Category: Sheria

MIK

TAREHE 21 OKTOBA, 2022 MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI ALIWASILISHA TAARIFA KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN

MAELEZO YA MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI KWA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI ANAWASILISHA RIPOTI YA KIKOSI KAZI

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa George B. Simbachawene (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu

Mheshimiwa Balozi Hussein Kattanga, Katibu Mkuu Kiongozi

Mheshimiwa Jaji Fransis Mutungi, Msajili wa vyama vya Siasa

Mheshimiwa Mohamed Ali Ahmed, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa

Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Makamu Mwenyekiti wa Kikosi Kazi

Waheshimiwa wajumbe wa Kikosi Kazi mliopo

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

SHUKRANI

 Mheshimiwa Rais, awali ya yote wajumbe wa Kikosi Kazi tunaomba kutumia fursa hii, kukushukuru na kukupongeza kwa juhudi unazofanya za kutuletea Watanzania maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, hususani kuboresha mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini. Mheshimiwa Rais, tunamshukuru na kumpongeza, Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa juhudi anazofanya Zanzibar za kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwemo kuboresha mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa.

CHIMBUKO LA KIKOSI KAZI

 Mheshimiwa Rais, Tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kulifanyika Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Jijini Dodoma ulioitwa “Mkutano wa Wadau wa Kujadili Hali ya Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini Tanzania”. Mkutano huo ulijadili mafanikio na changamoto zilizopo katika suala la demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini. Mkutano huo uliufungua wewe Mheshimiwa Rais na ulifungwa na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 

 Katika mkutano huo, masuala mengi yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa yalijadiliwa na washiriki walitoa maoni na mapendekezo ambayo idadi yake ilifikia tisini na nane (98). Kutokana na wingi wa maoni na mapendekezo yaliyotolewa na kiu ya washiriki wa mkutano huo kuona yanafanyiwa kazi, washiriki wa mkutano huo waliazimia kwamba kiundwe Kikosi Kazi cha kuchambua na kuandaa mapendekezo ya kuwasilishwa Serikalini

UUNDWAJI WA KIKOSI KAZI

 Mheshimiwa Rais, Kikosi Kazi kiliundwa tarehe 23 Desemba 2021 kikiwa na wajumbe ishirini na nne (24), kati ya hao, kumi na sita (16) wanatoka Tanzania Bara na wanane (8) wanatoka Zanzibar. Baada ya Kikosi Kazi kuanza kazi, mjumbe Bibi Christine Solomon Mndeme, Naibu Katibu Mkuu wa CCM alibadilishwa, nafasi yake ilichukuliwa na Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Rais, Uundwaji wa Kikosi Kazi ulizingatia uwakilishi wa wadau waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa uliofanyika tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 Dodoma. Hivyo, muundo wake unajumuisha aina za wadau wafuatao: Wasomi, Wanasiasa, Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Taasisi za Dini, Taasisi za Serikali na Vyama vya Kitaaluma. 

Mheshimiwa Rais, Majina ya wajumbe wa Kikosi Kazi ni haya yafuatayo kwa mpangilio wa alphabeti:-


KAZI ZILIZOFANYWA NA KIKOSI KAZI

Mheshimiwa Rais, baada ya uzinduzi Kikosi Kazi kilianza kazi tarehe 11 Januari 2022. Hadi sasa Kikosi Kazi kimefanya kazi zifuatazo:

  1. kupitia hadidu rejea;
  2. kuchambua hotuba ya kufungua, kufunga, maoni na mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa wadau na kuainisha masuala muhimu ya kufanyiwa kazi;
  3. kuandaa Mpango Kazi wenye masuala tisa (9) yaliyoanishwa;
  4. kuchambua na kuandaa maoni na mapendekezo kuhusu suala la mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa;
  5. kuandaa taarifa ya awali ya Kikosi Kazi iliyowasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12 Machi 2022;
  6. kukaribisha maoni ya wadau;
  7. kutoa maoni kwa Serikali kuhusu utungaji wa Kanuni za kuratibu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa;
  8. kuzungumza na wadau mbalimbali wa demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kupata maoni yao; na
  9. kuchambua maoni ya wadau na 
  10. kuandaa ripoti ya Kikosi Kazi.

MAENEO YA YALIYOFANYIWA KAZI

Mheshimiwa Rais, baada ya uchambuzi wa kina wa hotuba ya kufungua na kufunga, maoni ya wadau yaliyotolewa katika Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa wa tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021, Kikosi Kazi kiliainisha masuala tisa (9) ya kufanyia kazi yafuatayo:

  1. Mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani ya Vyama vya Siasa;
  2. Masuala yanayohusu Uchaguzi;
  3. Mfumo wa maridhiano ili kudumisha haki, amani, utulivu na Umoja wa kitaifa;
  4. Ushiriki wa Wanawake na Makundi Maalum katika siasa na Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa;
  5. Elimu ya Uraia;
  6. Rushwa na Maadili katika Siasa na Uchaguzi;
  7. Ruzuku ya Serikali kwa Vyama vya Siasa;
  8. Uhusiano wa Siasa na Mawasiliano kwa Umma; na
  9. Katiba Mpya.

Mheshimiwa Raisili kupata mtazamo mpana kuhusu masuala tisa yanayofanyiwa kazi, tarehe 14 Aprili, 2022 Kikosi Kazi kilitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kualika watanzania wote kuwasilisha maoni na mapendekezo kuhusu masuala hayo tisa (9), kwa njia mbalimbali ikiwemo, “WhatsApp” kupitia namba ya simu ya Katibu, barua pepe [email protected], anuani ya posta ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kuzungumza na wajumbe wa Kikosi Kazi ana kwa ana. 

 Mheshimiwa Rais, wakati wa kutekeleza majukumu yake, Kikosi Kazi kimechambua maoni na mapendekezo 98, yaliyotolewa na washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa uliofanyika tarehe 15-17 Desemba 2021 Dodoma. Vilevile, ilichambua maoni ya maandishi na kuzungumza yaliyotolewa na wadau mbalimbali waliowasilisha maoni na mapendekezo kwa Kikosi Kazi. Wadau waliowasilisha maoni kwa Kikosi walitoka katika makundi yafuatayo:

  1. Viongozi wa Serikali waliopo madarakani na wastaafu;
  2. Watu Mashuhuri;
  3. Taasisi za Serikali;
  4. Taasisi za Dini;
  5. Vyama vya Siasa; 
  6. Makundi ya Kijamii; 
  7. Wanataaluma
  8. Asasi za Kiraia
  9. Wafanyabiashara
  10. Wakulima
  11. Watanzania waishio nje -Diaspora

 Mheshimiwa RaisKikosi Kazi kimepata bahati ya kukutana na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara tatu. Tarehe 12 Machi 2022, tarehe 21 Machi 2022 na tarehe 30 Mei, 2022. Vilevile kimekutana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mara tatu tarehe 10 Januari 2022, tarehe 20 Aprili 2022 na tarehe 15 Agosti 2022. Hivyo, wajumbe wa Kikosi Kazi tunawashukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kwa fursa mlizotupa za kukutana nanyi pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kitaifa. Fursa hizi mlizotupatia ni moja tu kati ya mambo mengi yanayodhihirisha utashi wenu wa kisiasa kwa kazi tunayofanya na maboresho ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa katika nchi yetu. 

 Mheshimiwa Rais, wajumbe wa Kikosi Kazi tunakushukuru kwa usimamizi na mwongozo wako thabiti katika kutekeleza majukumu yetu ya Kikosi Kazi. Tangu tuanze kazi tarehe 10 Januari 2022, hatujawahi kusitisha kazi yetu kwa sababu ya kukosa rasilimali au vitendea kazi, changamoto yoyote ilipotokea umekuwa ukitoa maelekezo ifanyiwe kazi mapema iwezekanavyo, ili kazi isisimame, iendelee kama kauli mbiu ya Taifa letu uliyoiasisi inavyosema.

 MAPENDEKEZO YA KIKOSI KAZI

 Mheshimiwa Raisbaada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi kumi (10), sasa tunayo heshima kuwasilisha kwako, matokeo ya kazi uliyotupatia. Ripoti ya Kikosi Kazi tunayowasilisha ina sura kumi na moja ambapo kila sura imeeleza suala husika, maoni ya wadau, uzoefu nchi nyingine, uchambuzi na mapendekezo ya Kikosi Kazi. 

Mheshimiwa Rais, ili kuokoa mda, ninawasilisha mapendekezo tu. Nayo ni haya yafuatayo:

 1.    Kuhusu mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa Katiba na Sheria;
  2. Mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote;
  3. yafanyike marekebisho ya Sheria, ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi. Sheria hizo ni pamoja Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi Sura ya 322 na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2019.

2.    Kuhusu demokrasia ndani ya vyama vya siasa

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa: 

Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili:

  1. kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa linaloundwa na vyama vyenyewe,  mamlaka ya kushughulikia suala la uvunjifu wa maadili ya Vyama vya Siasa kupitia Kamati yake ya Maadili; yaani self-regulation
  2. Msajili wa Vyama vya Siasa aandae mwongozo wa uchaguzi wa ndani ya Vyama vya Siasa;
  3. kuweka masharti kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi vya chama cha siasa isipungue asilimia 40; na
  4. kukitaka kila chama cha siasa kuwa na sera ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika. 

