Category: Katiba
MASWALI NA MAJIBU YA MWENDELEZO WA MJADALA JUU YA KUMBUKUMBU YA MUUNDO WA KATIBA YETU NA HISTORIA YAKE..MJADALA UNAENDELEA
[06:59, 13/05/2023] A: Nimejaribu kufatilia kwa kina mjadala bado nimeona ipo haja kubwa mno wanachi kupewa elimu ili kuielewa kwa upana katiba tuliyonayo kuelekea ktk mpya kimsingi wananchi hawana uelewa mzuri wa katiba iliyopo kwa mantiki hiyo kutakuwa na ugumu wao kuchangia ktk upatikanaji wa katiba mpya ikiwa ya zamani hawaielewi [07:35, 13/05/2023] +255 783 157: Sisi tunataka katiba ile ya warioba. Anania njema kuliko ile rasimu ya Bunge iliyojaa maslahi ya wanasiasa. [07:41, 13/05/2023] A: ktk kupata kuna michakato ambayo ipo kisheria ktk kuchakata kuanzia ukusanyaji wa maoni hadi bunge la katiba,ndipo nikasema ipo haja ya wanachi kupewa elimu ili kuielewa katiba hii tulioonayo ili waweze kutoa maoni kwa ufasaha baada ya kuona mafungufu ambayo yakipatiwa ufumbuzi kwa faida ya afya ya Taifa kwa ujumla [07:58, 13/05/2023] +255 62: Mpaka watu tukaenda kutoa maoni kwenye ile ya jaji wariomba bado tulikua hatuelewi tu?
Hata ukianza saiz kuelimisha watu kuhusu katiba bado kunawengine kwa makuaudi kabisa wataamua wasichukue hiyo elimu ila kwakua wengi kwasasa wanayo iyo elim na watu wameshiriki kutoa maoni Yao tusipoteze muda ikashindwa kukamilika kwa wakat tuendelee na ile ya Jaji Wariomba
[08:13, 13/05/2023] P: Ukisema hivi, na mimi naomba niulize; kwani hiyo katiba ya zamani wangapi wameiona? Wangapi wameisoma? Lini Iliwahi kusambazwa kwa wananchi wakashindwa kuisoma?Na hao “wananchi wengi” tunaosema “hawajui katiba” ni akina nani hasa? Je, ni sisi tuliopo hapa mtandaoni au watanzania kwa ujumla?
Maana kama wengi wetu hapa hatuijui na hatuwahi kuiona ya zamani, achilia mbali kuisoma na kuielewa, je, hao wananchi wa kawaida huko mtaani inakuwaje?
Kwa mantiki hiyo ya “universal ignorance ya katiba”, wanaotegemewa kujadili na kutoa maoni yao na yachukuliwe serious, ni akina nani hasa? Maana sehemu kubwa ya watanzania watakuwa hawajui katiba ya zamani, na hata hii ya sasa ni wachache wamewahi kuisoma seriously kifungu kwa kifungu.
Kwa uzoefu wa kawaida, Katiba nzuri, huandaliwa na watu wacheche sana wenye weledi wa kiwango fulani cha mambo sheria, siasa, na utawala. Sehemu kubwa ya wananchi wa kawaida hushiriki m kutoa maoni yao tu wkt wa kukusanya maoni. Baada ya kukusanya maoni ya wenye nchi, hakunaga tena hizi gimmicks za kujizungusha zungusha.
Hata sisi Tanzania tumefanya haya, tena kwa ushirikishaji mpaka sana wa wananchi nchi nzima. “Rasimu ya matakwa ya wananchi” ipo intact kabisa.
Kinachotakiwa sasa hivi siyo kurudia tena kukusanya maoni, kwani tunataka maoni gani zaidi, ya nani, na kwa ajili gani?
Kinachobaki hapo ni timu ya watu wachache tu wenye sifa nilizotaja hapo juu, kujifungia mahala; kuchambua, kuchakata, kudadavua, na kuja na majibu ya kutukwamua tulipokomea last time, that’s it.
Nilidhani lengo la Rais kuunda Timu Kazi, na baadae kum task Msajili wa vyama na kazi ya kuwaita wanasiasa ili wakae na (timu kazi?) Ilikuwa ni kufufua tu kilichokuwa kimetaka kufishwa ili kiendelee kupumua na kuidhi.
Leo tunapianza mijadala ya kuhimizana kutoa maoni tena najiuliza: kumbe tayari imeshaamriwa kwamba mchakato wa kwanza ulikuwa batili, na kwa hiyo muda na gharama iliyotumika tuhesabu ndio tumeliwa?
Au kuna nini ambacho mimi sielewi? 🤷🏾♂️

Wazo langu bado elimu ya uraia inahitajika sinauhakika kama wananchi tunaijuwa katiba kutoka kava yake mpaka ukurasa wa mwisho,
1. Katiba ni nini
2. Kunaumuhimu gani wa kuwa na katiba
3. Je katiba iliyopo ina matatizo gani
4. Kwa nn tunahitaji katiba mpya
Najaribu kuyaeleza haya kwan masuala mengi yakiwemo haya wananchi wengi wanajiliza na kwa bahati mbaya hakuna jibu ambalo litamuezesha mwananchi wa kawaida kutoka hapa tulipo na kuingia katika hiyo mijadala ya katiba.

Elimu inahitajika na nishauru serikali zetu zote mbili kuvihusisha vyombo v…
[10:22, 13/05/2023] A: Hayo maswali manne ni muhimu mno lkn hata ukifatilia hao wanaojita wana harakati wote ni watu Dar Mjini ukiukiza uwakilishi wa wakulima huko vijivini uko wapi hupati jibu na hakuna mwaharakati hata mmoja wa nyamisati au kibondo wote ni wamjini wapiga dili [10:26, 13/05/2023] +255 : wakibondo tupo wasomi… tunawakilisha… ila naonga mkono hoja… wafikiwe wote kama zinavyopitishwa sheria ndogo za halmashuri inamaana mikutano ya wananchi kwenye vijiji na mitaa ifikiwe na kwenye kata. Maana sio wote wako kwenye mitandao wala kusikiliza radio.. [10:29, 13/05/2023] A: sasa nini tufanye ili kufikia malengo?..Mjadala unaendelea………….MJADALA JUU YA NAMNA BORA YA KUWA NA KATIBA MPYA,UELEWA WA MCHAKATO MZIMA NA KUFAHAMU KATIBA YA SASA UNAENDELEA KATIKA FORUM YETU YA KATIBA YA WATU MASWALI YA PAPO KWA HAPO YAMEULIZWA NA KUJADILIWA
[12:07, 11/05/2023] P:
Ndugu zangu,
Uzalendo wa kweli huwa haufundishwi darasani kwenye makongamano, warsha, au semina.
Uzalendo wa kweli hufundishwa na Serikali/nchi kuwafanyia wananchi wake vitendo chanya vyenye kuwawekea mazingira sahihi na bora ya kujitegemea na kufikia ndoto zao ndani na nje ya mipaka ya nchi yao.
