrasia na utawala bora.
[18:15, 11/05/2023] K:2. Kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa katiba: Vyama vya siasa vinaweza kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba kwa kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa katiba mpya na kuwahimiza kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya katiba.
3. Kutoa mapendekezo ya kuboresha rasimu ya katiba: Vyama vya siasa vinapaswa kutoa mapendekezo yao kwa ajili ya kuboresha rasimu ya katiba, kwa kuzingatia maslahi ya wananchi na mahitaji ya taifa kwa ujumla.
4. Kusimamia utawala bora na demokrasia: Vyama vya siasa vinapaswa kusimamia utawala bora na demokrasia kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa katiba unafanyika kwa njia ya uwazi, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora.
Kiukweli, vyama vya siasa vina jukumu muhimu katika kutoa maoni yao, kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi na kusimamia utawala bora na demokrasia.
[18:22, 11/05/2023] T: Karibu sana pamoja na kwamba swala hili liko Mbele lakini wataalamu hapa watakujibu kwa kifupi ili tuiweke kama MADA Baada ya kujadili wazo la @M “1. Hoja/Mada ya kwanza iwe KUJIKUMBUSHA KUHUSU, “Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mchakato ulianzaje, Ulifanyikaje na Uliishia wapi!?.”:- [18:31, 11/05/2023] T:Nakumbuka Mwanasheria Nguli na mataalamu mambo ya katiba ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu alisema Namnukuu “mchakato wa Katiba Mpya lazima utungiwe Sheria mpya ,sheria iliyounda Tume ya Warioba na Bunge Maalum la Katiba haiwezi kutumika tena, sababu ilishakamilisha majukumu yake.
Hivyo, tutachukua baadhi ya mambo mazuri kwenye rasimu ya Warioba, tutachukua baadhi ya mambo kwenye Katiba pendekezwa na kuyaunganisha na mawazo mapya ya wananchi ili tupate Katiba Mpya iliyo bora.”
Rais Jakaya Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba . Katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam April 6,2012 katika hafla iliyoshuhudia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani na badhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbali mbali.
April 6,2012 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza rasmi majina ya wajumbe walioteuliwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Kikwete aliyataja majina hayo mbele ya wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alisisitiza kwamba kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa. Ila kisheria tume ilitakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________
UONGOZI WA JUU
1.Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA
– Mwenyekiti
2.Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
RAMADHANI
– Makamu Mwenyekiti
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – BARA
1.Prof. Mwesiga L. BAREGU
2.Nd. Riziki Shahari MNGWALI
3.Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI
4.Nd. Richard Shadrack LYIMO
5.Nd. John J. NKOLO
6.Alhaj Said EL- MAAMRY
7.Nd. Jesca Sydney MKUCHU
8.Prof. Palamagamba J. KABUDI
9.Nd. Humphrey POLEPOLE
10.Nd. Yahya MSULWA
11.Nd. Esther P. MKWIZU
12.Nd. Maria Malingumu KASHONDA
13.Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)
14.Nd. Mwantumu Jasmine MALALE
15.Nd. Joseph BUTIKU
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – ZANZIBAR
1.Dkt. Salim Ahmed SALIM
2.Nd. Fatma Said ALI
3.Nd. Omar Sheha MUSSA
4.Mhe. Raya Suleiman HAMAD
5.Nd. Awadh Ali SAID
6.Nd. Ussi Khamis HAJI
7.Nd. Salma MAOULIDI
8.Nd. Nassor Khamis MOHAMMED
9.Nd. Simai Mohamed SAID
10.Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA
11.Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN
12.Nd. Suleiman Omar ALI
13.Nd. Salama Kombo AHMED
14.Nd. Abubakar Mohammed ALI
15.Nd. Ally Abdullah Ally SALEH
UONGOZI WA SEKRETARIETI
1.Nd. Assaa Ahmad RASHID
– Katibu
2.Nd. Casmir Sumba KYUKI
– Naibu Katibu
[17:18, 10/05/2023] AG:
Nimepitia majibu ya wadau juu ya Msajili na vyama vya siasa, lakini huku mtaani uhusiano wa siasa za Tanzania na Katiba mpya haueleweki, mara wanaharakati wanasema tusiwaachie wanasiasa, mara serikali itauvuruga, mara mchakato ni wa wananchi, bado najiuliza pengine si mimi tu…Siasa za Tanzania na Katiba mpya vina uhusiano gani na mlezi wake ni MSAJILI?