3.   Kuhusu ruzuku kwa vyama vya siasa inayotolewa na Serikali 

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku ya Serikali kwa Vyama vya Siasa uendelee, isipokuwa asilimia 10 ya fedha za ruzuku kwa Vyama vya Siasa zinazotengwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha husika, igawiwe sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili kwa mujibu wa vigezo na masharti yafuatayo: 
  1. chama kiwe na usajili kamili; 
  2. chama kiwe kimefanyiwa uhakiki na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuthibitishwa kwamba, kinakidhi vigezo vya usajili kamili; 
  3. chama kiwe kimeshiriki Uchaguzi Mkuu angalau mara mbili tangu kupata usajili kamili; 
  4. katika mwaka wa fedha uliopita, chama husika kisiwe kimepata Hati Chafu ya Mahesabu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; na
  5. ruzuku itumike kwa shughuli za kuendesha Ofisi ya Makao Makuu, Ofisi Ndogo au Ofisi Kuu ya Makao Makuu ya chama cha siasa husika.
  1. Sheria ya Vyama vya Siasa itamke kuwa, asilimia ishirini (20%) ya fedha za ruzuku kwa Vyama vya Siasa inayotolewa na Serikali katika mwaka wa fedha, igawiwe kwa Vyama vya Siasa vyenye Madiwani wa kuchaguliwa katika kata, kwa mujibu wa uwiano wa idadi ya Madiwani hao ambao kila chama kinao, kwani kwa sasa sheria haijatamka kiwango chochote bali imempa mamlaka Waziri Mwenye dhamana kuamua; na
  2. Serikali iongeze fedha za bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa, ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwemo jukumu linalopendekezwa la kusimamia Maadili ya Vyama vya Siasa.

4.    Kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. tume ya Taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya Serikali, maoni ya chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote; na
  2. utendaji wa Tume ya Uchaguzi uruhusiwe kuhojiwa kwenye Mahakama ya Juu pale itakapoanzishwa ili kuongeza uwajibikaji wa Tume.

5.    Kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa utaratibu ufuatao utumike kuwapata wajumbe wa tume ya Taifa ya Uchaguzi:

  1. kuwe na Kamati ya Uteuzi ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
  1. Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atakuwa ni Mwenyekiti; 
  2. Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti; 
  3. Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Tanzania Bara; 
  4.  Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Zanzibar;
  5.  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu; na 
  6.  wajumbe wengine wawili watakaoteuliwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupendekezwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika na Chama cha Wanasheria Zanzibar.
  1. angalau wajumbe wawili wa Kamati ya Uteuzi wawe wanawake;
  2. sifa za mtu kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ziainishwe;
  3. nafasi ya mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itangazwe na Mtanzania yeyote mwenye sifa aruhusiwe kuwasilisha maombi kwa Kamati ya Uteuzi ya kuwa mjumbe wa Tume;
  4. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili wa watu waliowasilisha maombi ya kuwa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaostahili kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
  5. Kamati ya Uteuzi itawasilisha kwa Rais majina manne (4) zaidi ya idadi ya nafasi zinazohitajika kujazwa; na
  6. Rais ateue wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi miongoni mwa majina yaliyowasilishwa kwake na Kamati ya Uteuzi.

 6.   Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutohojiwa Mahakamani

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa, matokeo ya uchaguzi wa Rais yahojiwe kwenye Mahakama ya Juu mara itakapoanzishwa.

 7.    Kuhusu watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, weledi, maadili, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao; na
  2. wasimamizi wa uchaguzi watakaokiuka sheria na utaratibu wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria.

8.    Kuhusu bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipewe fedha zilizotengwa katika bajeti kwa wakati, hata baada ya uchaguzi, ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wote.

9.    Kuhusu sheria zinazosimamia masuala ya uchaguzi Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. itungwe sheria ya kusimamia shughuli za Tume ya Taifa Uchaguzi; 
  2.  kuwepo na sheria moja ya uchaguzi itakayotumika kusimamia uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, badala ya kuwa na sheria mbili ambazo ni Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Madiwani Sura 292; na
  3. maafisa wa Tume ya Uchaguzi watakaowaengua wagombea kushiriki katika uchaguzi bila kuzingatia sheria na weledi  uchaguzi wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

10.  Kuhusu matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. matumizi ya TEHAMA katika mchakato wa uchaguzi yahamasishwe na kiwango chake kiongezwe;  
  2. zitayarishwe Kanuni mahsusi za kuratibu matumizi ya TEHAMA kwenye mchakato wa uchaguzi; na
  3. kuwepo na uwekezaji wa kutosha kwenye miundombinu ya TEHAMA na usalama wake wakati wa uchaguzi.

 11.  Kuhusu ushiriki wa Wanawake katika Siasa, Demokrasia na Uongozi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa: 

  1. Sheria ya Vyama vya Siasa irekebishwe ili:
  1. kuweka sharti la kila chama cha siasa kuwa na sera ya jinsia na ujumuishi wa makundi maalum katika jamii;
  2. kuweka sharti la kisheria kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi ndani ya chama cha siasa isipungue asilimia 40;
  3. Kanuni za Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa za Mwaka 2019 ziwe na vigezo vya ufuatiliaji ili kupima utekelezaji wa Sheria, katiba na kanuni za vyama vya siasa, kuhusu masuala ya jinsia na ujumuishaji wa makundi maalum ya jamii katika chama na uchaguzi; na
  1. katiba za vyama ziwe na Ibara zinazoshughulikia masuala ya ukatili wa jinsia ikiwemo udhalilishaji wa wanawake;
  2. kila chama cha siasa kiwe na programu maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake kugombea ubunge, uwakilishi na udiwani, ikiwemo kuwa na mipango na mikakati ya kufikia usawa wa kijinsia;
  3. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kila chama cha siasa kiwe na dawati la jinsia litakalofanyia kazi masuala ya jinsia ndani ya vyama vya siasa; 
  4. utaratibu wa kuwa na viti maalum vya Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wanawake uendelee, isipokuwa sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka kumi kwa mtu kuwa Mbunge, Mwakilishi au Diwani wa viti maalum vya wanawake. Uwakilishi huu uwe ni njia ya kupata uzoefu na kisha kupisha wanawake wengine wenye nia ya kuongeza ujuzi wa masuala ya siasa na uongozi. 
  5. kuwepo na mwongozo wa kisheria wa uteuzi wa wagombea na uchaguzi wa viongozi ndani ya Vyama vya Siasa, ikiwemo wabunge wa viti maalum ili kusaidia uteuzi na uchaguzi huo kuwa wa haki, uwazi na huru;
  6. kila chama cha Siasa kiweke mkakati wa kuongeza idadi ya wanawake wanaogombea katika majimbo na kata za uchaguzi; na
  7. kwa kuwa idadi ya wanawake ni ndogo katika Baraza la Vyama vya Siasa aongezwe mjumbe mmoja mwanamke kutoka kila chama cha siasa kuwa mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa; na
  8. Wabunge wa Viti Maalum vya Wanawake waitwe Wabunge wa Taifa na Madiwani, waitwe Madiwani wa Wilaya, kwa sababu wabunge hao wanatokana na kura za nchi nzima na Madiwani wanatokana na kura za Wilaya. Aidha, Sheria ya Mfuko wa Jimbo ifanyiwe marekebisho ili itambue Wabunge wa Taifa kuwa miongoni mwa Wabunge wanaofaidika na fedha za Mfuko huo.

 12. Kuhusu ushiriki wa Watu Wenye Ulemavu katika Siasa, Demokrasia na Uongozi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa: 

  1. sheria zisizozingatia ujumuishwaji wa Watu Wenye Ulemavu na zile zinazokwamisha ushiriki wao katika siasa, demokrasia na uongozi ndani ya vyama siasa zifanyiwe maboresho;
  2. Vyama vya Siasa viweke mazingira rafiki yatakayowawezesha Watu Wenye Ulemavu kufanya shughuli za kisiasa bila vikwazo;
  3. kila chama cha siasa kianzishe dawati la kushughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu;
  4. kuwepo na nafasi maalum kwa Watu Wenye Ulemavu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Madiwani. Viti vya uwakilishi wa Watu Wenye Ulemavu Bungeni viwe katika uwiano utakaozingatia jinsi. Sula hili lifanyiwe kazi katika mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ili lifanyike kwa ufanisi. Hata hivyo, kwa kuanzia kila chama cha siasa kitumie utaratibu wa sasa wa viti maalum vya Wanawake kujumuisha Watu Wenye Ulemavu;
  5. Sheria ya Vyama vya Siasa irekebishwe ili:
  1. iweke sharti kwamba chama cha siasa kiwe na nakala ya Katiba na Kanuni zilizo katika maandishi ya breli (nukta nundu). Aidha, katika mkutano mkuu wa chama taifa, awepo mkalimani wa lugha za alama;
  2. katazo la ubaguzi kwa Watu Wenye Ulemavu katika vyama vya siasa lililopo katika kifungu cha 9(1)(c) cha sheria ya vyama vya siasa liwahusu pia viongozi wa vyama vya siasa; na
  3. katiba ya chama cha siasa iwe na ibara inayokitaka chama husika kiwe na programu za kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika michakato ya kisiasa, demokrasia na uongozi ndani na nje ya chama.
  1. zitungwe Kanuni za utekelezaji wa Kifungu cha 6A (2) cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinachoelekeza chama cha siasa kuzingatia suala la ujumuishwaji wa Watu Wenye Ulemavu katika masuala ya vyama vya siasa na demokrasia; na
  2. vyombo vya habari viandae vipindi maalum vya elimu ya uraia vinavyoeleza haki na mahitaji ya Watu Wenye Ulemavu.