Mimi sijawahi kufundishwa uzalendo na mtu darasani au mtaani.
Lakini mtu akihoji uzalendo wangu kwa nchi yangu niko tayari kumtoa roho!
Mimi nilijikuta NAIPENDA NCHI yangu na NIKO TAYARI kuipigania, kuilinda, na kuitumikia kwa moyo wangu wote na hata kwa uhai wangu…kutokana na jinsi serikali/nchi yangu ilivyonionesha upendo, kunijali, kunilinda, kunitetea, na kuniwekea mazingira wezeshi ya kuja kuwa hivi nilivyo
[12:23, 11/05/2023] +: Hili neno UZALENDO nadhani linapaswa kutafsiriwa kwa upana once and for all. Tunapaswa tulijue kwa upya na katika tafsiri pana zaidi. Watanzania waliowengi, hasa wenye madaraka wanapaswa ku “unlearn and relearn” maana sahihi ya neno UZALENDO ikibidi liwe defined kwenye katiba.Why? Kwasababu neno uzalendo lilitumika vibaya sana regime iliyopita na kuumiza watu wengi. Kila aliyehoji chochote kama raia huru alikuwa branded kuwa siyo mzalendo, na wengi walipata “taabu sana”
[12:26, 11/05/2023] T: Tutajadili kwa mapana kila jambo hapa lakini mjumbe mwenzetu alikuja hapa na hoja hii na huko nje wadau wa mlezi wanamlalamikia mlezi wao yaani msajili..hoja hii haijaisha..na Msajli yuko hapa… [12:36, 11/05/2023] P:Huenda hata Msajiri akawa hajui maana halisi ya “uzalendo” kwa nchi.
Tusipuuze hili nalo neno..😂😂🇹🇿🇹🇿✅
[12:59, 11/05/2023] Pr:Naomba niulize wawezeshaji wa hili jukwaa : je mchakato huu tunaanza upya kana kwamba uliositishwa haukuleta mambo yaliyokubalika ? Tutawajibikaje na Rasilmali iliyowekezwa kwenye mchakato uliyositishwa dakika za mwisho kwa sababu za kisiasa a a??? Kama kuna mambo ambayo hayakuwa na utata hayawezi kubebwa ili mchakato huu usimbebeshe mlipa kodi mzigo wa ziada? Naomba mwongozo🤷🏽♂️
[13:07, 11/05/2023] T:Hii ni Mada mpya kutoka kwa Mdau..Tunaweza kuendelea nayo tukisubili Nondo za Ofisi ya Msajili? wajumbe mnasemaje? Lakini kwa kifupi Hali ya uelewa wa hili jambo Tangu 2014 ni ndogo mno ukizingatia Vijana wetu wa sasa ambao kwa maelfu walikuwa wadogo kudadavua mambo yale,sasa jukumu kubwa kama wadau ni kujadili kwa mapana hapa na kuwaelimisha wengine juu ya Historia yote ya michakato ya Katiba Yetu na mustakabali wa baadae..wakati jukumu hili la uratibu liko kwa Msajili..wajumbe walipendekeza awali tumjue kwanza Msajili na ofisi yake na majukumu yake..wengi hawajui..hapo ndio tulianzia jana..Prof.
[13:28, 11/05/2023] Dr.:Asante! Baada ya kujua maana ya Katiba tungepata pia historia ya Katiba ya nchi yetu.
[13:36, 11/05/2023] Dr.:Wawezeshaji, naomba kama inawezekana tuwe na muda maalum wa kujadili kila mada. Mfano maana ya Ijue Katiba tujadili kwa siku mbili au tatu. Pia wajumbe wa hili group tuhimizane kutenga muda wa kufuatilia mijadala ya Katiba ndani na nje group 🙏
[13:36, 11/05/2023] A:Nimepitia mada hii vizuri sana na nimeptia kipenegere kwa kipengere.
Nadhani inatupidi tuanze kutazama Katiba kwa mtazamo mwingine. Badala ya kuwaza kitu cha kwanza kuhusu utawala, tuanze kuwanza kuhusu “How to manage our resourse”. Kwa mtazamo wangu msingi wa kwanza ni kuongelea Management of our resource.
Tuanze kuongelea kwanza our National Interest, Kwamba maslahi yapi ya Taifa letu tunataka tuyalinde baada ya hapo ndipo tuweze kuanza kuongelea Utawala, Haki na wajibu.
NB: wazo langu ni kwamba tuanze kwanza na “Management of Our Resources and Defining of our National Interest”
[13:38, 11/05/2023] K:Ikiwa kuna matumizi mabaya/yasiyo ya lazima n.k n.k n.k
Je tufanye Kesi kwanza? Au Tuchukue yatokanayo yanayofaa ili yatumike kwenda mbele kwa ubora? Au tusubiri tuwakamate waliotumia fursa vibaya kwanza…..choices…choices! 🤷🏾♂️
[13:45, 11/05/2023] M: Lisu na Silaha wakilalamika kuwa Rais anaonekana kuuteka mchakato wa Katiba na kuuweka mikoni mwa wale wale. Sijui walitaka afanye nini!! Rais kama taasisi vipo, vyombo chini yake vya kumsaidia kuhahakisha kuwa Katiba inayokusudiwa, inapatikana na kuridhiwa na Watanzania kwa ujumla wao. Hivyo naamini Msajiri wa Vyama vya Siasa ndiye mtekelezaji mkuu wa mchakato huu. Nadhani tusubiri kuona hatua atakazochukua kutekeleza jukumu hili. [13:52, 11/05/2023] T: Ndio maana akamleta Msajili kama mlezi wao aongoze jahazi walitaka aanzie wapi? [13:53, 11/05/2023] A:1. Kwanza kabla ya kuanza kuongelea utawala. Nimuhimu kuongelea Lengo letu sisi kama watanzania kuwa pamoja (The purpose of Nationa)
2. Foundations of our nation. Je, Taifa letu lina misingi ipi? (Philosophical, Moral, Cultural) Hii ndiyo misingi.
3. What is our national interest (Sisi kama Taifa maslahi yetu ni yapi. Kutokana na maslahi yetu tunataka tujenge taifa la namna gani?)