MAJIBU
Siasa za Tanzania na Katiba mpya zina uhusiano mkubwa kwani siasa za Tanzania zinaathiri mchakato wa kupata katiba mpya na maudhui ya katiba yana athari kubwa katika mfumo wa siasa za Tanzania.
Katiba mpya inatarajiwa kusimamia mfumo wa siasa za Tanzania, kwa kuainisha muundo wa serikali, utaratibu wa utawala, utengenezaji wa sheria, utawala bora, na mambo mengine yanayohusiana na utawala wa nchi.
Katiba mpya itasimamia haki na wajibu wa serikali na wananchi na itaimarisha demokrasia na utawala bora.
Siasa za Tanzania zina athari kubwa katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Viongozi wa siasa na vyama vya siasa wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maudhui ya katiba mpya na wanaweza kushawishi mchakato wa kupata katiba mpya. Pia, siasa za Tanzania zinaweza kuathiri upatikanaji wa rasilimali na ushiriki wa wananchi katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Kwa hiyo, ili mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuwa na mafanikio, ni muhimu kwa siasa za Tanzania kuzingatia maudhui ya katiba na kusaidia kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa njia ya uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali wa kisiasa na kijamii.
TUNAULIZANA HAPA; Nini utofauti wa siasa za Tanzania na katiba ya Tanzania sasa?
Kuna tofauti kati ya Siasa na Katiba ya Tanzania lakn pia kuna uhusiano mkubwa wa siasa na katiba kwa nchi yeyote ile kama ifuatavyo;
1.Siasa ni mfumo wa kutawala au kusimamia mambo ya nchi ambao unahusisha shughuli za kisiasa kama vile uchaguzi,uteuzi wa viongozi wa serikali na maamuzi mengine ya kisiasa.Siasa inahusisha vyama vya siasa ambavyo vinashiriki ktk uchaguzi na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
2.Katiba ya Tanzania ni sheria kuu ambayo inaweka mfumo wa utawala,haki na wajibu wa raia na serikali na taratibu za kufanya maamuzi ya kisiasa.Katiba inaelezea Mamlaka na majukum ya vyombo vya dola kama vile,Mahakama,Bunge na Serikali.
3.Katiba pia inalinda haki na uhuru wa raia,na inatoa mfumo wa kudhibiti madaraka ya serikali.
Kwahiyo tofauti kuu kati ya Siasa na Katiba ni kwamba; Siasa inahusisha shughuli za kisiasa na Utawala wa nchi,wakati Katiba ni Sheria kuu inayoongoza shughuli hizo za kisiasa na utawala wa nchi.
Ahsante.
Mwl.Suleiman Ahmad
Usagara Sec
TUJADILI
WAJIBU WAKE NI NINI
MAJIBU
Mjumbe wa kwanza alitaja majukumu ya Msajiri wa vyama vya siasa
1. Usajili wa vyama vya siasa:
Msajili wa Vyama vya Siasa anawajibika kusajili vyama vya siasa vinavyotaka kufanya kazi nchini Tanzania. Vyama hivi vinatakiwa kutimiza matakwa ya kisheria kama vile kuwa na katiba na kanuni, na kuwa na wanachama wa kutosha.
2. Kusimamia shughuli za vyama vya siasa:
Msajili wa Vyama vya Siasa anasimamia shughuli za vyama vya siasa nchini Tanzania kuhakikisha kwamba vyama hivyo vinazingatia sheria, kanuni na taratibu za kisheria.
3. Kutoa ushauri na miongozo:
Msajili wa Vyama vya Siasa anatoa ushauri na miongozo kwa vyama vya siasa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa vyama hivyo.
4. Kufuta usajili wa vyama vya siasa:
Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kufuta usajili wa chama cha siasa endapo chama hicho kitakiuka sheria, kanuni na taratibu za kisheria.
Kwa hiyo, sheria hizi zinatajwa kuwa ni baadhi ya sheria zinazozorotesha uhuru wa vyama vya siasa nchini Tanzania, na zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu.
[12:22, 10/05/2023] J.Kiukweli Gap la msajili wa vyama vya siasa na mwananchii wa kawaida ni kubwa mno na kutokana na ukubwa huo unapelekea mtu wa kawaida nje ya chama cha siasa hahusiki juu ya msajili wa vyama vya siasa niombe ili mjadala uwe mzuri kwa wadau wote mwenye uelewa juu msajili uwepo wake kisheria atatusaidia wachache tusiojua ili tushiriki kikamilifu.