13. Kuhusu ushiriki wa vijana katika Siasa, Demokrasia na Uongozi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa, juhudi zinazofanywa na Serikali kuhusu ushiriki wa vijana katika siasa, demokrasia, uongozi, uchumi, ulinzi na usalama wa nchi yetu ziendelee na mikakati mipya ibuniwe ili kuongeza ufanisi na tija.

14.  Kuhusu elimu ya uraia

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. Serikali iandae mwongozo wa kitaifa, mpango kazi na mikakati ya utoaji elimu ya uraia, ili utoaji wa elimu hiyo uzingatie vipaumbele vya taifa na kuwa na uelewa wa pamoja wa walengwa;
  2. elimu ya uraia ikiwemo elimu ya mpiga kura ifundishwe katika ngazi zote za mfumo wa elimu kuanzia shule za awali mpaka katika vyuo vya elimu ya juu. Aidha, mtaala wa elimu ujumuishe masuala ya elimu ya uraia; 
  3. Serikali na wadau wengine waongeze kiwango cha ufadhili katika kutoa elimu ya uraia ikiwemo elimu ya mpiga kura, ili kukabiliana na upungufu wa rasilimali fedha, watu na vifaa katika kutoa elimu hiyo;
  4. elimu ya mpiga kura itolewe kipindi chote siyo cha uchaguzi pekee, ili kuongeza muda wa kutoa elimu hiyo kuwezesha kuwafikia walengwa wengi zaidi; na
  5. uratibu na ufuatiliaji wa elimu ya uraia unaofanywa na taasisi mbalimbali kwa mujibu wa sheria uendelee, isipokuwa ufanywe katika hali isiyokwamisha juhudi za kuwafikia watanzania wengi kupata elimu hiyo.

15. Kuhusu suala la kuzuia na kupambana na Rushwa katika Siasa na Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

    1. suala la rushwa litamkwe katika Katiba, ili wananchi watambue kuwa vitendo vya rushwa havitavumiliwa wala kuonewa muhali. Pendekezo hili lifanyiwe kazi katika mchakato wa kupata Katiba Mpya ili lifanyike kwa ufanisi;
    2. Sheria ya vyama vya Siasa Sura 258 irekebishwe ili:
  1. kuweka sharti kwamba, katiba ya chama cha siasa iwe na adhabu ya kumwondoa katika mchakato wa uchaguzi, mtia nia au mgombea aliyedhaminiwa na chama, endapo atathibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa;
  2. Msajili wa Vyama vya Siasa apewe mamlaka ya kuandaa mwongozo wa kufuatilia mchakato wa uteuzi wa wagombea na uchaguzi wa viongozi, ndani ya Vyama vya Siasa; na
  3. kukitaka kila chama cha siasa kuwa na Kanuni za Maadili, zitakazodhibiti ukiukwaji wa maadili ndani ya chama, ikiwemo mwanachama kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kanuni hizo ziweke utaratibu wa kushughulikia ukiukwaji wa maadili na adhabu, ikiwemo onyo, karipio, faini, kuvuliwa ujumbe wa kikao husika, kutoruhusiwa kugombea uongozi ndani ya miaka kumi tangu alipopatikana na hatia, kusimamishwa au kufukuzwa uanachama.
    1. Sheria ya Gharama za Uchaguzi irekebishwe ili:
  1. kutoa adhabu kwa mgombea atakayeshindwa kufanya marejesho ya gharama za uchaguzi badala ya kukiadhibu chama cha siasa;
  2. vitendo vinavyokatazwa katika sheria hiyo kuwa na sifa ya kuwa kosa la jinai;
  3. nyaraka za uthibitisho wa matumizi ya gharama za uchaguzi zibaki katika chama cha siasa husika badala ya kuwasilishwa kwa Msajili wa vyama vya siasa

Read More
PAMJ

VIONGOZI PAMOJA NA BAADHI YA WANACHAMA WA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS) PAMOJA NA CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR (ZLS) WAKIWA KWENYE KIKAO NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Kikao na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokwenda pamoja na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Masoud Rukazibwa akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokwenda pamoja na ujumbe wake Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati alipokutana na Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia Hati ya Kiwanja kilichopo Arusha kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi zao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Agosti 14, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Wanasheria Wanawake wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) pamoja na Wanasheria Wanawake wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Agosti 14, 2023.

Read More
MAH

YALIYOJILI KATIKA HUKUMU YA KESI YA KUPINGA MKATABA WA UWEKEZAJI WA BANDARI 10 AUGUST 2023

No 1

Majaji wote watatu wameingia muda huu saa 3:42.

Majaji;

Mhe. Ndunguru 

Mhe. Ismail 

Mhe. Kagomba

Wakili wa serikali anatambulisha mawakili wa pande zote mbili. Na wote wako tayari kupokea hukumu.

Mahakama imetulia kwa ukimya mkuu.

Majaji wanazungumza kidogo, Mhe. Ismail na Ndunguru.

Kisha, Jaji Kagomba na Ndunguru pia wanazungumza kidogo.

Wanaendelea kuandika.

Karani wa Mahakama leo ni MAPUNDA

Majaji wanasema wako tayari kusoma hukumu na kwamba itasomwa kwa kiswahili

Jaji Ndunguru: Kabla ya kuanza usililizwaji huo, Mawakili wa pande zote mbili waliunda kwanza viini vya kuamuliwa (Issues) pamoja na kiini kimoja ambacho kiliongezwa na Mahakama.

Jaji Ndunguru: Wajibu Maombi wameeleza kwamba Bunge lilitoa taarifa kwa umma ili kupata maoni, na wamesema kwamba watu 72 walijitokeza kutoa maombi.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa njia ya mdomo, mawakili wa pande zote mbili wakiwakilisha wadaawa.

Jaji Ndunguru anaanza kusoma hukumu.

HUKUMU YA MAHAKAMA 

Katika lalamiko hili waleta maombi wanne ni raia wa Tanzania wameleta maombi haya dhidi ya Mkataba wa Tanzania na Emirati ya Dubai.

 No 2

Kesi Bandari

Jaji Ndunguru: Wajibu maombi wamejenga hoja kwamba suala hilo ni la ndani ya Bunge.

Mahakama inatambua kuwa Ibara ya 63(3)(e) na Kanuni ya 108(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

Jaji Ndunguru: Kukosekana kwa Viambatanisho muhimu kama Mkataba wa IGA katika Tangazo hilo, na kutokea kwa watu 72 tu, ndiyo hoja ya Waleta Maombi.

Jaji Ndunguru: Viini hivyo ni pamoja na kuhoji iwapo Ibara kadhaa ya IGA zinakiuka Ubara ya 1, 8, 28(1)(3) za Katiba ya Tanzania.Pia, kiini kingine kilihoji iwapo IGA ni mkataba

Jaji Ndunguru: Kwa hoja tajwa hapo juu mahakama hii inatupilia mbali hoja za waleta maombi.

Anamaliza kusoma hukumu hiyo .

Watu wanasimama majaji wanatoka.

Jaji Ndunguru: Uandishi bora wa vifungu vya IGA unaweza kurekebisha Vifungu hivyo na kuondoa dosari hii.

Tunashangaa kwamba IGA itaongozwa na sheria za nchi, na mikataba ya miradi itaongozwa na sheria za ndani lakini migogoro yake itatatuliwa nje ya nchi.

 No 3.

KESI YA BANDARI.

Jaji Ndunguru: Baada ya kupitia hoja za pande zote, tunakubaliana na hoja za wajibu maombi kwamba Bunge halitakiwi kuingiliwa katika majukumu yake..

Read More
SAMI

NI UPI WAJIBU WA SERIKALI YA TANZANIA KWA WANANCHI WAKE KIKATIBA? SWALI LA MDAU KATIKA MJADALA WA KATIBA YA WATU

[10:41, 03/08/2023] A: Nimekuwa nawaza sana kuhusu katiba ya nchi ya kijamhuri. Kwamba inapoanza kuundwa huwa kuna misingi ipi inawekwa?

Napenda kuuliza 

Ni upi wajibu wa serikali ya Tanzania kwa wananchi wake kikatiba?

Maana kwenye katiba yetu ya sasa hakuna sehemu imeeleza wajibu wa serikali wa moja kwa moja kwa wananchi.

Ndio maana kuna mambo yanafanyika kwa utashi wa kiongozi tu na siyo kuongozwa na katiba. 

Kulingana na katiba ya sasa serikali haina responsibilities zozote kwa wananchi, yaani inafanya mambo yote kama msaada tu, huku serikali ikiweka masharti magumu kwa wananchi na kuwabana walipe kodi.

Yaani wananchi wanalazimishwa kulipa kodi huku serikali haina responsibility yoyote kikatiba

[12:09, 03/08/2023] T: Mimi naanza kwa kwa maana ya maneno hayo mawili WAJIBU na SERIKALI kwanza

[12:09, 03/08/2023] T: Neno “WAJIBU” linamaanisha majukumu au wajibu ambao mtu au taasisi inapaswa kutekeleza. Ni wajibu ambao mtu au kikundi hakiwezi kuepuka au kubadilisha. Wajibu hufafanua jukumu la kufanya jambo fulani au kutimiza majukumu ya kijamii, kisheria, au kimaadili.