3. Lazima tuangalie hustoria yetu. Yaani tunataka Tanzania ya sasa lakini ni vizuri kuikubali historia yetu.
ALL NATIONS HAVE FUNDAMENTAL INTERESTS THAT THEY WOULD LIKE TO DEFEND AND PRESERVE
[13:55, 11/05/2023] T:Muda tutaupanga sisi hapa nashauri kwa vile kunauchambuzi kwa sauti pia ni vema wadau kuwe na mpangilio kwa kifupi Tumeanza vyema na sasa tuweke bayana nini tunapaswa kukiweka awali HISTORY KWANZA
[13:57, 11/05/2023] P:Kwa vile Mwenzeshaji ameshauri tuairishe hii mada basi ngoja nisubiri wakati Mwafaka. Kwa ufafanuzi wangu nilieibua hii mada niseme tu kwamba kwa vile katiba ni Sheria mama/Sheria kuu inayobainisha misingi mikuu inayoelekeza mamlaka na mipaka ya wenye dhamana ya kuongoza na kubainisha haki za raia na wajibu wao pamoja na misingi ya uwajibikaji, basi bila Shaka mchakato uliyositishwa kulikuwa na misingi ambayo haikuwa na utata🤷🏽♂️je hatuwezi kuibeba? Hilo ni swali kuhusu mchakato🤷🏽♂️
[14:07, 11/05/2023] P:Hii ya kuanza kuelimishana kuhusu Katiba Mpya ni tactical maneuvre ya irresponsible stakeholders kuchukua hatua stahiki kumaliza hii deadlock.
Kwani tunataka wananchi waelimishwe juu ya Katiba kwani wao ndio waliokwamisha mchakato kukamilika?
Kama wananchi walizungukiwa nchi nzima wakatoa hadi maoni yao juu ya Katiba Mpya kweli walikuwa hajui wanachokifanya?
Unajua kuna vitu vinfanywa mpaka unacheka.
We are an independent nation of more than 60 years. Lakini kuna vitu tunafanya kama watoto wa miaka 6.
We wasted taxpayers money on a sham exercise. We should be ashemed and apologize to the public.
Badala yake tunataka kuwarudia waliokwisha kutupa maoni yao juu ya Katiba kuwaelimisha nini?
How absurd..
[14:10, 11/05/2023] P:Watu wengi kina nani? Kwani hao watu wengi wasioelewa huwa tunasubiri waelewe kwenye mambo mengine yote yanayoamriwa bila uelewa au consent yao?
The rest is same old staff that have gotten this nation into this s**t
[14:42, 11/05/2023] M:Tusiyumbishane bure hapa. Ushiriki wa watu kwenye jambo lolote lile kote duniani, ni kupitia uwakilishi. Ndio maana tuna vyama vya siasa wanaowasilisha itikadi za vyama vyao kwa umma, na wabunge katika ngazi ya kuisimamia serikali na kutunga sheria. Hivyo mtu kusema watu wengi waelewe kwanza ndipo hatua zaidi zifuate, huo uwingi unaupima vipi kama sio kwa njia za kiuwakilishi zilizopo kufutana na Katiba na sheria za nchi! Group hii ni uwanja wetu kuchangia kile mtu anachokiona kingefaa kuzingatiwa au kuangaliwa katika mchakato huu wa sasa wa kutupatia Katiba itakayoridhiwa na umma wa Watanzania kupitia uwakilishi kwa njia moja au nyingine. Tushiriki kutoa mawazo/maoni humu ambayo naamini wahusika watayatumia katika ngazi zao za uwakilishi.
[14:47, 11/05/2023] T:Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 Ongezeko la watotoni Mil 16 baada ya miaka 10 wengi wao watakuwa watu Wazima Rudi nyuma sensa ya 2012 mwaka mmoja baada ya mchakato kuanza..watoto wale ambao ni more than 40% ya raia wote leo ni watu wazima wala hawakuhusika kabisaa na hayo maoni na ndio kizazi kina hoji nini kilitokea
[14:49, 11/05/2023] T:Na ndio maana hata wewe leo huelewi kwanini Msajili anajukumu hili leo…
[14:51, 11/05/2023] P:Ufikiri wa aina hii ni very mediocre. Tukianza kusubiriana kila mtu ashikishwe basi hata hii Katiba iliyodumu kwa mingo zaidi ya 4 sasa ni uhalifu kwa wale ambao hawakushirikishwa?
[14:57, 11/05/2023] T:Ndio maana uko hapa kujadili namna bora ya kupata katiba bora kama Rais alivyoainisha na kumtaka Msajili kutekeleza jukumu la msingi kuwaita washirika wake wakuu vyama vya siasa wewe na walioleta mada wakataka kujua nini wajibu na jukumu la msajili katika hili Tuendelee kutoka hapo
[15:00, 11/05/2023] P:Nina hofu wadau wenzangu kuhusu mchakato wa Katiba ya Wote kuendesha na vyama vya siasa.vyama hivi ni wadau wanaowakilisha sehemu ndogo tu ya Watanzania. Hivyo Vina uhalali wa kushiriki kama wadau wengine , asasi au mashirika mengine: kwa maoni yangu Vyingi haviongozwi na misingi ya demokrasia( internal democracy) Mimi najiuliza kwanini Asili Mia tisini ya vyama tangu viundwe hadi Leo vinaongozwa na watu walewale tena wanaume 🤷🏽♂️Ni vyama vingapi vimefungua milango ya demokrasia shirikishi? Kwenye uongozi?? Kwangu mimi kuwe na tume huru ya kuongoza mchakato ili dhamira ya Rais wetu ya kuleta mabadiliko katika mifumo kandamizi na ya ubaguzi.
👆👆👆👆👆Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.
[15:08, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU:
1. Napongeza Mwanzilishi wa Jukwaa hili kwa maana litasaidia kupata mawazo mapya; mbadala; kujikumbusha tulikotoka, tulipo na tunakokwenda ni wapi kuhusiana na suala la Katiba.
2. Mimi ninavyojua ni kwamba, Mchakato kuhusu mwendelezo wa Mabadiliko ya Katiba mpya ya Tanzania “Bado haujaanza rasmi katika kuuendeleza.” Kwa sababu:-
2.1: Tangazo la Serikali bado halijatolewa tena kuhalisha Mwendelezo wa Mchakato.
2.2: Bado hakuna na haupo Mwongozo wowote juu Mwendelezo wa suala hili maana siku zimepita nyingi saana tangu kukoma kwa Mchakato wa Katiba na Tangazo la Serikali likatoka juu ya kukoma kwake.
2.3: Tangu kukoma kwake, imepita takriban miaka 9 (hii ni miaka mingi) ambayo inatutaka kama taifa pengine Mchakato uanze upya ama uwe na mwendel…
[15:09, 11/05/2023] P:Naelewa mno ndio maana naona this is yet another waste of the Tanzanian people’s time and tax money.
It’s time tuwaheshimu watanzania na kuwaona wana akili timamu. Wanajua kinachoendelea wa sehemu kubwa tusema hawana tabia a ku protest kwa kila kitu.
Why these gimmicks every now and then?
The country has a lot of more pressing issues to deal with than keep tip toeing around Katiba Mpya wakati tunajua kinachoweza kufanywa na tunaweza kukifanya without all these back and forth drama.
[15:11, 11/05/2023] M:Mimi nadhani kazi kubwa ilifanyika chini ya Tume ya Warioba. Jambo la kuangalia tulikwama wapi na nini kifanyike kukwamua mchakato huu. Kwa wale wenye muda, tuipitie Rasimu hii na kutoa maoni yetu.