[12:23, 10/05/2023] T.Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imejikita katika usimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo na ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini. kwa vile wako hapa wote watatudadavulia vyema
[12:25, 10/05/2023] J.Kuletwa tu hapa na hao wajumbe wawili inatoa mwanya kuksanya Nondo kuujulisha umma yote tutayajadili mpaka kieleweke…Karibu
[12:36, 10/05/2023] J.Hii ni changamoto kubwa sana kwani wengi hawajui kabisa na wachache wanajua yupo mwenye cheo hiki cha msajili japo hawajui majukumu yake na kidogo wanajua kila kitu juu ya uwepo wake na chini ya sheria ipi hivyo haja ya kuwaelimisha wengi ni kubwa sana.
[13:17, 10/05/2023] A.Wataalamu wa sheria watatuongoza zaidi lakini nafikri kuna hatua mbalimbali ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kuboresha utendaji kazi wa Msajili wa vyama vya siasa nchini:
1. Kwanza, ni muhimu kufanya mabadiliko ya kisheria ili kuondoa upendeleo wowote wa kisiasa na kuimarisha uhuru wa vyama vya siasa
2. Ni muhimu kuimarisha utendaji wa Msajili kwa kumwezesha kufanya kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na mashinikizo yoyote ya kisiasa ikiwemo chama tawala
3. Ni muhimu kwa serikali kuhakikisha kuwa Msajili anapata rasilimali za kutosha kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hii inaweza kujumuisha kumpatia wafanyakazi wenye ujuzi na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kazi zake
[13:21, 10/05/2023] b:Jukumu la msajili wa vyama vya siasa katika mchakato wa katiba Tanzania kutokana na barua ya Rais ni lipi na mbona analalamikiwa sana huku mitandaoni. Anatakiwa aishie wapi msajili wa vyama vya siasa kutokana na barua ama maelekezo ya Rais?
MAJIBU
[13:42, 10/05/2023] S:Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,
Jukumu lake katika mchakato wa Katiba nchini Tanzania ni kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa ili kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Kwa msingi huo, Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu muhimu katika kuhakikisha kuwa wadau wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato huo wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania.
Pia, Msajili wa Vyama vya Siasa anatarajiwa kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambayo ni miongoni mwa sheria ambazo zinatarajiwa kufanyiwa marekebisho wakati wa mchakato wa kupata Katiba mpya.
[13:42, 10/05/2023] S: Kwa uelewa wanguNYONGEZA
[13:57, 10/05/2023] T:Ingawa barua hiyo haijatoa mpango kamili wa kazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, inaonekana kwamba ofisi hiyo ina jukumu kubwa katika kuhakikisha kuwa wadau wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania. Hapa chini ni baadhi ya mambo yanayoweza kufanywa na ofisi hiyo kulingana na barua hiyo:
1. Kuitisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa:
Kwa kufuata maelekezo ya Rais, Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kujadili na kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
2. Kuwashirikisha wadau:
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaweza kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wananchi, vyama vya siasa, taasisi za kiraia, na wadau wengine muhimu katika mchakato huo wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania. Hii itahakikisha kuwa maoni ya kila mmoja yanapewa kipaumbele na kuzingatiwa.
[13:58, 10/05/2023] T3. Kutoa maoni na mapendekezo: Msajili wa Vyama vya Siasa anatarajiwa kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria nyingine zinazohusiana na uchaguzi. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa sheria hizo zinaweka mazingira bora ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
4. Kutoa ushauri wa kitaalamu: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaweza pia kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau mbalimbali katika mchakato huo wa kutengeneza Katiba mpya. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa mchakato huo unafanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu zote zilizowekwa.
5. Kusimamia utekelezaji: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaweza pia kusimamia utekelezaji wa mapendekezo yote yanayohusiana na vyama vya siasa na uchaguzi. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa mabadiliko yanayofanyika yanatekelezwa kwa ufanisi na kwa njia ambayo inaweka mazingira bora ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
[13:59, 10/05/2023] Mt:Tufafanuliwe kwa kirefu na undani zaidi kuboresha hali ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, serikali inaweza kuchukua hatua?. kivipi wakati ndio chombo imekiunda yenyewe?
MASWALI YA ZIADA
[14:25, 10/05/2023] b:Sawaa Rais si kesha mpa jukumu Msajiri?na majukumu yake kama yalivyotajwa hapa,Rais Mama,Dr Samia afanye nini ili katiba mpya ipatikane maana kila sehemu Rais…rais na Mjumbe amewataja wananchi na jukumu lao kwa msajiri…
[14:26, 10/05/2023] H:Kama Rais katoa go ahead what’s the way forward? Wengine layman kidogo kwenye hii michakato
MAJIBU KWA MJUMBE B.