Kwa mfano, wajibu wa raia kwa nchi yao unaweza kujumuisha kufuata sheria, kuheshimu haki za wengine, na kuchangia kwa maendeleo ya taifa. Vilevile, wazazi wana wajibu wa kulea na kutoa malezi bora kwa watoto wao. Katika sehemu za kazi, wafanyakazi wana wajibu wa kutimiza majukumu yao kazini kwa uaminifu na uadilifu.

Ni muhimu kutambua kuwa wajibu na haki ni vitu viwili vinavyohusiana. Kwa mfano, haki za raia huenda zikajumuisha haki ya kupiga kura, uhuru wa kujieleza, na haki ya kufanya maamuzi ya kibinaf…

[12:13, 03/08/2023] T: SERIKALI ni mfumo au taasisi inayoshikilia mamlaka ya utawala na udhibiti juu ya eneo fulani au taifa. Ni chombo cha utendaji kilichowekwa rasmi ambacho kinashughulikia masuala ya umma na kusimamia uendeshaji wa nchi.

Kazi kuu za serikali ni pamoja na:

1. Kutoa Huduma za Umma: Serikali inatoa huduma za msingi kwa wananchi wake, kama vile huduma za afya, elimu, maji, miundombinu, usafiri, ulinzi wa usalama, na huduma za kijamii.

2. Kusimamia Sheria na Utaratibu: Serikali ina jukumu la kuandaa sheria, kuzitekeleza na kusimamia utekelezaji wa sheria hizo. Inahakikisha kuwa watu wanatii sheria na wanapata haki sawa mbele ya sheria.

3. Kulinda na Kusimamia Rasilimali za Nchi: Serikali inasimamia na kulinda rasilimali za nchi kama vile ardhi, madini, maliasili, na mali zingine za umma kwa faida ya wananchi wote.

4. Kukusanya Mapato na Kutoa Matumizi: Serikali hukusanya mapato kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara kupitia kodi na tozo mbalimbali. Mapato haya hutumika kwa kugharamia huduma za umma na miradi ya maendeleo.

5. Kuwakilisha Nchi Kimataifa: Serikali inawakilisha nchi yake katika jumuiya za kimataifa, mikutano, na mashirika ya kimataifa. Inashiriki katika majadiliano na kufanya maamuzi yanayohusu masuala ya kimataifa.

Serikali inaweza kuwa ya aina mbalimbali kulingana na muundo wake. Kuna serikali za kidemokrasia ambazo zinahusisha uwakilishi wa wananchi kupitia chaguzi na uhuru wa kujieleza. Pia, kuna serikali za kidikteta ambazo nguvu zote zinakaa kwa kiongozi mmoja au chama kimoja. Baadhi ya serikali zinaweza kuwa za shirikishi, kikoloni, au za kifalme, kulingana na mifumo ya kisiasa na tamaduni za nchi husika.

[12:19, 03/08/2023] T: KATIBA ya nchi ni msingi wa sheria na taratibu za nchi ambazo huongoza uendeshaji wa serikali, haki na wajibu wa raia, na muundo wa taasisi za serikali. Katiba inaweza kueleza wazi misingi na wajibu wa serikali kwa wananchi wake, lakini inaweza pia kutafsiriwa na kutekelezwa tofauti na serikali inayoongoza.

Kwa ujumla, katiba inaweza kutoa maelezo ya wajibu wa serikali kwa wananchi wake. Hii inaweza kujumuisha mambo kama haki za raia, huduma za msingi za kijamii na kiuchumi, ulinzi wa haki za kibinadamu, na kujitolea kwa maendeleo ya nchi.

Kwa kuwa una wasiwasi juu ya jinsi serikali inavyofanya kazi na kutafsiri wajibu wake kwa wananchi, ni muhimu kufahamu na kusoma kwa kina katiba ya nchi  ili kuelewa wajibu uliowekwa rasmi kwa serikali. Pia, inaweza kuwa ni wakati muafaka kwa wananchi na wadau wengine kujadili na kuhoji maudhui na utekelezaji wa katiba ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika uongozi na utawala wa nchi.

Kuhusu masuala ya kodi na majukumu ya serikali, katika nchi nyingi, wananchi hulipa kodi ili kufadhili shughuli za serikali na huduma za umma. Serikali inawajibika kwa kutumia mapato hayo kwa manufaa ya wananchi kwa kutekeleza majukumu yake, kama vile kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu, ulinzi wa usalama, na kadhalika. Hivyo, majukumu ya serikali kwa wananchi yanapaswa kujumuisha utoaji wa huduma bora na ulinzi wa maslahi ya umma.

Kama mwananchi, una haki ya kufuatilia jinsi serikali inavyotekeleza majukumu yake na kuhoji uzingatiaji wa sheria na taratibu. Pia, ni muhimu kushiriki kikamilifu katika michakato ya kidemokrasia, kama vile uchaguzi na mchakato wa kutunga au kurekebisha katiba, ili kusaidia kuunda serikali inayowajibika na inayotii matakwa ya wananchi.

[12:44, 03/08/2023] b: Nchini Tanzania, wajibu wa serikali kwa wananchi wake unaweza kutofautiana kulingana na katiba na sheria zinazotumika. Wajibu wa serikali mara nyingi unajumuisha majukumu yafuatayo:

1. Kulinda Haki za Raia: Serikali inapaswa kulinda haki za kibinadamu za raia wake kama vile haki ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuabudu, haki ya usalama wa mtu na mali, na haki ya kupata haki sawa mbele ya sheria.

2. Kutoa Huduma za Msingi: Serikali ina wajibu wa kutoa huduma za msingi za kijamii kwa wananchi wake, kama vile huduma za afya, elimu, maji safi na salama, na malazi bora.

3. Kulinda Usalama wa Taifa: Serikali ina jukumu la kulinda usalama na mipaka ya nchi na kuhakikisha ulinzi wa raia wake kutokana na vitisho vya ndani na nje.

4. Kusimamia Sheria na Haki: Serikali …

[12:51, 03/08/2023] b: Katika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, kama ilivyo katika katiba nyingine, serikali ina jukumu la kutoa huduma na kulinda maslahi ya wananchi wake. Ingawa katiba inaweza kutofautiana kwa kila nchi, kwa ujumla, inaweka msingi wa majukumu na wajibu wa serikali.

Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, inayoitwa “Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” imekuwa ikifanyiwa marekebisho kadhaa, na nafasi ya Katiba inayotumika inaweza kuwa na mabadiliko kadiri miaka inavyosonga mbele.

Katika Katiba, majukumu ya serikali yanaweza kujumuisha mambo kama vile:

1. Kutoa huduma za umma kama vile elimu, afya, maji, umeme, na miundombinu.

2. Kulinda haki na uhuru wa wananchi, ikiwa ni pamoja na haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

3. Kulinda usalama wa nchi na mipaka yake dhidi ya vitisho vya ndani na nje.

4. Kuandaa na kusimamia sheria za nchi na kuhakikisha zinatekelezwa kwa haki na usawa.

5. Kusimamia uchumi na maendeleo ya nchi ili kuboresha maisha ya wananchi.

6. Kulinda na kuhifadhi maliasili na mazingira ya nchi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Ingawa majukumu haya yanaweza kufahamika katika katiba, utekelezaji wake unaweza kuwa changamoto kutokana na mambo mengi, kama vile rasilimali, miundombinu, uongozi, na mambo ya kisiasa. Pia, mchakato wa kutekeleza majukumu ya serikali unaweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii katika nchi husika.

Ni muhimu kwa wananchi kufahamu katiba ya nchi yao na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa kufanya ushiriki wa kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia, kuhoji viongozi, na kudai uwajibikaji kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa taifa.

[13:30, 03/08/2023] T: Hoja yako @A “Ndio maana kuna mambo yanafanyika kwa utashi wa kiongozi tu na siyo kuongozwa na katiba.”Kuna ukweli katika hoja yako kwamba katika baadhi ya mazingira, mambo yanaweza kufanyika kwa utashi wa kiongozi au kundi la watu wenye mamlaka, badala ya kufuata misingi ya katiba au sheria. Na hii sasa inaweza kusababisha matatizo kadhaa katika utawala na uongozi wa nchi. Mfano

1. Ukosefu wa Uwajibikaji: 

Wakati maamuzi na vitendo vya viongozi vinapokwenda kinyume na katiba au sheria, huwa vigumu kwa wananchi kuwajibisha viongozi hao kwa sababu wanaonekana kuwa juu ya sheria.

2. Ukiukwaji wa Haki za Binadamu: 

Serikali inayotenda kwa utashi wa kiongozi inaweza kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari, kuwakandamiza wapinzani, na kukiuka haki za kiraia na kisiasa za raia.

3. Rasilimali na Mipango Isiyo na Ufanisi: 

Maamuzi ya kibinafsi ya viongozi yanaweza kusababisha matumizi mabaya ya rasilimali za nchi na kutekelezwa kwa mipango isiyotekelezeka au isiyolingana na mahitaji ya wananchi.