[15:15, 11/05/2023] T:Wazo la kujadili pamoja kwa staha ni jema.. na ndio maana mijadala hii ipo tumeanza na namna tunaovyona Msajili na majukumu yake anatakiwa atupitishe wapi Mjadala huu unaendelea na tutafika kote wajumbe wanakotaka tupite na uzuri wadau wote wako hapa..nashauri Lugha za staha na kuepuka mihemko ili tuwe na mawazo yenyetija kwa mustakabali wa pamoja…
[15:26, 11/05/2023] Pasta Martin: Precisely!Tume ya Warioba walifanya kile ambacho hakijawahi kufanyika katika historia ya nchi hii nzuri.
Kwa mara ya kwanza maoni ya wananchi yalikuwa broadly collected and accurately documented.
Tunajua wananchi (wenye nchi yao) walichotaka. Tatizo hatujawahi kuwa na utamaduni wa kuheshimu wanachotaka wananchi!
Demokrasia yetu ni ya kijanja janja hivi. Hata pale tunapojua wananchi wanataka nini lazima tu edit kidogo ili kuingiza matakwa yetu binafsi.
Even on this attaempt, we are commiting the same sin of arm twisting the public to bend to our tune.
Mchakato ulishaisha. Msimamizi wa mchakato bado yupo hai. Mzee Warioba bado yupo timamu kabisa. Kama nia yetu kweli ni kuheshimu maoni ya watanzania, kwa nini asiitwe msimamizi wa ukusanyaji wa maoni pek…
[15:31, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 2:
1. Msajili wa Vyama vya Siasa yuko chini ya Mamlaka katika Mhimiri mtambuka. Kwa hiyo, sio Mhusika Mkuu wa kuuendeleza Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba mpya ya Tanzania.
2. Ninavyojua Mwendelezo wa suala hili liko chini ya “Wizara ya Sheria na Katiba” ndo wanaotakiwa kutoa Mwendelezo na Kutuongoza tunaanzaje na tunaendaje.
3. Kiongozi wa Jukwaa letu hili, ajikite katika kushinikiza Mwendelezo na uhalalishaji wa Mchakato husika.
[16:21, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 3:
1. Hoja/Mada ya kwanza iwe KUJIKUMBUSHA KUHUSU, “Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mchakato ulianzaje, Ulifanyikaje na Uliishia wapi!?.”:-
1.1: Kwa nini Wananchi walidai Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.?
1.2: Je, Wananchi na wadau mbalimbali walishiriki kikamilifu kutoa Maoni yao!?
1.3: Bunge la Katiba lilifanya kazi yake ipasavyo kuwakilisha makundi ya Jamii yote ya Tanzania kuipata Katiba waitakayo.?
1.4: Nini kilikwamisha kutokuwepo Katiba Mpya licha ya Mchakato kufanyika na ushiriki wa Wadau wa makundi yote kushiriki!?
2. Hoja/Mada ya pili iwe NAFASI NA WAJIBU WA SERIKALI KATIKA KUUENDELEZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:-
2.1: Kwa sasa Serikali ifanye n…
[16:25, 11/05/2023] A:Naona sijajibiwa hoja yangu ipasavyo, pengine tujuzane tu Hali ya sasa na takwimu za sasa juu ya uelewa wa Mtanzania kuhusu maswala ya katiba Tanzania ikoje maana naona kama kuna mkanganyiko baina ya wanaojua na sisi tusiojua..
[16:40, 11/05/2023] K:Mimi Sijaweza kupata takwimu kamili za hivi karibuni juu ya uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya katiba nchini Tanzania. Hata hivyo, ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya katiba ni mdogo. Ripoti ya Jukwaa la Katiba Tanzania iliyochapishwa mwaka 2019 inaonesha kuwa asilimia 62 ya wananchi hawajui kuhusu mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania.
Ripoti nyingine ya Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ya mwaka 2018 inaonesha kuwa asilimia 50.8 ya wananchi hawaelewi kikamilifu maudhui ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ripoti hiyo inaeleza kuwa wananchi wengi hawajui wajibu na majukumu ya serikali na wananchi, haki za msingi za binadamu, utawala bora na demokrasia.
Hata hivyo Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan , amesiskika mara kwa mara akizitaka Taasisi za Kiraia na zile za kidini wasaidie katika kutoa elimu ya uraia katika katika maeneo haya, na wengine waliopewa majukumu naamini kabisa kuwa moderator umewaweka humu.
Ni muhimu sasa kwa serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari, na taasisi nyingine kushirikiana katika kutoa elimu na kuongeza uelewa kuhusu masuala ya katiba na mchakato wa kupata katiba mpya nchini Tanzania. Hii itasaidia kujenga uelewa wa pamoja kwa wananchi na kuongeza ushiriki wao katika mchakato huu muhimu wa kitaifa.
[16:41, 11/05/2023] K:Ninaunga Mkono Hii Hoja ni sawa sana!!
[16:44, 11/05/2023] K:1. Hoja/Mada ya kwanza iwe KUJIKUMBUSHA KUHUSU, “Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mchakato ulianzaje, Ulifanyikaje na Uliishia wapi!?.”:-
[16:45, 11/05/2023] Pasta Martin: This is a non-issue guys.Watanzania wengi au wachache kujua Katiba au kutojua haizuwii au kusababisha chochote kifanyike au kisifanyike.
Kuna mambo mengi tu watanzania hawajui na yanafanyika lkn hakuna tatizo.
Kwa Katiba, watanzania wanajua sana tu. Na walitoa maoni yao. Sasa hiyo kusema hawana uelewa inatoka wapi. Mi naona wasioelewa au wanaojifanya hawaelewi ni sisi wasomi na wajanja wachache tunaojadiliana humu kwenye mitandao.
[16:49, 11/05/2023] K:Hoja hii ya uelewa wa wananchi imetokana na ripoti za Utafiti na nadhani wasomi wanatembea na hizi takwimu ….ndicho kinachotatarajiwa kutoka kwa wasomi
[16:49, 11/05/2023] M:Mimi nadhani suala la Katiba kwa mwanchi wa kawaida, kwake is not an issue. Yeye anachohitaji ni utawala bora unaokidhi haki na huduma zake muhimu za kijamii. Zinapatikana vipi sio tatizo kwake. Hapo ndipo linapokuja suala la uwakilishi kupitia kwa wale wanaolewa nini maana ya Katiba ambayo ni sheria mama. Hivi niulize tu ni wangapi kati yetu siku za nyuma tumewahi kuhangaika kutafuta Katiba yetu inasemaje juu ya mambo mbali mbali? Ni kiri mimi sio miongoni mwa wale ambao nimewahi kujighulisha sana kujua vifungu vya Katiba yetu vinasemaje. Na kwa hali hiyo, sishangai sana watu kutoijua Katiba. Kama iliyopo mtu huijui utasumbuka kweli ni hiyo inayopiganiwa!!! Tuelezane ukweli tu kwamba Katiba ni eneo moja la taaluma ya Kisheria. Hata kwenye mijadala ya aina hii tuntegemea wanasheria kushiriki na kutuongoza zaidi. Huu ndio ukweli wenyewe.