[14:36, 10/05/2023] S:Ili kuhakikisha kuwa mchakato wa Katiba mpya unafanikiwa na hatimaye kupatikana Katiba mpya nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kufanya mambo yafuatayo:
1. Kutoa msukumo na uongozi wa kisiasa: Rais anaweza kutoa msukumo na uongozi wa kisiasa kwa wadau wote katika mchakato wa Katiba mpya. Hii inamaanisha kuwa anaweza kushirikiana na wanasiasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuwa kila mtu anashiriki na anaonyesha mshikamano katika mchakato huu muhimu.
2. Kusimamia mchakato: Rais anaweza kusimamia mchakato wote wa Katiba mpya na kuhakikisha kuwa kuna uwazi na ushirikishwaji wa wadau wote. Hii ni pamoja na kufanya kazi kwa karibu na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge, wadau wa kisiasa na asasi za kiraia ili kuhakikisha kuwa mchakato unafanyika kwa njia ya haki na usawa.
3. Kuhamasisha mjadala wa kitaifa: Rais anaweza kuhamasisha mjadala wa kitaifa juu ya mabadiliko ya Katiba na kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru. Hii inaweza kufanywa kwa kuunda majukwaa mbalimbali ya majadiliano, mikutano ya hadhara na vikao vya wadau kuhakikisha kuwa kila mmoja ana nafasi ya kutoa maoni yake.
4. Kuzingatia maslahi ya umma: Rais anaweza kuzingatia maslahi ya umma na kuhakikisha kuwa mabadiliko yanayopendekezwa yanaendana na mahitaji na matarajio ya wananchi. Hii inamaanisha kuhakikisha kuwa Katiba mpya inaleta mageuzi ya kweli ya kisiasa na inakidhi mahitaji ya wananchi kwa kuzingatia utawala bora, uhuru wa kiraia na haki za binadamu.
Kwa kufanya mambo hayo, Rais Samia anaweza kusaidia kuhakikisha kuwa mchakato wa Katiba mpya unafanikiwa na kuleta mabadiliko chanya nchini Tanzania.
[14:42, 10/05/2023] A:Kwa kuongezea nyama kwenye nilichoelezea juu;
Kwanza, inaweza kufanya marekebisho ya sheria za vyama vya siasa ili kuondoa upendeleo wowote wa kisiasa na kuimarisha uhuru wa vyama. Kwa mfano, sheria zinaweza kurekebishwa ili kutoa uhuru kwa vyama vya siasa kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na serikali.
Pili, serikali inaweza kuhakikisha kuwa Msajili anapata rasilimali za kutosha kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hii inaweza kujumuisha kumpatia wafanyakazi wenye ujuzi, vifaa vya kutosha na rasilimali nyingine za kifedha ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Tatu, serikali inaweza kuimarisha utendaji wa Msajili kwa kuhakikisha kuwa anafanya kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na mashinikizo yoyote ya kisiasa. Hii inaweza kufanyika kwa kuhakikish…
[14:43, 10/05/2023] H:Kiongozi mimi nawaza tu,
1.Serikali kwanza ianzishe mchakato wa kutoa elimu kuhusu Kazi za Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kwa wananchi kupunguza huu mtanzuko uliopo.
2. Elimu ya Katiba kwa wananchi wote kwa ujumla inapaswa kutolewa ili kusaidia huu mchakato ili yaliyojitokeza kipindi kile yasijirudie
Huwezi kuandaa mchakato wakati walengwa wenyewe hawana idea yoyote ya kile kinachofanyika kwa kuwa kilichofanyika kipindi kile ni kuanzisha mchakato huku elimu inatolewa at per, misuguano mingi sana ilitokea mwisho wa siku tukafeli.
Kama inaweza kutoa fungu kwajili ya vitu vingine hata hili ni la msingi sana hivyo watoe pesa, waajiri vijana wasomi wawape mafunzo halafu wazunguke nchi nzima kutekeleza hayo majukumu hayo. Hao wasomi wasiwe wanasheria pekee maana hilo nalo tatizo kuja angle hutohitaji hao pekee watahitajika wataalam wa kada nyingine pia kwenye huo mchakato
MJADALA UNAENDELEA NA SASA WAMEKARIBISHWA MSAJIRI NA TIMU YAKE KUJIBU HOJA ZINAZOIBULIWA.