4. Kupotosha Maendeleo ya Nchi: Maamuzi yasiyoendana na katiba yanaweza kusababisha kutoweka kwa dira na mwelekeo wa maendeleo ya nchi, na badala yake kusababisha maslahi ya kibinafsi au ya wachache.

Kuwa na katiba madhubuti na kuhakikisha utawala wa sheria ni muhimu kwa kuweka vizuizi na kuwajibisha viongozi, kuhakikisha uwiano na usawa katika maendeleo ya nchi, na kulinda haki na uhuru wa raia. Wananchi wanapaswa kuwa na sauti na nafasi katika kushiriki katika mchakato wa kisiasa na kudai utawala bora ili kuhakikisha kuwa serikali inahudumia maslahi ya umma.

[13:39, 03/08/2023] A: Mtaalam, ikikupendeza tupia ibara na vifungu vyake ili kutoa uelewa zaidi na mpana wa hoja na mashaka ya wadau kwa ujumla wake.

[13:42, 03/08/2023] W: 🙏🏽

[13:46, 03/08/2023] T: Shukrani sana mdau..kwavile wataalamu wa sheria na wale wanohusika na wizara huusika wako hapa tuwaombe wasikae kimya pale panapoonekana pana hitajika utaalamu wao wa sheria na uhakika.Lakini tunajitahidi kupata vifungu na ibara zinazoainisha hofu ya mdau juu ya wajibu wa serikali ya Tanzania kwa wananchi wake kikatiba

[14:06, 03/08/2023] A: Asante sana!

[15:20, 03/08/2023] T: Ibara na vifungu katika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 huenda vikawa vingi na virefu, hivyo nitawasilisha baadhi ya ibara zinazoangazia majukumu ya serikali na wajibu wake kwa wananchi. 

1. Ibara ya 3 – Madaraka ya Umma na Umiliki wa Taifa:

o Kifungu cha 9: Kinathibitisha kuwa madaraka yote ya nchi hutoka kwa wananchi na kwamba wananchi wana haki ya kushiriki katika kuamua masuala ya nchi.

2. Ibara ya 9 – Muundo wa Serikali:

o Kifungu cha 25: Kinaeleza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na mihimili mitatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Mitaa, na Mahakama.

3. Ibara ya 13 – Serikali za Mitaa:

o Kifungu cha 145: Kinasema kuwa serikali za mitaa zitakuwa na madaraka ya kutumika kwa ajili ya masuala ya kienyeji na utawala wa maeneo yao.

4. Ibara ya 26 – Haki na Wajibu wa Raia:

o Kifungu cha 29: Kinasema kuwa kila mtu anapaswa kutii sheria za nchi.

o Kifungu cha 30: Kinafafanua haki na uhuru wa kimsingi wa raia, pamoja na uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa na kupokea habari, na uhuru wa kukusanyika na kujumuika.

o Kifungu cha 31: Kinafafanua wajibu wa kila raia kuheshimu haki na uhuru wa wengine.

5. Ibara ya 146 – Majukumu ya Serikali za Mitaa:

o Kifungu cha 152: Kinasema kuwa serikali za mitaa zina jukumu la kufanya maamuzi na kutoa huduma kwa wananchi kulingana na sheria na taratibu.

[15:34, 03/08/2023] T: baadhi ya ibara na vifungu vingine vinavyohusiana na majukumu na wajibu wa serikali katika Katiba ya Tanzania ya 1977:

6. Ibara ya 9A – Ulinzi wa Rasilimali za Nchi:

o Kifungu cha 26A: Kinasema kuwa serikali itahakikisha rasilimali za nchi, ikiwa ni pamoja na ardhi, maji, madini, misitu, na mazingira, zinatumika kwa faida ya wananchi na kuhifadhiwa kwa vizazi vijavyo.

7. Ibara ya 9B – Maendeleo Endelevu na Kusawazisha Maendeleo:

o Kifungu cha 26B: Kinasema kuwa serikali itachukua hatua za kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo, na kuhakikisha maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa yanafanyika kwa usawa na haki.

8. Ibara ya 9C – Ustawi wa Jamii na Huduma za Jamii:

o Kifungu cha 26C: Kinasema kuwa serikali itatekeleza sera na mipango ya kuendeleza ustawi wa jamii na kutoa huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, makazi, na mazingira bora.

9. Ibara ya 9D – Utunzaji wa Mazingira na Hifadhi ya Maliasili:

o Kifungu cha 26D: Kinasema kuwa serikali itaweka mikakati ya kutunza mazingira, kuhifadhi maliasili, na kupambana na uharibifu wa mazingira.

[18:29, 03/08/2023] M: Katiba haijaishia hapo ukisoma

10. Ibara ya 9E – Kufanikisha Uchumi wa Taifa:

o Kifungu cha 26E: Kinasema kuwa serikali itaendeleza uchumi wa taifa kwa kukuza uzalishaji, biashara, ajira, na kuboresha maisha ya wananchi.

11. Ibara ya 9F – Kuhakikisha Uadilifu wa Rasilimali za Taifa:

o Kifungu cha 26F: Kinasema kuwa serikali itahakikisha kuwa matumizi ya rasilimali za taifa yanaendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji, na kuondoa ubadhirifu na ufisadi.

12. Ibara ya 9G – Uwiano wa Maendeleo Kitaifa:

o Kifungu cha 26G: Kinasema kuwa serikali itahakikisha kuwa maendeleo yanafanyika katika maeneo yote ya taifa kwa usawa, na kuzingatia haki na usawa wa kijamii.

13. Ibara ya 9H – Kusimamia Uchumi wa Nchi:

o Kifungu cha 26H: Kinasema kuwa serikali itasimamia uchumi wa taifa kwa kutoa mwelekeo na kusimamia sera za uchumi.

14. Ibara ya 9I – Kuendeleza Sekta ya Kilimo:

o Kifungu cha 26I: Kinasema kuwa serikali itachukua hatua za kuendeleza sekta ya kilimo na kusaidia wakulima kuboresha uzalishaji na kipato.

15. Ibara ya 9J – Kuhakikisha Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Watu:

o Kifungu cha 26J: Kinasema kuwa serikali itatekeleza sera na mipango ya kuendeleza ustawi wa jamii, kupunguza umaskini, na kuboresha maisha ya wananchi.

16. Ibara ya 9K – Kuendeleza Elimu:

o Kifungu cha 26K: Kinasema kuwa serikali itaweka sera na kutekeleza mipango ya kuendeleza sekta ya elimu na kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa wananchi wote.

17. Ibara ya 9L – Kulinda na Kuendeleza Afya:

o Kifungu cha 26L: Kinasema kuwa serikali itatekeleza sera na mipango ya kuboresha huduma za afya na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

18. Ibara ya 9M – Kuhakikisha Ustawi wa Watoto, Wanawake, na Watu wenye Ulemavu:

o Kifungu cha 26M: Kinasema kuwa serikali itachukua hatua za kulinda na kuendeleza ustawi wa watoto, wanawake, na watu wenye ulemavu.

Hizi ni baadhi tu ya ibara na vifungu katika Katiba ya Tanzania ya 1977 vinavyojumuisha majukumu na wajibu wa serikali katika kuwahudumia wananchi wake. Katiba hii ni kielelezo muhimu cha mfumo wa kisheria na utawala wa nchi na inabeba misingi na taratibu ambazo zinasimamia shughuli za kila siku za serikali na wananchi. Kuzingatia na kutekeleza matakwa ya Katiba ni msingi muhimu wa kujenga nchi imara na yenye maendeleo kwa ustawi wa wote.

Read More
GRP

ACT -WAZALENDO ZANZIBAR YAFURAHISHWA ZOEZI LA UHAKIKI VYAMA VYA SIASA

Baadhi ya wataalam kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha ACT – Wazalendo Zanzibar mara baada ya kumaliza zoezi la uhakiki wa chama hicho katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu zilizopo Vuga Mjini Magharibi.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo Kazi (wapili kushoto) akisoma moja ya nyaraka za chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembelea katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Zanzibar zilizopo Vuga mkoa wa Mjii Magharibi Zanzibar  tarehe 09 Agosti, 2023. Wengine ni viongozi wa chama hicho Zanzibar na kushoto kwake ni Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bibi. Grace Mushi.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo akionyesha Ilani ya Uchaguzi ya chama cha Alliance for Change and transparency (ACT – Wazalendo)  mahususi kwa ajili ya upande wa SMZ wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama walipotembelea katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Zanzibar zilizopo Vuga mkoa wa Mjii Magharibi Zanzibar tarehe 09 Agosti, 2023. Kushoto ni Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bibi. Grace Mushi.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulikia Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo pamoja na Afisa Sheria toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bibi. Grace Mushi wakikagua taarifa za fedha za ACT – Wazalendo ikiwa ni sehemu ya zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa lililoanza terehe 09 Agosti, 2023 visiwani Zanzibar. Zoezi la uhakiki linafanyika visiwani humo baada ya kuhitimishwa katika Ofisi za vyama hivyo zilizoko upande wa Tanzania Bara kwa lengo la kutathmini hali ya utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria ya gharama za uchaguzi.