[16:52, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 4 KULINGANA NA ULIVYOULIZA:
1. Suala la utoaji wa Elimu kwa Raia kuhusiana na Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lazima utolewe Mwongozo wa Elimu yenyewe, kwa sababu kama Mchakato/Mwongozo toka Serikalini haujaanza rasmi AZAKI na Taasisi mbalimbali zitatoa Elimu gani.!?
[16:52, 11/05/2023] +255:Na ndiyo maana tuna wana sheria, hao kazi yao ni kusoma na kuelewa katiba, sheria na kanuni. Sisi wananchi tunataka utawala bora unaofuata sheria, kwa upande wa wananchi awatakaa waielewe sheria tena hasa hii iliyoandikwa kwa kizungu. Mamlaka zinachoweza kufanya ni kutengeneza uelewa wa haki za watu hayo mengine tutakutana mahakamani😊
[16:53, 11/05/2023] K: exactly [16:54, 11/05/2023] K: Elimu ya aina ya Elimu! [16:54, 11/05/2023] M: 👍 [16:54, 11/05/2023] M: 👍👍👍 [17:02, 11/05/2023] : ipi sasa namna bora ya kutoa elimu ya katiba na mchakato ndio huu uko jikoni [17:05, 11/05/2023] K: 🤔Kwa Kufikiri kwa sauti NINACHOONA, Kutoa elimu ya Katiba kunapaswa kuwa endelevu na yenye kufikia watu wengi iwezekanavyo. Hapa ni baadhi ya njia bora za kutoa elimu ya Katiba:1. Kutoa elimu ya Katiba katika shule: Elimu ya Katiba inapaswa kuanza mapema shuleni. Wanafunzi wanapaswa kufundishwa kuhusu maana na umuhimu wa Katiba na jinsi inavyoongoza nchi yetu.
2. Matumizi ya teknolojia: Matumizi ya teknolojia kama vile mitandao ya kijamii, redio, televisheni, na programu za simu yanaweza kutumika kwa kutoa elimu ya Katiba kwa watu wengi zaidi.
3. Kutoa mafunzo kwa wanasiasa: Wanasiasa wana jukumu la kuelimisha wananchi kuhusu Katiba. Hivyo, mafunzo yatolewe kwa wanasiasa kuhusu maudhui ya Katiba ili waweze kutoa elimu sahihi kwa wananchi wao.
4. Kutoa semina na mihadhara: Semina na mihadhara ya umma yanaweza kutoa fursa kwa wataalamu wa Katiba na wananchi kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Katiba.
5. Kutoa machapisho na vifaa vya elimu: Vifaa vya elimu kama vile vipeperushi, machapisho, na vitabu vinaweza kusambazwa kwa wananchi kama njia ya kutoa elimu ya Katiba.
Kwa ujumla, njia bora ya kutoa elimu ya Katiba ni kutumia njia mbalimbali za mawasiliano ili kufikia watu wengi iwezekanavyo na kuifanya iwe ya kuvutia na inayoeleweka kwa wananchi wote
[17:09, 11/05/2023] M:MTAZAMO WANGU 5:
1. Niombe kiongozi/viongozi wa Jukwaa hili kutenga muda na saa maalumu ya kuchangia hoja (Mfano Jioni/Asubuhi/Usiku ya siku inayofuata ndio Hoja/Mada itachangiwa na Itatolewa kwa wote ili siku inayofuata kwa muda utakaowekwa kuchangia).
2. Napendekeza Hoja/Mada moja isizidi SAA 1.20.
3. Baada ya Hoja/Mada kujadiliwa, yatolewe Majumuisho na Maazimio.
[17:10, 11/05/2023] K:Ni Haki ya Rais kuwa ndiye ‘custodian’ wa mchakato huu kwa nia njema tu, kwa nafasi yake kama The Executive anatarajiwa kuwa ndiye mjibu maswali pindi mambo yakienda mrama ( of which hatuombi yatokee ) but, Asante Hon Judge kwa insight hii!!🙌🏽
[17:11, 11/05/2023] M: 👍👍👍Safi
[17:12, 11/05/2023] T: Kunamambo ya kujifunza hapa safi sana..mchanganuo wenye tija [17:15, 11/05/2023] +25: Kwani wanamlalamika bila kushauri? Muhimu tuangalie nini kinashauliwa kutoka kwako na sio kutaka watu Woote wasifieMe naona hata hao wasaidizi wake pia wanategemea mawazo yetu na taasisi inajua kutakua na lawama ushauri
[17:15, 11/05/2023] M: Mimi nafikiri katika mijadala itakayofuata na nadhani hata hii ambayo imekwisha anza, ijikite zaidi kutafuta sababu za kukwama kwa mchakato wa Katiba uliopita. Tukivuka ngazi hiyo kwa kuafikiana, then tatakuwa tumepiga hatua mbele ya kupata Katiba tunayoitaka. [17:17, 11/05/2023] M: Safi..!👍 [17:36, 11/05/2023] +255:kwa Kuzingatia Haya. kuwe na utaratibu mzuri wa kuwafikia viongozi wa serikali za mitaa(kata) na viongozi wa vyama vya siasa (kata) nchi nzima hapa ndio mzizi wa fitina wa kujua au kutoijua katiba kwa wananchi utakua ukomo wake na maoni yatapatikana hapa na kila kitu kama sheria zote ndogo au sheria za halmashuri zinavyoshirikishwa kwa wananchi na zinapelekwa bungeni na mwisho kufanya kazi hili muhimu sana…. ngazi ya chini ya serikali za mitaa na vyama vya siasa uko chini linatibu kila kitu…
[17:42, 11/05/2023] P:Kuna nchi nyingi tu duniani ambazo wananchi wake hawajui Katiba yao inasemaje, na hawajali.
Lakini kutokana mifumo imara ya kiutawala na UZALENDO wa viongozi wao husikii watu wakipewa elimu ya Katiba. Ili iweje?
Sisi hata tukifundishana katiba tukatoa na mitihani kabisa. Kama nia ya Katiba mpya haipo haipo tu.
Tutapeana elimu. Tupoteze muda. Tutatumi pesa. Lakini kama nia haipo, itabaki hivi hata miaka 10 ijayo.
[17:49, 11/05/2023] +:Jamani mimi ni mgeni humu ndani, tafadhali msinipige mawe….. Katika huu mchakato mpya wa katiba mpya, ile katiba ya Warioba inawekwa wapi? Au inakuwa kama Research Report!?? Maana kama kumbukumbu zangu ziko sahihi ilikuwa karibu na stage ya adoption. Na kama inakuwa considered, je mchakato utapaswa kuanzia stage gani??
[17:51, 11/05/2023] Kopwe:ni vyema tusifike hapa👆🏾 labda tunapishana namna nina Imani hata kama dhamiri haikuwepo sasa ipo tuanzie hapo! kwa kujenga juu ya “tofali hili”
[17:55, 11/05/2023] T:Nini sasa wajibu wa vyama vya siasa katika mchakato wa katika kwa sasa kunawano laumu na tukirudi nyuma hawa hawa wametufikisha hapa….
[18:10, 11/05/2023] K:Vyama vya siasa jukumu lao ni kubwa sana katika mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania kwa hapa tulipo. Ninaamini wana Wajibu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu, kwanza kwa kutoa maoni yao kuhusu vipengele mbalimbali vya katiba mpya na Pili, kutoa mapendekezo yao kwa ajili ya kuboresha rasimu ya katiba.
Tunaweza kuona mifano ya wajibu wa vyama vya siasa katika mchakato wa katiba ambayo ni pamoja na;
1. Kutoa maoni yao kuhusu vipengele mbalimbali vya katiba: Vyama vya siasa vinapaswa kutoa maoni yao kuhusu vipengele mbalimbali vya katiba mpya, kama vile mfumo wa serikali, muundo wa bunge, muundo wa vyombo vya dola na masuala mengine yanayohusiana na demokrasia na utawala bora.
[18:15, 11/05/2023] K:2. Kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa katiba: Vyama vya siasa vinaweza kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba kwa kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa katiba mpya na kuwahimiza kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya katiba.
3. Kutoa mapendekezo ya kuboresha rasimu ya katiba: Vyama vya siasa vinapaswa kutoa mapendekezo yao kwa ajili ya kuboresha rasimu ya katiba, kwa kuzingatia maslahi ya wananchi na mahitaji ya taifa kwa ujumla.
4. Kusimamia utawala bora na demokrasia: Vyama vya siasa vinapaswa kusimamia utawala bora na demokrasia kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa katiba unafanyika kwa njia ya uwazi, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora.
Kiukweli, vyama vya siasa vina jukumu muhimu katika kutoa maoni yao, kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi na kusimamia utawala bora na demokrasia.
[18:22, 11/05/2023] T: Karibu sana pamoja na kwamba swala hili liko Mbele lakini wataalamu hapa watakujibu kwa kifupi ili tuiweke kama MADA Baada ya kujadili wazo la @M “1. Hoja/Mada ya kwanza iwe KUJIKUMBUSHA KUHUSU, “Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mchakato ulianzaje, Ulifanyikaje na Uliishia wapi!?.”:- [18:31, 11/05/2023] T:Nakumbuka Mwanasheria Nguli na mataalamu mambo ya katiba ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu alisema Namnukuu “mchakato wa Katiba Mpya lazima utungiwe Sheria mpya ,sheria iliyounda Tume ya Warioba na Bunge Maalum la Katiba haiwezi kutumika tena, sababu ilishakamilisha majukumu yake.
Hivyo, tutachukua baadhi ya mambo mazuri kwenye rasimu ya Warioba, tutachukua baadhi ya mambo kwenye Katiba pendekezwa na kuyaunganisha na mawazo mapya ya wananchi ili tupate Katiba Mpya iliyo bora.”
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA MAJINA YA WALIOKUWA MAKAMISHINA WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA MPYA YA TANZANIA APRIL 6,2012.
Rais Jakaya Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba . Katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam April 6,2012 katika hafla iliyoshuhudia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani na badhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbali mbali.
April 6,2012 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza rasmi majina ya wajumbe walioteuliwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Kikwete aliyataja majina hayo mbele ya wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alisisitiza kwamba kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa. Ila kisheria tume ilitakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________
UONGOZI WA JUU
1.Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA
– Mwenyekiti
2.Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
RAMADHANI
– Makamu Mwenyekiti
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – BARA
1.Prof. Mwesiga L. BAREGU
2.Nd. Riziki Shahari MNGWALI
3.Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI
4.Nd. Richard Shadrack LYIMO
5.Nd. John J. NKOLO
6.Alhaj Said EL- MAAMRY
7.Nd. Jesca Sydney MKUCHU
8.Prof. Palamagamba J. KABUDI
9.Nd. Humphrey POLEPOLE
10.Nd. Yahya MSULWA
11.Nd. Esther P. MKWIZU
12.Nd. Maria Malingumu KASHONDA
13.Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)
14.Nd. Mwantumu Jasmine MALALE
15.Nd. Joseph BUTIKU
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – ZANZIBAR
1.Dkt. Salim Ahmed SALIM
2.Nd. Fatma Said ALI
3.Nd. Omar Sheha MUSSA
4.Mhe. Raya Suleiman HAMAD
5.Nd. Awadh Ali SAID
6.Nd. Ussi Khamis HAJI
7.Nd. Salma MAOULIDI
8.Nd. Nassor Khamis MOHAMMED
9.Nd. Simai Mohamed SAID
10.Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA
11.Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN
12.Nd. Suleiman Omar ALI
13.Nd. Salama Kombo AHMED
14.Nd. Abubakar Mohammed ALI
15.Nd. Ally Abdullah Ally SALEH
UONGOZI WA SEKRETARIETI
1.Nd. Assaa Ahmad RASHID
– Katibu
2.Nd. Casmir Sumba KYUKI
– Naibu Katibu
MJADALA JUU YA OFISI YA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA,WAJIBU WAKE NA MAHUSIANO YAKE NA KATIBA MPYA KATIKA FORUM YA KATIBA YA WATU JUNI 10,2023. MJADALA ULIENDELEA KWA MTOA MADA KUULIZA MASWALI MAWILI YA NYONGEZA
[17:18, 10/05/2023] AG:
Nimepitia majibu ya wadau juu ya Msajili na vyama vya siasa, lakini huku mtaani uhusiano wa siasa za Tanzania na Katiba mpya haueleweki, mara wanaharakati wanasema tusiwaachie wanasiasa, mara serikali itauvuruga, mara mchakato ni wa wananchi, bado najiuliza pengine si mimi tu…Siasa za Tanzania na Katiba mpya vina uhusiano gani na mlezi wake ni MSAJILI?
MAJIBU
Siasa za Tanzania na Katiba mpya zina uhusiano mkubwa kwani siasa za Tanzania zinaathiri mchakato wa kupata katiba mpya na maudhui ya katiba yana athari kubwa katika mfumo wa siasa za Tanzania.
Katiba mpya inatarajiwa kusimamia mfumo wa siasa za Tanzania, kwa kuainisha muundo wa serikali, utaratibu wa utawala, utengenezaji wa sheria, utawala bora, na mambo mengine yanayohusiana na utawala wa nchi.
Katiba mpya itasimamia haki na wajibu wa serikali na wananchi na itaimarisha demokrasia na utawala bora.
Siasa za Tanzania zina athari kubwa katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Viongozi wa siasa na vyama vya siasa wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maudhui ya katiba mpya na wanaweza kushawishi mchakato wa kupata katiba mpya. Pia, siasa za Tanzania zinaweza kuathiri upatikanaji wa rasilimali na ushiriki wa wananchi katika mchakato wa kupata katiba mpya.