Read More
MMA

“UKABILIANAJI NA ‘SEXTORTION’ KATIKA VYUMBA VYA HABARI: WITO WA KUSIMAMA DHIDI YA GBV NA KUIMARISHA KUJIAMINI KWA WAANDISHI WA HABARI – DKT. ANNA HENGA”

“Ukabilianaji na ‘Sextortion’ katika Vyumba vya Habari: Kuongeza Ujasiri na Usawa kwa Waandishi wa Habari Wanawake – Hotuba ya Dkt. Anna Henga katika Mkutano wa WAN-IFRA Tanzania”

Katika hotuba ya Dkt. Anna Henga wakati wa mkutano wa kujenga ujuzi na mtandao wa wafanyakazi wa zamani wa Women in News – WAN-IFRA Tanzania tarehe 28 Julai 2023 uliofanyika katika Hoteli ya Giraffe Beach jijini Dar es Salaam, alizungumzia suala la “sextortion” ambalo linawakumba waandishi wa habari katika vyumba vya habari. 

Waandishi hawa wanadaiwa kushurutishwa kutoa miili yao ili kupata nafasi za kazi au vyeo. Baadhi yao wana ujasiri wa kukataa, lakini wengine wanajikuta wakiingia katika mtego wa ukatili unaotokana na jinsia (GBV) ambao pia unaathiri sana njia zao za kazi na kujiamini kwao.

“Sextortion” ni aina ya ukatili unaofanyika kwa kuwatishia au kuwahadaa waandishi wa habari, hasa wanawake, kwa kutumia madaraka yao ili kudhibiti kazi zao kwa kubadilishana na mahitaji ya kimapenzi. 

Tabia hii si tu inakiuka heshima na haki za waathirika, lakini pia inajenga hali ya hofu na udhaifu katika mazingira ya vyumba vya habari.

Dkt. Anna Henga anathaminiwa kwa kuwatambua na kuwatia moyo waandishi wa habari ambao wanakataa kabisa shinikizo hili la “sextortion” na kusimama imara katika kudumisha maadili yao. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa baadhi ya waandishi wanaweza kuingia katika mtego huu wa “sextortion” na kukabiliwa na madhara makubwa katika maisha yao na kujiamini kwao.

Matokeo ya GBV yanazidi kuathiri zaidi ya madhara yanayosababishwa moja kwa moja kwa waathirika. Athari hizi zinaweza kusababisha kikwazo kwa maendeleo ya wanawake katika tasnia ya habari, kusababisha kutopata fursa sawa na mazingira ambayo talanta na uwezo wa kufanya kazi unapuuzwa kutokana na unyanyasaji.

Mkutano kama huu ulioandaliwa na Women in News – WAN-IFRA una jukumu muhimu katika kuongeza uelewa kuhusu masuala haya na kutoa jukwaa ambapo wataalamu wanaweza kushirikiana uzoefu na mikakati ya kukabiliana na GBV na kukuza mazingira salama na yenye usawa kazini.

Kuwashughulikia na kuondoa “sextortion” na aina nyingine za GBV kutoka kwenye vyumba vya habari ni hatua muhimu katika kujenga tasnia ya habari ambayo inathamini maadili, usawa, na usalama wa waandishi wake. Inahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa mashirika, walezi wa sera, na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mazingira ya kazi bila unyanyasaji, ubaguzi, na dhuluma.

Read More
JAMA

MBEYA: FUATILIA MLOLONGO WA KESI YA KUPINGA MKATABA WA BANDARI NA DP WORLD JULAI 28,2023. SEHEMU YA NNE

 KESI YA BANDARI TAREHE 28 JULAI 2023

Majaji wote watatu wanaingia saa 09: 44 asubuhi Tarehe 28 Juli 2023.

MAJAJI WATATU;

1. Hon. Ndunguru

2. Hon. Ismail

3. Hon. Kagomba

Wote wameinama wanaandika

Anasimama wakili wa serikali kutambulisha mawakili wa pande zote.

MAWAKILI WA SERIKALI;

1. Adv. Chang’a

2. Edson Mwaiyunge

3. Alice Mkulu

4. Stanley Kalokola

5. Edwin Lwebilo

MAWAKILI WA WALETA MAOMBI/ WALALAMIKAJI;

1. Mpale Mpoki

2. Boniface MWABUKUSI

3. Philip Mwakilima

4. Livino Ngalimitumba.

WALALAMIKAJI WOTE WAMEFIKA WAPO MAHAKAMANI

1. Alphonce Lusako

2. Emmanuel Chengula

3. Raphael Ngonde

4. Frank Nyarusi.

Anasimama wakili wa serikali na kusema wako tayari kwa ajili ya REJOINDER kama hakuna pingamizi.

Anasimama wakili senior Mpale Mpoki kwamba wako tayari na anaijulisha mahakama kwamba ataanza wakili msomi Boniface Mwabukusi kuwasilisha majibu yake. Atafuata wakili Msomi Livino na atamalizia Wakili Msomi Philip Mwakilima.

Sasa anamkaribisha Wakili  Mwabukusi aendelee.

Anasimama sasa wakili msomi Boniface Mwabukusi ( Mayweather) kwa ajili ya kuwasilisha majibu.

Adv. Mwabukusi: Wakili: Mwabukusi: nitajikita katika issue namba 1, 4 na 5

Wahe. majaji naomba kuelezea kuhusu Capacity to contract. Jambo la msingi sana kwa pande mbili katika mkataba.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walitumia katiba ya Dubai kwamba inaruhusu hiki kilichofanyika, wasilisho hilo sio sahihi kwani ibara ya 120 (1] Cha katiba ya UAE

Kifungu hiki kipo wazi, unapo Montevideo convention, Viena convention. Vinahusu mambo ya kimataifa na sio domestic matter.

Adv. Mwabukusi: Tulitarajia wenzetu watuonyeshe sifa za Dubai kama nchi kimataifa. Mpaka wanafunga mawasilisho yao, hakuna chochote tulichoonyeshwa kinachokidhi matakwa ya viena convention.

Adv. Mwabukusi: Kuhusu hadhi ya ubalozi, hadhi ya nchi m, kama dubai inakiti umoja wa mataifa. Hatujaambiwa sio kwa bahati mbaya, ni kwa sababu havipo.

Waheshimiwa, wenzetu walisema IGA imeeleza kwamba ibara ya 28 ya IGA Imeeleza kuhusu Competence.

Adv. Mwabukusi: In that angle they missed the target.

Wenzetu walisema IGA ni International treaty hivyo inatakiwa kushugulikia kwa sheria za kimataifa sio za ndani. Waheshimiwa majaji.

Adv. Mwabukusi: Kwakuwa wenzetu wameshindwa kuonyesha utu wa kisheria wa DUBAI, hawawezi kutengeneza kitu ambacho kikapata sifa za International teaty.

Adv . Mwabukusi: IGA hii katika ibara 2(1) wenzetu hawajakataa wala kukanusha kwamba huu mkataba wa IGA is a binding agreement unaohusu kuendeleza, kuimarisha, kuendesha na kusimamia bandari za maziwa na bahari.

Adv. Mwabukusi: Ili kuimarisha maeneo ya kiuchumi na shoroba za kibiashara pamoja na miundombinu ambata kuhusiana na Bandari.

Adv. Mwabukusi: Kwa wenzetu kukubali; wamekubali kwamba mkataba huu unagusa Mali asili (Natural resources) za Tanzania ambazo zinagusa sovereign na kunasheria maalumu ziinazolinda permanent sovereign kwenye Natural resources.

Adv.Mwabukusi: Wenzetu hawajapingana na mawasilisho yangu ya sheria za Rasilimali Na.5 ya mwaka 2017 ambayo inatoa sovereignty kwa Watanzania katka rasilimali zao.

Adv. Mwabukusi: Ili kuhakikisha ulinzi wa Rasilimali za nchi. Preamble ya hii sheria ipo wazi ambayo inatoa effect ya article 8(1] 9[f), ya katiba ya Tanzania na wenzetu hawajapinga.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa Sheria hii Na.5 katika Preamble inaakisi ibara 27(1) ya Katiba ya Tanzania kuhusu permanent sovereignty ya Rasilimali zetu.

Waheshimiwa majaji, ukisoma sheria ya maliasili Na 5 na Na 6 za mwaka 2017. Kwenye sheria na 6. Kifungu cha 6(a,b,c)

Adv. Mwabukusi: Maudhui yake ni kuweka usimamizi wa Rasimali za Watanzania kwa watanzania na wenzangu hawajasema hizi sheria kama zimeshafutwa. Sheria hizi bado ni hai na are so fundamental.

Adv. Mwabukusi: Na are forming basis of protection of our natural resources. Ibara zote tulizozitaja kwenye IGA , inakiuka Katiba ya Tanzania.

Waheshimiwa majaji maudhui ya sheria hii yana ukatiba kwani sheria hizi zinafafanua Katiba ya Tanzania Ibara ya 27[1

Adv. Mwabukusi: Wenzetu wanasema Kwa sababu ni International treaty hivyo Viena Convention kutumika na wao walisahau kuwa sheria husika imeweka pia angalizo.

Katika ibara ya 46(1) cha Viena Convention [Quote).

Anasimama wakili wa serikali aitwaye Kalokola anaweka pingamizi.

SA Kalokola: Objection, waheshimiwa majaji msomi hakutumia Ibara ya 46(1) na hawakutumia ibara husika hivyo hatakiwi kutumia ibara yako.