Kwa hiyo, ili mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuwa na mafanikio, ni muhimu kwa siasa za Tanzania kuzingatia maudhui ya katiba na kusaidia kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa njia ya uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali wa kisiasa na kijamii.
TUNAULIZANA HAPA; Nini utofauti wa siasa za Tanzania na katiba ya Tanzania sasa?
Kuna tofauti kati ya Siasa na Katiba ya Tanzania lakn pia kuna uhusiano mkubwa wa siasa na katiba kwa nchi yeyote ile kama ifuatavyo;
1.Siasa ni mfumo wa kutawala au kusimamia mambo ya nchi ambao unahusisha shughuli za kisiasa kama vile uchaguzi,uteuzi wa viongozi wa serikali na maamuzi mengine ya kisiasa.Siasa inahusisha vyama vya siasa ambavyo vinashiriki ktk uchaguzi na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
2.Katiba ya Tanzania ni sheria kuu ambayo inaweka mfumo wa utawala,haki na wajibu wa raia na serikali na taratibu za kufanya maamuzi ya kisiasa.Katiba inaelezea Mamlaka na majukum ya vyombo vya dola kama vile,Mahakama,Bunge na Serikali.
3.Katiba pia inalinda haki na uhuru wa raia,na inatoa mfumo wa kudhibiti madaraka ya serikali.
Kwahiyo tofauti kuu kati ya Siasa na Katiba ni kwamba; Siasa inahusisha shughuli za kisiasa na Utawala wa nchi,wakati Katiba ni Sheria kuu inayoongoza shughuli hizo za kisiasa na utawala wa nchi.
Ahsante.
Mwl.Suleiman Ahmad
Usagara Sec
MJADALA JUU YA OFISI YA MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA,WAJIBU WAKE NA MAHUSIANO YAKE NA KATIBA MPYA KATIKA FORUM YA KATIBA YA WATU JUNI 10,2023
TUJADILI
WAJIBU WAKE NI NINI
MAJIBU
Mjumbe wa kwanza alitaja majukumu ya Msajiri wa vyama vya siasa
1. Usajili wa vyama vya siasa:
Msajili wa Vyama vya Siasa anawajibika kusajili vyama vya siasa vinavyotaka kufanya kazi nchini Tanzania. Vyama hivi vinatakiwa kutimiza matakwa ya kisheria kama vile kuwa na katiba na kanuni, na kuwa na wanachama wa kutosha.
2. Kusimamia shughuli za vyama vya siasa:
Msajili wa Vyama vya Siasa anasimamia shughuli za vyama vya siasa nchini Tanzania kuhakikisha kwamba vyama hivyo vinazingatia sheria, kanuni na taratibu za kisheria.
3. Kutoa ushauri na miongozo:
Msajili wa Vyama vya Siasa anatoa ushauri na miongozo kwa vyama vya siasa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa vyama hivyo.
4. Kufuta usajili wa vyama vya siasa:
Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kufuta usajili wa chama cha siasa endapo chama hicho kitakiuka sheria, kanuni na taratibu za kisheria.
Kwa hiyo, sheria hizi zinatajwa kuwa ni baadhi ya sheria zinazozorotesha uhuru wa vyama vya siasa nchini Tanzania, na zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu.
[12:22, 10/05/2023] J.Kiukweli Gap la msajili wa vyama vya siasa na mwananchii wa kawaida ni kubwa mno na kutokana na ukubwa huo unapelekea mtu wa kawaida nje ya chama cha siasa hahusiki juu ya msajili wa vyama vya siasa niombe ili mjadala uwe mzuri kwa wadau wote mwenye uelewa juu msajili uwepo wake kisheria atatusaidia wachache tusiojua ili tushiriki kikamilifu.
[12:23, 10/05/2023] T.Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imejikita katika usimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo na ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini. kwa vile wako hapa wote watatudadavulia vyema
[12:25, 10/05/2023] J.Kuletwa tu hapa na hao wajumbe wawili inatoa mwanya kuksanya Nondo kuujulisha umma yote tutayajadili mpaka kieleweke…Karibu
[12:36, 10/05/2023] J.Hii ni changamoto kubwa sana kwani wengi hawajui kabisa na wachache wanajua yupo mwenye cheo hiki cha msajili japo hawajui majukumu yake na kidogo wanajua kila kitu juu ya uwepo wake na chini ya sheria ipi hivyo haja ya kuwaelimisha wengi ni kubwa sana.
[13:17, 10/05/2023] A.Wataalamu wa sheria watatuongoza zaidi lakini nafikri kuna hatua mbalimbali ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kuboresha utendaji kazi wa Msajili wa vyama vya siasa nchini:
1. Kwanza, ni muhimu kufanya mabadiliko ya kisheria ili kuondoa upendeleo wowote wa kisiasa na kuimarisha uhuru wa vyama vya siasa
2. Ni muhimu kuimarisha utendaji wa Msajili kwa kumwezesha kufanya kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na mashinikizo yoyote ya kisiasa ikiwemo chama tawala
3. Ni muhimu kwa serikali kuhakikisha kuwa Msajili anapata rasilimali za kutosha kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hii inaweza kujumuisha kumpatia wafanyakazi wenye ujuzi na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kazi zake
[13:21, 10/05/2023] b:Jukumu la msajili wa vyama vya siasa katika mchakato wa katiba Tanzania kutokana na barua ya Rais ni lipi na mbona analalamikiwa sana huku mitandaoni. Anatakiwa aishie wapi msajili wa vyama vya siasa kutokana na barua ama maelekezo ya Rais?
MAJIBU
[13:42, 10/05/2023] S:Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais kwa Msajili wa Vyama vya Siasa,
Jukumu lake katika mchakato wa Katiba nchini Tanzania ni kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa ili kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichoratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Kwa msingi huo, Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu muhimu katika kuhakikisha kuwa wadau wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato huo wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania.
Pia, Msajili wa Vyama vya Siasa anatarajiwa kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambayo ni miongoni mwa sheria ambazo zinatarajiwa kufanyiwa marekebisho wakati wa mchakato wa kupata Katiba mpya.
[13:42, 10/05/2023] S: Kwa uelewa wanguNYONGEZA
[13:57, 10/05/2023] T:Ingawa barua hiyo haijatoa mpango kamili wa kazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, inaonekana kwamba ofisi hiyo ina jukumu kubwa katika kuhakikisha kuwa wadau wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania. Hapa chini ni baadhi ya mambo yanayoweza kufanywa na ofisi hiyo kulingana na barua hiyo:
1. Kuitisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa:
Kwa kufuata maelekezo ya Rais, Msajili wa Vyama vya Siasa anaweza kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kujadili na kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
2. Kuwashirikisha wadau:
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaweza kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wananchi, vyama vya siasa, taasisi za kiraia, na wadau wengine muhimu katika mchakato huo wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania. Hii itahakikisha kuwa maoni ya kila mmoja yanapewa kipaumbele na kuzingatiwa.
[13:58, 10/05/2023] T3. Kutoa maoni na mapendekezo: Msajili wa Vyama vya Siasa anatarajiwa kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria nyingine zinazohusiana na uchaguzi. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa sheria hizo zinaweka mazingira bora ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
4. Kutoa ushauri wa kitaalamu: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaweza pia kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau mbalimbali katika mchakato huo wa kutengeneza Katiba mpya. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa mchakato huo unafanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu zote zilizowekwa.
5. Kusimamia utekelezaji: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaweza pia kusimamia utekelezaji wa mapendekezo yote yanayohusiana na vyama vya siasa na uchaguzi. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa mabadiliko yanayofanyika yanatekelezwa kwa ufanisi na kwa njia ambayo inaweka mazingira bora ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
[13:59, 10/05/2023] Mt:Tufafanuliwe kwa kirefu na undani zaidi kuboresha hali ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, serikali inaweza kuchukua hatua?. kivipi wakati ndio chombo imekiunda yenyewe?
MASWALI YA ZIADA
[14:25, 10/05/2023] b:Sawaa Rais si kesha mpa jukumu Msajiri?na majukumu yake kama yalivyotajwa hapa,Rais Mama,Dr Samia afanye nini ili katiba mpya ipatikane maana kila sehemu Rais…rais na Mjumbe amewataja wananchi na jukumu lao kwa msajiri…
[14:26, 10/05/2023] H:Kama Rais katoa go ahead what’s the way forward? Wengine layman kidogo kwenye hii michakato
MAJIBU KWA MJUMBE B.
[14:36, 10/05/2023] S:Ili kuhakikisha kuwa mchakato wa Katiba mpya unafanikiwa na hatimaye kupatikana Katiba mpya nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kufanya mambo yafuatayo:
1. Kutoa msukumo na uongozi wa kisiasa: Rais anaweza kutoa msukumo na uongozi wa kisiasa kwa wadau wote katika mchakato wa Katiba mpya. Hii inamaanisha kuwa anaweza kushirikiana na wanasiasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuwa kila mtu anashiriki na anaonyesha mshikamano katika mchakato huu muhimu.
2. Kusimamia mchakato: Rais anaweza kusimamia mchakato wote wa Katiba mpya na kuhakikisha kuwa kuna uwazi na ushirikishwaji wa wadau wote. Hii ni pamoja na kufanya kazi kwa karibu na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge, wadau wa kisiasa na asasi za kiraia ili kuhakikisha kuwa mchakato unafanyika kwa njia ya haki na usawa.
3. Kuhamasisha mjadala wa kitaifa: Rais anaweza kuhamasisha mjadala wa kitaifa juu ya mabadiliko ya Katiba na kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru. Hii inaweza kufanywa kwa kuunda majukwaa mbalimbali ya majadiliano, mikutano ya hadhara na vikao vya wadau kuhakikisha kuwa kila mmoja ana nafasi ya kutoa maoni yake.
4. Kuzingatia maslahi ya umma: Rais anaweza kuzingatia maslahi ya umma na kuhakikisha kuwa mabadiliko yanayopendekezwa yanaendana na mahitaji na matarajio ya wananchi. Hii inamaanisha kuhakikisha kuwa Katiba mpya inaleta mageuzi ya kweli ya kisiasa na inakidhi mahitaji ya wananchi kwa kuzingatia utawala bora, uhuru wa kiraia na haki za binadamu.
Kwa kufanya mambo hayo, Rais Samia anaweza kusaidia kuhakikisha kuwa mchakato wa Katiba mpya unafanikiwa na kuleta mabadiliko chanya nchini Tanzania.
[14:42, 10/05/2023] A:Kwa kuongezea nyama kwenye nilichoelezea juu;
Kwanza, inaweza kufanya marekebisho ya sheria za vyama vya siasa ili kuondoa upendeleo wowote wa kisiasa na kuimarisha uhuru wa vyama. Kwa mfano, sheria zinaweza kurekebishwa ili kutoa uhuru kwa vyama vya siasa kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na serikali.
Pili, serikali inaweza kuhakikisha kuwa Msajili anapata rasilimali za kutosha kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hii inaweza kujumuisha kumpatia wafanyakazi wenye ujuzi, vifaa vya kutosha na rasilimali nyingine za kifedha ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.
Tatu, serikali inaweza kuimarisha utendaji wa Msajili kwa kuhakikisha kuwa anafanya kazi zake kwa uhuru na bila kuingiliwa na mashinikizo yoyote ya kisiasa. Hii inaweza kufanyika kwa kuhakikish…
[14:43, 10/05/2023] H:Kiongozi mimi nawaza tu,
1.Serikali kwanza ianzishe mchakato wa kutoa elimu kuhusu Kazi za Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kwa wananchi kupunguza huu mtanzuko uliopo.
2. Elimu ya Katiba kwa wananchi wote kwa ujumla inapaswa kutolewa ili kusaidia huu mchakato ili yaliyojitokeza kipindi kile yasijirudie
Huwezi kuandaa mchakato wakati walengwa wenyewe hawana idea yoyote ya kile kinachofanyika kwa kuwa kilichofanyika kipindi kile ni kuanzisha mchakato huku elimu inatolewa at per, misuguano mingi sana ilitokea mwisho wa siku tukafeli.
Kama inaweza kutoa fungu kwajili ya vitu vingine hata hili ni la msingi sana hivyo watoe pesa, waajiri vijana wasomi wawape mafunzo halafu wazunguke nchi nzima kutekeleza hayo majukumu hayo. Hao wasomi wasiwe wanasheria pekee maana hilo nalo tatizo kuja angle hutohitaji hao pekee watahitajika wataalam wa kada nyingine pia kwenye huo mchakato
MJADALA UNAENDELEA NA SASA WAMEKARIBISHWA MSAJIRI NA TIMU YAKE KUJIBU HOJA ZINAZOIBULIWA.
DR.SAMIA SULUHU HASSAN, AMEJITOKEZA KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA YA TANZANIA
Tangu alipoingia madarakani Aprili 2021 amefanya kazi ya kuunda tume ya kuchunguza mchakato wa Katiba iliyopita, na pia ameunda kamati ya kushauri juu ya mabadiliko ya Katiba ya sasa. Aidha, ameshiriki katika kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa ili kujadili mapendekezo ya Kikosi Kazi cha Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa.

Rais Samia pia ameweka bayana nia yake ya kufanya mabadiliko ya Katiba, kuhakikisha kuwa inaleta mageuzi ya kisiasa na kuhakikisha kuwa inawakilisha maoni ya wananchi. Hivi karibuni, Rais Samia amezindua mchakato wa kupata maoni kutoka kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba, akisema kuwa anataka kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo yanaungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania.

Kwa hiyo, ushiriki wa Rais Samia katika mchakato wa Katiba unaonyesha nia yake ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania na kuhakikisha kuwa wananchi wote wanashiriki katika mchakato huo.

Na sasa Mei 6 2023 amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa.Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Turne ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa
