Adv. Mwabukusi: Mwabukusi: wao walisoma kifungu cha Viena convention in absolute na wakasahau kwamba kuna angalizo kwenye VIENA CONVENTION.

Jaji: Tunakubaliana na wakili wa serikali kwamba hiki kitu ni kipya na wao hawana nafasi ya kujibu.

Adv. Mwabukusi: Taifa letu tume-domesticate charter of Economic rate and Duty of the state, under Article 2(1)(2)a, b kwenye sheria ya Rasilimali. Na.6 ya 2019.

Wakili Mwabukusi anasoma hivyo vifungu.

Adv. Mwabukusi: Yametumika maneno Sovereignty na maneno haya hayapo kwa bahati mbaya. Kesi ya SMZ Vs. Machano Hamisi, page 7 paragraph 1 inayoeleza nini maana ya Sovereignty.

Paragraph ya kwanza na paragraph ya mwisho: (isomwe) kwa msisitizo.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walisema IGA ni frame work na kutakuwa na mikataba mingine midogo kwamba HGA ndio zitaweka masharti haikuwa sahihi.

Kwa sababu ibara ya 12 (2) ya IGA imeeleza wazi na naomba waheshimiwa majaji wakati mnatafakari msome ni kinyume cha wenzetu walivyosema.

Adv. Mwabukusi: Wenzetu walisema masuala yanayolalamikiwa yatakuwa kwenye HGA lakini ukweli ni kwamba kifungu cha 12(2) kimeshaweka masharti.

Jaji: Naomba usome 12(1)d.

#Updates kesi ya bandari.

Anaendelea wakili Mwabukusi kuwasilisha majibu yake.

Adv. Mwabukusi: kifungi hiki kimetumia neno shall na hivyo HGA tayari masharti yake yapo kwenye mkataba wa IGA na nawaalika msome Ibara ya 20[3] ya Mkataba wa IGA.

Adv. Mwabukusi: Hii ibara wenzetu wanasema tutaikuta kwenye mkataba wa HGA wakati tayari imeshatajwa kwenye Mkataba wa IGA. Hivyo HGA tayari ipo kwenye Mkataba wa IGA.

Anasimama wakili wa serikali anaweka pingamizi kwamba Boniface Mwabukusi anaingiza jambo jipya.

SA Kalokola: Objection, tunapinga kinachoendelea, ni kubadili pleadings hawakulalamikia ibara ya 23[3) atuonyeshe wapi wamelalamikia hiyo ibara.

Jaji: SA Kalokola, nenda kwenye Originating Summons soma kwenye paragraph 2 kinasomekaje

SA Kalokola: hakuna ibara hiyo ya 20[3) ya Mkataba wa IGA.

Adv. Mwabukusi: Wao waliwasilisha kuhusu HGA kwamba HGA itafanyika baada ya MKATABA wa IGA na mimi ninajibu kwenye hoja waliyoiwasilisha.

SA Kalokola: waheshimiwa majaji akijielekeza kwenye ibara ya 20, 21 ya mkataba wa IGA Na sio Ibara ya 23(1].

Jaji: Kuanzisha hoja mpya katika Rejoinder ni kukuza mjadala naomba juelekeze kwenye hoja ambazo sio mpya. Sisi tutasoma nyaraka zote.

Adv. Mwabukusi: Wakati mawakili wa serikali wanawasilisha majibu yao walisema migogoro ya IGA itatatuliwa na mahakama za ndani, lakini ibara ya 20(2]a,e(i)[ii][iii][iv] ya IGA zinaeleza kwamba mabaraza ya kigeni ndio yatashughulikia migogoro baina ya pande mbili.

Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa majaji, hiki ni kinyume na Katiba ya Tanzania na sheria za nchi zinazohusu rasilimali za nchi.

Kesi na 23 ya TLS ya mwaka 2014 ulioamuliwa mwaka 2019 uamuzi huu haukuzingatia Sheria hizi za Rasilimali za asili Na.5 na 6 za 2017.

Anamaliza wakili Mwabukusi sasa anamkaribisha wakili Livino kuendelea kujibu.

#Updates kesi ya bandari.

Anasimama wakili Livino Ngalimitumba.

Jaji; maana ya jina Ngalimtumba ninini

Adv.Livino: kwa asili sisi ni wakisi na maana ya hili jina maana ake ni Kutatua migogoro.

Mahakama: kichekoooo

Adv. Livino: Wakili : Nitajibu hoja za wakili wa serikali Edwin aliyejibu hoja zangu waheshimiwa.

Kwanza alilalamikia kwamba kitabu cha Rules of Law VRulers of law sikuwapa kopi ili akasome.

Adv. Livino: Ningependa kujibu kwamba alikuwa na muda wa kujiandaa maana alikuja kujibu hoja siku ya pili na Senior wake Wakili Mark alikubaliana na kitabu husika na content zake.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, alieleza kuhusu kanuni zilizowekwa kwenye kesi mbalimbali haswa kunapokuwa na malalamiko kuhusu uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Ni muhimu kulinganisha vifungu vya katiba pamoja na vifungu vinavyolalamikiwa.

Adv. Livino: Alitaka kesi ya AG Vs dickson sana, kesi ya Christopher Mtikila Vs AG 1995.

Na kunukuu maneno yaliopo katika kesi ya mtikila ya 1995 ukurasa wa 34.

Naomba mahakama itambua kuwa katika hizo kesi kulikuwa na issue tofauti na issue tulizonazo leo.

Adv. Livino: Kesi ya Dickson ilieleza kuhusu uhalali wa kifingu cha 145[8] CPA Cap 20 kuhusu issue ya dhamana katika makosa ya jinai.

Kesi ya mtikila, mahaka ilikuwa inatatua hija nyingi, uk.36 par. [g) ilijikita Katika kurekebisha marekebisho ya 8 ya katiba ya Tanzania ya 1977.

Adv. Livino: Kesi zote hizi mbili mahakama ilialikwa kutazama uhalali wa Statutes Act of Parliament na sisi tuko hapa kutazama vifungu vya mkataba na sio statutes na sio bunge.

Adv. Livino: Ni rai yangu kesi alizozinukuu SA Edwin hazipaswi kuwa applied kwenye kesi hii absolute bila kutazama circumstances ya kesi tuliyonayo hapa

Kwa kuwa tunatazama uhalali wa Mkataba, ni kanuni ya wazi kuwa mkataba wowote unaokwenda kinyume na sheria ni mkataba Batili.

Adv. Livino: Kwakuwa tunatazama uhalali wa Mkataba, ni kanuni ya wazi kwamba mkataba wowote unaokwenda kinyume na sheria ni mkataba Batili.

Waheshimwa majaji, mwenzangu alicante kesi ya SMZ Vs. MAchano Hamisi na wenzake, katika ukurasa wa 17 haswa kwenye tafsiri ya Sovereignty.

Adv. Livino: Tunakubaliana kwamba tafsiri husika ni sahihi kwakuwa ndio standard ya sheria za kimataifa.

Ningependa kukumbusha mahakama na wakili wa serikali Edwin kwamba issue zilizokuepo katika hiyo kesi, inapatikana katika page na 4 na 12 ya hiyo hukumu. Mahakama inaeleza.

Adv. Livino: Kwamba watuhumiwa hawa walikuwa wameshitakiwa kwa makosa ya uhaini ya kumuondoa Raisi wa Zanzibar.

Na page namba 12 paragraph 3 inaeleza kama Zanzibar ni Sovereignty state (Is zanzibar a Sovereign state.

Adv. Livino: Katika hilo naungana na wakili wa serikali kalokola alieleza kuwa muundo wa Emirates of Arabs inafanana kabisa na muundo wa Tanzania.

Hivyo Dubai haina mamlaka ya kuingia mkataba wa kimataifa kwa kuwa sio sovereign.

Adv. Livino: Wakati wakili wa serikali anawasilisha majibu yao alisema hatuwezi kupoteza Sovereignty kwa kuwa Tanzania ilipata uhuru 1961. Namkumbusha kwamba huo mwaka wa 1961 Tanzania haikuwepo.

Adv. Livino: Tanzania iliundwa 1964 Kwa hiyo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika ilipoteza sovereignty zanzibar ilipoteza sovereignty na kuunda Tanzania yenye sovereignty kama nchi moja.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, Mwenzangu alielezea Ibara 6(2) ya IGA kwamba Tanzania inaweza kuinterfere DP WORLD. Sisi tunapenda kusisitiza kwamba ibara hiyo imeweka interference Conditionally.

Adv. Livino: Kwamba interference lazima ieleweke na pande zote mbili na zjnapaswa kukubaliwa na pande zote mbili.

Hivyo Tanzania ikikubali kwamba kuna mgogoro na wenzetu wasipokubali maana yake Tanzania haita fanya interference. Hii inapoka sovereignty kama nchi.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, ni ukweli kwamba uandishi wa kifungu hiki unanyang’anya Sovereignty kinyume na ibara ya 1,8 na 28 ya Katiba ya Tanzania.

Kama nchi inawekewa vikwazo vya kujilinda kwa namna yoyote IGA ni batili.

Adv. Livino: Kuhusu ibara ya 8(2] ya IGA issue ya Land Rights alisema tusome tafsiri na anakubali kwamba sheria za nchi haziruhusu mgeni kumiliki ardhi.

Adv. Livino: Namkumbusha kwamba tafsi aliyoitaja ya IGA kuhusu land Rights. Ni mtizamo wetu kwamba inaongelea Ownership of land na inampa mgeni haki ya Occupancy of land.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, tafsiri ya ibara husika, ni mtizamo wetu kwamba sheria zetu zinaeleza kuhusu occupancy. Ukisoma kifungu cha 8(1)[2] vifungu hivi vinakusudia kumpa title DP WORLD Ku-occupancy land in Tanzania.

Adv. Livino: Waheshimiwa majaji, wenzetu walieleza ibara ya 66 ya Viena Convention ambayo inaeleza kuhusu kutatua migogoro kati ya nchi zilizokuwa katika nakubaliano.

Imeeleza kuwa kuna kwenda ICJ na pili ni ARBITRATION na migogoro chini ya IGA itakwenda kwenye mabaraza ya nje.

Adv. Livino: Ni mtizamo wetu kwamba uwepo tu wa vifungu vya IGA vjnavyoelekeza utatuzi wa migogoro katika mabaraza ya nje ni kitendo kinachokinzana na sheria za nchi kama Senior wakili mwabukusi slivyosema hapo awali.

Adv. Livino: Serikali wakati inaenda Dubai kufanya mazungumzo na DP World ilitakiwa kuwa na duty bind ya kuzingatia sheria za nchi yetu na kwa mantiki hiyo IGA inakuwa batili tangu mwanzo kwa kuwa sheria hazikufuatwa.

Adv. Livino: Ibara ya 21(3) ambayo inakataza Tanzania kujiondoa katika mkataba mpaka ridhaa ya DP WORLD ni mtizamo wetu kwamba kifungu hiki kinapoka sovereignty kama nchi

Ibara ya 23[4] isomwe pamoja na 23(4] kwamba mkataba huu hautaruhusiwa kuvunjwa inapoka sovereignty ya nchi.

Adv. Livino: Wenzetu walieleza juu ya Termination ibara ya 54 ya Viena convention. Ni maoni yetu kwamba ibara hii isomwe na ibara ya 60 ya Viena convention.

Waheshimiwa majaji, IBARA 23[4] wa IGA inasema mkataba huu haupaswi kuvunjwa hata kama kuna uvunjwaji wa terms za mkataba.

#Updates kesi ya bandari,

Anaedelea wakili Msomi Livino kujibu hoja zake.

Adv. Lovino: Tunaomba mahakama hii itambue kwamba hata VIENA CONVENTION Imevunjwa ambayo ilikuwa basis ya submission yao.

Adv. Livino: Wahe.majaji,wenzetu walieleza kuhusu nchi yetu kutii masharti ya kimataifa na serikali pamoja na Bunge ilitekeleza hilo.

Ni msimamo wetu kwamba ibara ya 14 ya Viena convention inatamka kwamba sovereignty ya mataifa iheshimiwa na Sheria za ndani ziheshimiwe.

Adv. Livino: Hivyo ni mtizamo wetu kwamba malengo ya kufanya ratification ya IGA kwa mujibu wa sheria za kimataifa na ndani hayakuzingatiwa.

Tunaomba mahakama hii itamke kuwa mkataba wa IGA imevunja pamoja na Viena Convention.

Wakili wa serikali Kalokola anaweka pingamizi kwamba; wenzetu hawakuomba order ya mahakama kwamba IGA imevunja Viena convention.

Jaji : Kwamba usingeomba order kungekuwa na tofauti?

Adv. livino; naondoa prayer husika waheshimiwa.

Adv. Livino: Wakili wa serikali Mr. Edwin alitaja ibara 4(2) ya IGA kwamba hakuna Binding obligation ya Tanzania kutoa taarifa kuhusu fursa za Tanzania. Ningependa kumwambia kwamba Mkata wote wa IGA is a binding document. Na hiyo inaonekama katika ibara 4(2) ya IGA.

Adv. Livino: Wakili wa serikali alisema ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania kwamba ibara hii inaongelea VITA. Alieleza kwa IGA haijaeleza masuala ya Vita.

Ningependa kusema kwamba Dunia imebadilika. Uvamizi wa sasa sio lazima wavamizi wakanyage ardhi ya Tanzania.

Adv. Livino: Uvamizi ni pamoja na uvamizi wa misingi ya uchumi pamoja na vyanzo vya mapato yake kama Rasilimali za nchi ikiwemo Bandari.

Kwa hiyo tunaposema usalama wa nchi na kutambua adui wa nchi. Hatupaswi kuangalia ardhi pekee na nimaelekezo ya kanuni za utafsiri wa Katiba.

Adv. Livino: Kwamba isitafsiriwe kwa namna ambayo inapoteza maslahi ya nchi. Kuna kesi ya Julius Ishengoma ipo naomba musome page 16 ambapo mahakama inaeleza namna ya kutasmfsiri vifungu vya katiba.

Adv. Livino: Ilisema mambo yafuatayo, Katiba itafsiriwe in a Liberal manner, jealously, our people enjoy their rights, will of the people must prevail.

Adv. Livino: Dhumuni letu kwamba katiba itafsiriwe kwa mawanda hayo na tunapoitafsiri ibara ya 28 ya Katiba ya Tanzania kuhusu usalama wa nchi tunamaanisha tusiishie maneno tu yaliyopo hapo kwenye katiba tunapaswa kuakisi mabadiliko ya nchi.

Adv. Livino: Tuko ibara 2(1) ya Katiba Tanzania inaeleza mawanda ya Tanzania (Quote) lakini neno anga halijatajwa hapa.

Na ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania haijataja anga. Swali ni je, Watanzania hawahusiki na anga na hivyo tusideal na anga.

SA Edwin: Objection, Ibara ya 2(1) haikutajwa hivyo tunaomba asiitumie

Livino: Naondoa kwa kuwa mahakama ilisema itasoma nyaraka zote.

Kwa kumalizia ni kwamba mahakama ijielekeze katika nyanja mbalimbali katika kutafsiri Masuala ya Katiba.

Adv. Livino: Kwa kumalizia wakili wa serikali alitaja taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo TBS , uhamiaji n.k lakini ukweli ni kwamba hayo ni maneno yake mwenyewe na wala hayapo kwenye IGA.

Anamaliza Wakili Livino sasa anamkaribisha Philip Mwakilima.

#Updates kesi ya bandari.

Anasimama wakili Philip Mwakilima kujibu hoja

Adv. Mwakilima: Waheshimiwa majaji: nitajikita katika issue na.6 kama IGA ilifuata sheria ya Manunuzi(Procurement Act) na naomba sehemu niliyofanya katika mawasilisho ya awali iwe sehemu ya Rejoinder hii.

Adv. Mwakilima: Wakili Kalokola akirespond kiapo cha walalamikaji kuhusu neno DPW na neno linatakiwa kusomwa ni DP Word.

Adv. Mwakilima: Kutokana na principle za overriding objectives ibara 107A (2)e ya Katiba ya JMT,1977 as amended inaitaka mahakama ijikite katika kutenda haki kwenda kwenye substance na sio legal technicalities.

Adv. Mwakilima: Hivyo typing Error inapaswa kutoathiri haki za wateja wetu.

Katika kiapo kinzani wamekiri kwamba hakukuwa na Mchakato wa kutoa Tenda na pia hawapingi kwamba sheria inayotuongoza mcahakato wa Tenda ni Procurement Act.

Adv. Mwakilima: Ni kwamba wanakili kuwa sheria hiyo imevunjwa.

Waheshimwa majaji wenzetu walitaja kifungu cha 4(1) ya Procurement Act, wakili akiwa amekuja na tafsiri kwamba IGA ni International treaty.

Adv. Mwakilima: Waheshimiwa majaji kifungu husika, there is no any conflict between PROCUREMENT ACT and International treaty. Pia IGA haina sifa ya kuwa International treaty.

Adv. Mwakilima: Kama kalokola alivyosema Zanzibar na Tanzania ni sawa Dubai na Emirates of Dubai. Kwa misingi hiyo hakuna International treat

Kama mahakama itakubaliana na sisi kwamba kifungu cha 64 cha Sheria ya Manunuzi (Procurement Act) Mkataba wa IGA Umekinzana na sheria hii.

Adv. Mpoki: Waheshimiwa imetuchukua siku nne, na research imefanyika. Kuna msemo unasema if you can’t convince them confuse them.

Mahakama: kicheko kidogo 

Adv. Mpoki: Waheshimiwa majaji, tunasubiria uamuzi wenu. Thus all.

Anamaliza wakili Mpoki sasa mahakama inakaa kimya kwa muda.

Majaji Ndunguru: naomba kabla sijatamka tarehe ya maamuzi; kwa niaba ya majaji wenzangu nawashukuru sana Mawakili pande mbili.

Jaji: Kwa kile mlichokionyesha, sisi tumeona the highest level of professionalism namshukuru sana.

Jaji: Naomba pia kipekee nimshukuru wakili Boniphace Mwabhukusi kwa kucheza vizuri sana akiwa ndani ya mahakama na akiwa ulingo wa siasa huko nje. Mwabukusi ameitendea haki taaluma yake.

Baada ya kusema hayo niseme kwamba mahakama hii itatoa hukumu yake siku ya tarehe 7 August 2023 siku ya jumatatu.

Majaji wanatoka.

Read More